Saturday, February 23, 2013

MAGAIDI WAMUUWA IMAMU WA MSIKITI WA MWAKAJE-NCHINI ZANZIBAR.


HAWA KAZI YAO NINI..?KULA,KUVIMBA,NA KUWA NA VYEO MPAKA MABEGA YANAUMA KWA VYEO AU SIO..?

SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri Evarist Gabriel Mushi na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi kichwani eneo la Beit el Raas, Jana Imamu wa Msikiti wa Mwakaje amefariki dunia baada ya kupigwa mapanga hadi kufa na magaidi wasio julikana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya saa 8 mchana na kumtaja aliyefariki ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.
Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada alisema tukio hilo limetokea baada ya Sheikh Khamis kwenda shambani kwake katika shmba la minazi Kidoti ambapo wakati akiwa shambani hapo ndipo walipotokea watu kadhaa na kumpiga mapanga sehemu za shingoni mwake na kusababisha kifo chake muda mfupi baada ya kipigo hicho.
Alisema baada ya tukio hilo, watu walimchukua na kumkimbiza hospitali lakini kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki dunia wakati akiwa njiani na hivyo harakati za mazishi zinafanyika za kumzika baada ya kuchukuliwa vipimo vya wataalamu wa afya.
Kamanda Ahmada ametoa wito kwa wananchi kutopuuzia taarifa za watu ambao wanawashuku na wenye kuleta maafa yakiwemo mauaji hapa nchini, kwani kuwaficha wahalifu ni kuendeleza utamaduni usiofaa katika jamii ambayo imeanza kuharibika kutokana na mauaji hayo yanayoendelea kila kukicha.
Hili ni tukio la tano kwa viongozi wa dini kuhujumiwa ambapo tukio la kwanza Sheikh Fadhil Suleiman Soraga kumwagiwa tindi kali na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya wakati akifanya mazoezi nyakati za asubuhi karibu na nyumbani kwake Magomeni, tukio la pili ni lile la sheikh farid hadi kutekwa na watu wasio julikana na la tatu ni la Padri Ambrose Mkenda aliyepigwa mapanga shingoni na kurejuhiwa vibaya na watu wasiojulikana wakati akitaka kuingia nyumbani kwake huko Tomondo Mjini Unguja. matukio hayo matatu yalitokea mwaka jana.
Katika mwaka huu nako kumetokea matukio mawili kwa kuuwawa kwa Pardi Evarist Mushi huko Beit El Raas wakati akitaka kuingia Kanisani na pia kuuawa kwa Sheikh Ali Khamis huko Kidoti shambani kwake Mkoa wa Kaskanizini Unguja.  Inna lillahi wainna ilayhi rajiiun.ina bidi sasa serekali ya GNU-SMZ pia ikaite CIA nchini marekani waje wachunguze maana hichi ni kitendo cha KIGAIDI cha kuliwa IMAMU akiwa shambani kwake kujitafutia riziki lazima MAGAIDI hawa walio muuwa imamu wasakwe na wafikishwa katika vyombo vya sheria.tunaiomba serekali ya GNU-SMZ kuchukuwa hatuwa maramoja ya kuwaita CIA kuja hapa nchini zanzibar na kuchunguza ili waweze kujulikana hawa MAGAIDI WALIO MUUWA IMAMU na wakamatwa MAGAIDI hao na kuhukumiwa.

No comments:

Post a Comment