Tuesday, December 31, 2013

TUTA FIKE TU WANA WA MAMLAKA KAMILI


WAKOMBOZI NA WAASISI WA MARIDHIANO YA NCHI YETU YA ZANZIBAR NDIO HAWA MAALIM SEIF NA KARUME

Kwanza niaze kutoa pongezi zangu kwa wazanzibar wote wenye kutaka mamlaka kamili ,Kitendo cha Warioba kutangaza tu hadharani kwamba asilimia 60 ya Wazanzibari walitaka Muungano wa Mkataba peke yake ni ushindi mkubwa kwa kila mzanzibar mwenye kuipenda nchi yake.
Niseme wazi kwamba wazanzibar sasa tumepiga hatua moja kubwa mbele leo hii,lakini pia kinachotakiwa hatutakiwi kuonesha hisia kama sasa tumefanikiwa safari ndio kwanza inaanza,kinachotakiwa hivi sasa ni kuendelea na harakati ambazo zifanyike kwa njia ya amani na kidemokrasia kukamilisha mambo yaliobakia.
Lakini pia wale wote wanaosema tumekosa hiki au kile kwa hatua hii warudi kwenye historia ya Mkataba wa Hudaibiya ambapo mengi yalikosekana lakini hatimaye kupitia Mkataba huo ambao awali baadhi ya Maswahaba walimbeza Mtume (s,a,w)kwa kukubali kwake mkataba huo kwani ulionekana kama wenye sura ya kuwakandamiza Waislamu lakini mwisho wake ukapatikana ukombozi wa Makka kwakutokana na makafiri kushindwa kutimiza makubaliano ya mkataba huo wa hudaibiya.
Kutokana na kisa hichi ni wazi kabisa wazanzibar tunatakiwa kujifunza,kuwa na subra na uvumilivu wa hali ya juu huku tukiendeleza harakati zetu kwa njia ya amani kuhakikisha tunayashika yale yote yaliobakia kutoka katika orodha ya muungano huu feki unao ila nchi yetu ya Zanzibar.
Ikiwa tutaendelea kushikamana na kuwa wamoja bila ya kubaguana basi ukombozi wa Zanzibar unakuja karibuni Inshallah.

No comments:

Post a Comment