Rais wa nchi ya Tanganyika, Jakaya Mrisho Kikwete amewashauri watu wanaopanga kulipa kisasi pindi watakapopata madaraka kuachana na mawazo hayo.
Rais Kikwete ametoa ushauri huo wakati akitoa hotuba yake kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa nchi ya Tanganyika, ambapo ameelezea mengi mazuri aliyoyafanya rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na kuwataka viongozi wa nchi ya Tanganyika kuiga mfano wa maisha yake ikiwa ni pamoja na kusamehe na kusahau bila kulipa kisasi.
“Najua kuna wengine hapa wamepanga kulipa kisasi, wanasema nikipata watanikoma.” Amesema rais Kikwete na kuwataka waache yaliyopita yapite na kuendelea kuganga yajayo, “acheni kulipa kisasi.” Rais Kikwete amesisitiza.
Hotuba ya Rais Kikwete ilijikita zaidi katika maisha ya mzee Nelson Madiba Mandela, katika kuungana na Afrika Kusini kuomboleza kifo cha kiongozi huyo shupavu na kutoa mfano wa jinsi viongozi wa Afrika wanapaswa kuiga mfano wa uongozi.
WAZANZIBARI TUNAKULIZA JE BENJAMEN MKAPA NA YEYE ASAMEHEWE KWA KUWAKATA WAZANZIBARI ROHO ZAO MBICHI 26/27...???
KAMA MNATAKA TUSILIPE KISASI BASI TUPENI NCHI YETU YA ZANZIBAR MUSIJIDAI KUTUPOZA NA KATIBA LENU LA UWONGO HATUNAHAJA NA KATIBA ZANZIBAR INA KATIBA YAKE TUPENI NCHI YETU TU BASI.
BAADA YA KUTUPA NCHI YETU TUTAWAULIZA WANANCHI WA ZANZIBAR KAMA WANATAKA KUWASEMEHE AU LAA TUKI WAULIZA WAKISEMA HAWAJAWASAMEHE NA TUKIGUNDUWA MAUWAJI YOTE YALIYOFANYA ZANZIBAR KUANZIA 1964 MPAKA 2015 NI YA MAKSUDI KWA MASLAHI YENU BASI LAZIMA TUWAWAJIBISHE,WALE WOTE WALIO WAUWA WAZANZIBARI HAKUNA CHA MSAMAHA,CHA MSINGI SIASA ZA UBAGUZI NDIO ZIPIGIWE MFANO HUKO AFRIKA YA KUSINI.
No comments:
Post a Comment