Friday, December 27, 2013

ASKOFU DAMIANI DALLU ACHANGANYA DINI NA SIASA (AKEMEA UTANGANYIKA AHOFIA MUUNGANO)


MUBAKI NA TANGANYIKA YENU MUENDELEZE ULANISI WENU HUKO HUKO TANG

ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita, Damiani Dallu amekemea vuguvugu la watu wanaotaka kuirejesha NCHI YA TANGANYIKA katika siasa za Muungano.
Akizungumza kwenye Ibada ya Sikukuu ya Krismas Geita jana, Askofu Dallu alisema Tanganyika iliishi kwa muda mfupi mpaka mwaka 1964 na baada ya hapo kwa miaka 50, imekuwepo Tanzania:
“Hao wanaoitaka Tanganyika nawashangaa…kama wanataka kutoka  watoke…sisi tutatangulia mbele tukiwa Watanzania,” alisema Dallu.
Alisema katika Afrika si kitu cha ajabu kwa nchi kubadilisha jina baada ya kupata uhuru na kuhoji: “Ni nani ambaye jina analoitwa leo alizaliwa nalo?,” aliongeza:
“Nchi nyingi za Afrika zimebadilisha majina yake ya zamani…hii haiwafanyi eti wasisherehekee uhuru siku waliyoupata…Tuache upuuzi tujenge nchi yetu Tanzania hata kama wenzetu katika Muungano walibaki na jina lao,” alisema Dallu.
Alizitaja nchi za Malawi, Msumbiji, Ghana, Zimbabwe na Zambia ambazo majina yake ya awali hayakuwa hayo, lakini bado zinasherehekea uhuru wao kwa muda waliyoupata.
Alisema ni kawaida katika jamii kuwa na watu watakaojitokeza kupinga mambo na watu hao huwa chachu ya kufanya mageuzi ya kweli.
Askofu Dallu, pia alitaka Watanzania kumuomba Mungu, ili kupata Katiba ambayo itaendeleza furaha ya kweli, iliyodumu kwa miaka 52 sasa.
Naye, Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaa, Mhashamu Titus Mdoe alitaka Watanzania wenye nyadhifa za uongozi kuwa na hofu mbele ya Mungu, na kuacha vitendo vya kinyama na udhalilishaji dhidi ya binadamu wenzao.
Askofu Mdoe alisema hayo kwenye mkesha wa Krismas katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, na kuongeza kuwa umefika wakati kwa viongozi hao kujitoa kwa ajili ya maisha ya watu na si yao binafsi.
Alisema wapo baadhi ya watu wenye nyadhifa (viongozi) wanaojiona ndiyo kila kitu kwa wenzao na kujiona kuwa ndiyo wenye haki ya kuwafanyia wengine kila ubaya, bila kujali kuwa nao ni binadamu wanaostahili haki kama wao..
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA TUNAKUAMBIA DALLU TANGANYIKA NDIO BABA YENU NA MAMA YENU, WASWAHILI WANASEMA MKATA KWAO MTUMWA , SIO WATANGANYIKA TU HATA SISI WAZANZIBARI HATUTAKI TENA KUWA NA NYINYI WATANGANYIKA MSHATUUWA SANA SIKU ZA CHAGUZI,MSHATUIBIA SANA MPAKA MEETUTIA UFUKARA KILICHOBAKI SASA NI KUWA WAZANZIBARI TUNATAKA WENYEWE KILE KIBWAGIZO CHETU NA NYINYI MUCHUKUWE CHENU CHA TAN-TANGANYIKA , NA SIS TUCHUKUWE CHETU CHA ZAN-ZANZIBAR TUNATAKA ZAN YETU TIMECHOSHWA NA NYINYI MITANGANYIKA.
KIKWETE JE UTAFUNGA JELA ASKOFU DALLU KWA KUCHANGANYA DINI NA SIASA KAMA ULIVYO MFUNGA SHEIKH MPONDA NA MASHEIKH WETU WA UAMSHO HUKU ZANZIBAR AU UTAMUACHIA ASEME ANAVYO TAKA MAANA NDIO WAO WALIOKUWEKA HAPO KATIKA KITI CHA URAISI WA TANGANYIKA...????

No comments:

Post a Comment