Tuesday, October 14, 2014

MH MANSOUR YUSSUF HIMID ANGURUMA KIBANDA MAITI NCHINI ZANZIBARZANZIBAR KWELI NI JEMAA NDIO MAANA MAHASIDI WANATKA KUIFISIDI

MAELFU YA WAZANZIBARI WALIO HUDHURIA MKUTANO WA KIBANDA MAITI NCHINI ZANZIBAR

Mjumbe wa kamati ya maridhiano na mshauri wa katibu mkuu wa Chama cha wananchi CUF Mh.Mansour Yussuf Himid amesema ataendelea kuitetea nchi ya Zanzibar kwa hali na mali mpaka ahakikishe nchi ya Zanzibar inapata mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa.
Mansour aliyasema hayo katika mkutano mkubwa wa aina yake wa Chama cha wananchi CUF uliofanyika viwanja vya kibanda maiti mjinu Unguja nchini Zanzibar.
Mansour alieleza kwamba ataendelea na msimamo wake wa kupinga muungano huu uliopo mpaka siku ya kiama kwani ni aina ya muungano uliojaa ukatili kwa wananchi wa nchi ya Zanzibar.
Aliwataka Wazanzibar kuelewa kwamba kwa mujibu wa vitabu mbali mbali vya dini ni wazi kabisa kuwa kila mmoja wetu atakufa hivo hakuna haja ya kuogopa kwa kuitetea nchi yao.
Pamoja na hayo aliwata wananchi wote wa nchi ya Zanzibar bila ya kujali itikadi zao kuikataa katiba iliopitishwa na Bunge maalumu la katiba kwani haikukidhi vigenzo wala matakwa ya wananchi wa nchi ya Zanzibar kufuatia maoni yao waliotoa kwenye tume ya Jaji warioba.
Mkutano huo wa CUF uliofanyika kibanda maiti nchini Zanzibar hudhuriwa na maelfu ya watu wa mikoa yote ya Unguja walihudhuria kuja kujuwa hatma ya nchi yao wanayo ipenda ya Zanzibar.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment