HAWA WASHEREHEKEA KUIYUWA NCHI YA ZANZIBAR NA KUIGEUZA KUWA MOJA KATIKA MITAA YA NCHI YA TANGANYIKA.
NA SISI TUNASEMA MUTAITOWA NCHI YETU YA ZANZIBAR MUKITAKA MUSITAKE MPAKA KIELEWEKE ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA ZANZIBAR KWANZA
TUACHIWEE TUPUMUWEEE TUACHIWEE TUPUMUWEEE TUACHIWEE TUPUMUWEEE
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba (BMK), Samuel Sitta,Saba,Nane na Tisa ameendelea kubanwa baada ya Jukwaa la Katiba (Jukata), kudai kura nyingine iliyopigwa kwa ajili kuhalalisha theluthi mbili za nchi ya Zanzibar ilichakachuliwa kutokea kwa wajumbe wa bara.Mwishoni mwa wiki, mmoja wa wajumbe wa bunge hilo kutoka Zanzibar, ambaye ni Makamu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Haji Ambari Khamis, aliwaambia waandishi kwamba hakupiga kura lakini jina lake lilichomekwa ili kulazimisha upatikanaji wa theluthi mbili ya Wazanzibari.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika jana, Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba, alisema wakati wakifanya uchambuzi linganifu wa katiba iliyopo ya mwaka 1977, rasimu ya pili ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba na Katiba pendekezwa, walibaini mjumbe wa BMK, Zakia Meghi mwenye namba 149 amepiga kura kama mjumbe wa nchi ya Zanzibar wakati ni kutoka nchi ya Tanganyika.
“Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa majina ya makundi yote ambayo yatashiriki BMK na baadaye tangazo la gazeti la serikali la Februari kuweka bayana makundi hayo…mjumbe Zakia Meghi jina lake lilikuwa upande wa nchi ya Tanganyika na ndiko anakofanyia shughuli za siasa.“Katika Katiba pendekezwa namba 149, Zakia Meghi amesaini kupigia kura ya nchi ya Zanzibar wakati yeye ni mjumbe wa nchi ya Tanganyika, anatuambia kuwa amepiga kura feki …kapiga pasipo husika kwa kuwa kila mfuatiliaji wa masuala ya siasa anafahamu kuwa mwanasiasa huyu yuko nchini Tanganyika muda mrefu hata kutambuliwa na Rais Kikwete hivyo,” alisema.Kibamba, alisema kutokana na udanganyifu huo uliofanywa na Sitta kumruhusu Meghi kupiga kura upande usio wake na wakati huo huo mjumbe NCCR-Mageuzi kutoka nchi ya Zanzibar, Haji Ambar Khamis kulieleza mbele ya waandishi kuwa alisingiziwa kupiga kura nambari 39 katika ukurasa wa 209 zote ni feki.
Aidha, Mwenyekiti huyo, alisema Jukata imesikitishwa na vitendo vya wajumbe wa BMK na viongozi wake kuvunja maadili ya Kitanganyika na ya Kizanzibari kwa mujibu wa katiba iliyopo, waliposerebuka kwa kukata viuno na kubanana wanaume na wanawake kusherehekea ushindi wa kupata theluthi mbili ya nchi ya Zanzibar.“Bunge lolote likiwa katika vikao linakuwa katika sehemu muhimu ya kufanya maamuzi ya wananchi, lakini tulisikitika pale tulipoona wajumbe wanaserebuka hata kupoteza maana ya maadili kwa wajumbe wa kike na kiume kukata viuno na kubanana hadharani …Jukata tumesikitishwa sana na tukio hilo,” alisema.Akizungumzia yaliyomo katika Katiba pendekezwa, Kibamba alisema kilichofanywa na wajumbe wa BMK katika siku zote walizokaa bungeni, walitoa masuala muhimu na kufifisha hoja zilizobaki, ambazo alidai ziliandaliwa kwa umakini katika rasimu ya Jaji Warioba.
Alisema kazi ya kufifisha hoja hizo, ilifanywa na genge la watu wachache kwa maslahi yao, ambao mara nyingi ndiyo humpotosha Rais na kuwachanganya Wananchi ili washindwe kufanya maamuzi magumu ya nchi kwa ajili ya Watanganyika na Wazanzibari kwa ujumla na Taifa kwa jumla.Kibamba, alikwenda mbali zaidi na kusema, genge hilo hilo ndilo sasa linalomshawishi Rais Kikwete afikirie na kutangaza ndani ya siku 84, tarehe ya kupiga kura ya maoni kukubali au kukataa Katiba inayopendekezwa ili waweze kunufaika zaidi.“Watanganyika na Wazanzibari wote tunajua kuwa kura ya maoni ya kupitisha Katiba pendekezwa itapigiwa kura mwaka 2016… hii ni kwa mujibu wa makubaliano kati ya Rais Kikwete na Viongozi wa Kituo cha Demokrasia Nchini (TCD), walipokutana hivi karibuni,” alisema.Mwenyekiti huyo wa Jukata, alisema genge hilo kama litaendelea kumlazimisha Rais Kikwete akubali Waatanganyika na Wazanzibari wapige kura tofauti na makubaliano, atakuwa analazimisha machafuko yasiyo ya lazima.
Aidha, alisema Katiba pendekezwa imeongeza ukubwa wa serikali hususan tume, kutoka nne kwa katiba ya sasa hadi 12 na kuweka uwezekano wa kuanzisha tume za kisekta zisizo na idadi, hivyo kufanya mzigo wa uendeshaji wa serikali kuwa mkubwa.Kuhusu uwiano wa kijinsia, Kibamba alisema Katiba inayopendekezwa imeondoa matumaini ya kufikia usawa kamili wa kijinsia kwa mfumo wa uwazi kama ilivyokuwa katika Katiba ya 1977 ambao ni asilimia 30. Rasimu ya Jaji Warioba ilipendekeza 50/50 kuingia jimboni.Alisema kwa sasa hakuna mfumo rasmi na kuondoa fursa za uteuzi wa Rais wa wabunge 10 huku watano wakiwa wa kike, kuondoa uteuzi wa wawakilishi watano kutoka Zanzibar, ambako wawili ni wa kike na fursa zingine za kijinsia kubanwa.
“Natoa rai kwa wanawake wote nchini, ambao walidhani wamepewa pipi na BMK walambe kwa kuwekewa 50/50, kumbe hakuna walichowekewa…nawaomba watenge muda wao, watulie na kusoma Katiba pendekezwa, iliyopo ya 1977 na rasimu ya Jaji Warioba kisha washangilie,” alisema. Alisema mwonekano wa Watanganyika na Rais Kikwete wa kuwapo kwa Katiba mpya ambayo ingeondoa kero za Watanganyika na Wazanzibari na kuifanya idumu kwa mika 50 au 1000 ijayo bila kuhitaji marekebisho makubwa au katiba nyingine, limeshindwa kutimia. Hata hivyo, Kibamba alisema ili kufanikisha uelewa wa wananchi kuhusu Katiba pendekezwa, Jukata linaiomba serikali na wadau wengine kuchapisha nakala za kutosha ili kila mtanganyika anayetaka kuifahamu Katiba pendekezwa, aweze kufanya hivyo bila kikwazo.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment