Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Kisonge na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi wa Zanzibar wasikubali kugawiwa kutokana na mchakato wa Katiba unaoendelea
Akihutubia maelfu ya wana CCM na wananchi wa Zanzibar katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika viwanja vya Demokrasia Kibandamaiti mjini Unguja, Dk. Shein alisema wananchi wote waliridhia na kushiriki mchakato huo hivyo hakuna sababu ya kugawanyika baada ya Bunge la Katiba kupendekeza Katiba Mpya.
Alisisitiza kuwa mchakato wa Katiba kamwe usiwagawe wananchi wa Zanzibar na badala yake waendelee kudumisha amani na utulivu uliopo na kamwe wasikubaliane na viongozi wasioitakia mema Zanzibar.
Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa anashangazwa na viongozi wa Chama cha Wananchi-CUF kwa kuikataa katiba wakijua kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maslahi ya Zanzibar na watu wake.
“Napata mas
haka na viongozi wa CUF kama kweli wanataka maendeleo ya Zanzibar kwa kuwa tulipigania wote suala la mafuta na gesi liondolewe katika mambo ya muungano na Katiba inayopendekezwa imefanya hivyo sasa wanachokataa ni nini?”Alihoji Dk. Shein.
“Napata mas
haka na viongozi wa CUF kama kweli wanataka maendeleo ya Zanzibar kwa kuwa tulipigania wote suala la mafuta na gesi liondolewe katika mambo ya muungano na Katiba inayopendekezwa imefanya hivyo sasa wanachokataa ni nini?”Alihoji Dk. Shein.
Katika mnasaba huo aliwataka wananchi kuwa makini na viongozi wa chama hicho wanapokwenda kwao kuzungumzia suala la Katiba mpya kwa kuwa hoja zao zimekwisha ilichobaki ni kuwadanganya na kamwe wasikubali jambo hilo.
Alisema wananchi wa Zanzibar wana kila sababu za kuipigia kura ya ndio Katiba hiyo wakati utakapofika kwa kuwa inaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na serikali yao katika kuiletea nchi maendeleo ikiwemo suala hilo la kuendeleza wa sekta ya mafuta na gesi.
Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa Katiba inayopendekezwa imezingatia maslahi ya Zanzibar kwa ukamilifu wake na kufafanua kuwa masuala yote yaliyokuwa yakiitwa kero za muungano yamepatiwa ufumbuzi.
Aliwapongeza viongozi mbalimbali waliotoa maelezo ya vifungu mbalimbali vya Katiba hiyo ambavyo vinaonesha jinsi maslahi ya Zanzibar yalivyozingatiwa katika Katiba hiyo ikiwemo fursa mbalimbali itakazopata Zanzibar endapo Katiba hiyo itapitishwa. Alimpongeza piaMzee Hamid Ameir kwa kuvunja ukimya na kueleza juu ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964
Dk. Shein alisema kuwa mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania si jambo la kukurupuka bali ni suala la muda mrefu ambapo yeye pamoja na Rais Jamhuri wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete walishauriana wakati wote na kuwakumbusha wananchi kuwa suala hilo mwanzoni lilitakiwa na upinzani wenyewe.
Katika mkutano huo Dk. Shein aliwahakikishia tena wananchi hao kuwa Zanzibar ilishirikishwa na kushiriki kikamilifu katika mchakato huo tangu mwanzo hadi hatua iliyopofikia sasa kwa kuzingatia sheria ya mabadiliko ya Katiba pamoja na taratibu nyingine zilizowekwa.
Rais wa Kisonge na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliwataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi kutembelea kifua mbele kutokana na Serikali yake kutekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Alirejea kauli yake kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo chini mfumo wa Umoja wa Kitaifa inatekeleza Ilani ya CCM ambayo ndio iliyoshinda uchaguzi na kuwa masuala yote hayo ikiwemo mchakato wa Katiba umewashirikisha vingozi wote katika Serikali hiyo.
Dk. Shein aliwahakikishia wana CCM na wananchi wa Zanzibar kuwa chama hicho kitashida uchaguzi wa Mkuu ujao kwa kishindo na kuongeza kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa chama cha CUF.
“Ushindi wa CCM uchaguzi ujao hauepukiki na huo ndio utakuwa mwisho wa CUF na hawatakuwa na kisingizio” alisema Dk. Shein na kuwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi ujao utakuwa wa kidemokrasia zaidi kuliko chaguzi zilizopita.
Nae Balozi Seif Idd alimshangaa kiongozi mkubwa wa chama cha CUF kumwita msaliti na kusema kuwa msaliti ni yeye ambaye amewatoa Wajumbe wa Katiba hiyo ambayo ilikuwa inawatetea Wazanzibari.
Alisema kuwa Wajumbe wa CCM wa Bunge la Katiba lililopita wamemtetea Rais wa Zanzibar ambapo kwenye Ibara ya 96 inaonesha wazi Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nayo risala ya WanaCCM wa Mikoa minne ya Kichama ya Unguja ilitoa shukurani kwa Wajumbe wote wa CCM katika Bunge la Katiba na kueleza kuwa kazi kubwa na ya thamani wameifanya viongozi hao katika kuimarisha Muungano pamoja na kuenzi Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Risala hiyo, ilieleza kuwa licha ya kuwepo kwa wapinga Mapinduzi hapa nchini ambayo kila siku wamekuwa wakiaandaa mbinu mpya za kuyahujumu Mapianduzi hayo kamwe hawatofanikiwa.
Aidha risala hiyo ilieleza kuwa kazi ya kuyalinda Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ni endelevu na inamuhusu kila mwana chama CCM na kumpongeza Dk. Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na kusisitiza kuwa Muungano utaendelea kuwa imara.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment