Thursday, October 30, 2014

LUKUVI ALISEMA WAZANZIBARI %95 NI WAISLAMU TUNATAKA WAJITANGAZEYE SEREKALI YA KISLAMU KULE..? MNAJUWA MADHARA YAKE..? WALE WAARABU WATARUDI WATAZALISHA SIASA KALI KULE WATAKUJA KUTUSUMBUWA AMII LUKUVI YAKHEE WACHA UCHEEPE UKO OMAN SASA WALA KUKU AU HUKO NI ARUSHA..?


LUKUVI WAARABU HAWAKURUDI NAONA UMEWAFUATA MWENYEWE SHAABAASHI
IMG-20141023-WA0000
LUKUVI AMIII USHAKULA HARUWAAA NA CHAI YA MAZIWA........?

FANYA MCHEZO NA HELA WEYE MAKINDA KAVA BUIBUI MWENYEWE NA MTANDIO
WILLIAM Lukuvi ambaye ni Waziri wa Nchi ya Tanganyika na Aduwi mkumbwa wa Wazanzibari na Uislamu amejikuta akikolewa na utamu na kujikuta ananyenyekea kama mbwa aliye ruwa na mvua,Lukuvi pia ni Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu na Bunge), ametokea kuwa mtu mwenye sura mbili kisiasa! Sura ya kwanza ni unafiki wa kisiasa na sura ya pili ni woga unaotokana na adui asiyekuwapo.
Mtazamo huu juu yake unaanzia pale alipoamua kuhutubia (kanisani) na kuonesha wasiwasi wake juu ya wale wanaodai serikali tatu wakati Bunge Maalum la Katiba (BMK) lilipokuwa linaendelea Giningi Dodoma nchini Tanganyika.
Tarehe 12 April, 2014; mjini Giningi Dodoma nchini Tanganyika, Lukuvi alimwakilisha Waziri Mkuu kwenye hafla ya kutawazwa Askofu wa Kanisa la Methodist, ndipo alipotumia nafasi hiyo kutimiza na kutowa chuki zake,uwaduwi wake,uhasidi wake fikra zake katika kuonesha sura yake ya kwanza, yaani wasiwasi, woga na hofu kuu!!! iliyo mjaa ndani ya moyo wake
Pamoja na mambo mengine, Lukuvi akihutubia kwenye hafla hiyo alisema: Wazanzibari kule waliko asilimia 95 ni Waislamu, tunataka wajitangazie serikali ya kiislam kule..?? Mnajua madhara yake..?? Wale Waarabu watarudi, watazalisha siasa kali kule, watakuja kutusumbua..!!
Lukuvi alionesha hofu kuu (phobia) juu ya madai ya serikali tatu zilizodaiwa na baadhi ya wananchi na maoni hayo kuratibiwa na tume ya mabadiliko ya katiba (TMK) na kuwekwa kwenye rasimu ya katiba (2013).
Alidai kwamba, lazima waing’an’anie Zanzibar kwa kuwa ni kisiwa na visiwa vinasumbua sana kwa kuwa haiwezekani kujua kitu gani kitaingia na kitaweza kufika bara (maana yake, Tanganyika). Huu ni wasiwasi, woga na hofu kuu kwa mtu aliyepoteza mizania halisi kiakili na kimantiki..!!!
Kwa dhana hii; wasiwasi, woga na hofu kuu (phobia) kwa Lukuvi ni juu ya kurudi kwa Waarabu nchini Zanzibar...!!! Inaweza kuwa ni kichekesho; lakini, chambilecho waswahili, acha tuweke akiba ya maneno.
Lukuvi anawaogopa Waarabu ati watarudi nchini Zanzibar..!!! Ndio hoja yake..!!! Baada ya shutuma, zilizotolewa na baadhi ya wajumbe wa BMK hususan kutoka kwa kundi la Ukawa juu ya hotuba aliyoitoa kanisani, tarehe 17 April 2014, Mwenyekiti wa BMK alimpa Lukuvi takriban dakika 32 kujibu yalioitwa mapigo..!!!
Katika majibu yake, Lukuvi alionesha sura ya pili, japokuwa aliahidi angalitumia nafasi aliyopewa kurasmisha aliyoyasema mtaani (kanisani). Hata hivyo, Lukuvi alisahau alichosema kule mtaani..!!! Kanisani alionesha wasiwasi, woga na hofu kuu. Lakini, kwenye BMK alisema; kwa tabia yake yeye huwa haogopi na sio mnafiki kama walivyozoea watu wengine kwa ahadi kwamba atasema vilevile ili siku nyingine watu wamkumbuke kwamba alivyosema ni kweli..!!!!!
Hapa, kwa mantiki Lukuvi alisahau kwamba tayari alishatanguliza wasiwasi, woga na hofu kuu juu ya serikali tatu; kurudi kwa Waarabu; na kuporomoka kwa serikali ya muungano na madhara yatakayotokana na hali hiyo.
Huu ni wasiwasi, woga na hofu isiyokuwa na ushahidi wowote wa kiakili na kiintelijensia..!!! Uko wapi ushahidi wa visiwa kusumbua duniani, kama tukichukua nchi zinazopaka na bahari kuu! Kwani nchi za Rwanda na Burundi kulikotokea sintofahamu na songombingo iliyotuhatarishia amani yetu na usalama wetu miaka ya 1990, ni visiwa....??
Pamoja na woga na hofu kuu aliyokuwa nayo Lukuvi juu ya kurudi kwa Waarabu nchini Zanzibar; hususan wale waliyoitawala nchi hiyo kabla ya mapinduzi, ushahidi umeonesha dhahiri kwamba Lukuvi alikuwa na sura mbili zisizokuwa na mashiko.
Katika mazingira ya kuonesha ushahidi wa hili, ndani ya mwezi wa Oktoba, 2014 yeye na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika walikwenda Oman kwa ziara maalum kiofisi.
Lukuvi, akiwa miongoni mwa wajumbe wa ziara hiyo, alikuwa mstari wa mbele hata kuvaa kanzu (kama wavaavyo Waislam)! Huyu ndiye yule aliyetangaza wasiwasi, woga na hofu juu ya kurudi kwa Waarabu...!!!!! Je, Lukuvi kwa kwenda kwake Oman kama waziri ni busara kudhani kwamba alikwenda kuwafuata watawala wa zamani wa Zanzibar ili warejee.....?? Kama anawaogopa sana Waarabu juu ya siasa kali, alifuata nini Oman.....???
Hizi ni sura mbili za mtu mmoja...!!! Na kwa mujibu wa falsafa ya sura mbili, ni kwamba; mtu huyo ni mwovu lakini anajifanya mwema na rafiki (mnafiki au mzandiki)! Unafiki ni sifa mbaya kwa kiongozi wa umma.
Kama Lukuvi anawaogopa Waarabu waliotawala Zanzibar, kisha yeye anakwenda huko huko walipo na kuwacheza shere hata kwa kuvaa mavazi yanayofanana na Wao Waoman; huu ni nini kama sio unafiki...???
Katika kulitazama hili, na yale yaliyotokea Dodoma kwenye BMK, hadi pale wajumbe waliyo wengi walipopitisha katiba inayopendekezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni dhahiri kwamba Lukuvi alikuwa na dhana hasi iliyojificha hata kufika kutumia hafla ya kutawazwa kwa askofu kuitimiza hofu kuu (phobia) kwa mambo yasiyokuwa na mashiko ya kiakili na au kimantiki.
Lukuvi alikuwa na agenda ya siri na iliyoratibiwa kimkakati na sio wasi wasi, woga na hofu ya kurudi kwa Waarabu..!!! Kama ingalikuwa hivyo, angaliogopa kwenda Oman hata kama kulikuwa na ulazima huo.
Kinyume chake, Lukuvi alikuwa anatumikia mkakati uliyompeleka kwenye hafla ya kidini katika kutafuta uungwaji mkono wa itikadi ya uhafidhina na ukiritimba wa chama chake katika kufanikisha mchakato wa kupitisha serikali mbili kwa utashi wa CCM Chukua Chako Mapema.
Na kwa vyovyote viwavyo, wasi wasi, woga na hofu kuu kwa Lukuvi ilikuwa ni undumilakuwili ulioatamizwa kwa unafiki na uzandiki katika kutafuta uungwaji mkono na kundi la kiitikadi kwa mtazamo wa kimaslahi zaidi kuliko ujenzi wa jamii ya watu waliyo sawa na huru.
Lukuvi ni mbaguzi mwenye maslahi binafsi zaidi kuliko utumishi wa umma uliyotukuka. Ni kiongozi hatari kwa jamii ya watu wenye mitazamo tofauti ya kiimani. Viongozi wa aina hii hawafai kwa mustakabali wa taifa, kwa kuwa wanasababisha mpasuko wa jamii!
WAJINGA NI SISI WAZANZIBARI TULIO TIWA SUMU NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA TUWACHUKIE DUNGU ZETU WA OMAN WAKATI WAO WATANGANYIKA SIKU HIZI WAKIWASHWA OMAN WAKIUMWA NA UPELE OMAN WAKISIKIA KIU OMAN HAWATOKI SISI TUMO TU MUARABU WEEE JEMSHI WEEE MAJUHA WAKUBWA.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
IMG-20141019-WA0004

No comments:

Post a Comment