Huu ni wakati mgumu sana kwa Wazanzibar kutokana msiba mkubwa ambao utachukua karne kusahaulika katika Visiwa vyetu vya Unguja na Pemba. Sote Wazanzibar ni waumini wa dini ya kiislam ambayo kiitikadi tunaamini kwamba, tukipatwa na msiba miongoni mwetu kubwa kwetu ni kushukuru kwa mola na kusema INNALLILLAH WAINA ILLAH RAJIUN.
Sisi kama Waislam hatuna budi kushikamana na kamba ya m/mungu licha ya kwamba ni vigumu lakini hatuna budi kufanya subira kwani wenzetu wameshafika mbele ya haki,lililo bakia ni kuwaombea maghufra kwa M/Mungu ili awasamehe madhambi yao- amin.
Hata hivyo nimejawa na hasira pamoja na huzuni nyingi pale ninapoona baadhi ya Viongozi wa juu wakijaribu kuficha ukweli wa tokeo lilivyo huku wakitafuta njia ya kujificha na kuwaelemezea mzigo watu wengine ambao hawahusiki. Ni jambo la aibu na fedheha kubwa kuona kwamba Waziri kama Aboud anashindwa hata kumjua mmiliki wa meli hiyo, hivi sisi kama Raia tuwaelewe vipi viongozi wa aina hii ?HUYU NDIYE WAKWANZA KUJIUZULU LAZIMA AJIUZULU MAANA HATA MILIKI WA MELI HAMJUWI.
Mimi binafsi kama Raia mwema nahisi hakuna sababu ya kufanya uchunguzi kwani ukweli ni kwamba boti ambayo imepinduka haina uwezo wa kuchukua abiria na wala sio boti ya ya abiria ni ya kubeba maguniya ya michele,unga gano,sukari n.k leo mumewajaza abiria kwa makusudi na sasa mumeshatuuwa.hivi sasa watu dinuniani kote watu wanastaajabu, huku Serikali ikificha ukweli wa mambo ulivyo.Uwezekano mkubwa meli hiyo ni kwamba inamilikiwa na mtoto wa kiongozi au Waziri fulani, hao Wahindi wamepewa tu kama kufichwa sisi wanyonge, haiwezekani Waziri ashindwe kujua mmiliki wa meli hiyo, ni vichekesho vitupu.
Kama kuna watu wa kushtakiwa basi wawe ni viongozi wote wa juu kwani hili wamelisababisha wao hakuna haja ya kuwakamata madagaa mukawaadhibu wakati manyangumi na mapapa ndio wahusika. Na wale Viongozi wanaofikiria kwamba tukio hili watalizima kwa fedha kwa Wafiwa, ni kwamba wamechelewa hatuwezi kuuza utu wetu kwa fedha zenu, ndugu na jamaaa zetu mumeshawaua hizo fedha tumieni wenyewe. Kama kweli mwatupenda basi mungetununulia meli tokea hapo awali sio leo hii, watu wetu hata miili yao imeshindwa kupatikana.
Waliokufa ni wanyonge wa Mungu ndio maana no body care,haswa nyinyi viongozi serekalini ndio musio jali kabisa watu munatujali wakati wa KURA TU ILI MUKAE MADARAKANI MUSIO KUWA NA HAYA WALA FADHILI NYINYI SIO VIONGOZI NI MAJINI NA MAZWIMWI WAKUBWA itakuwaje boti ambayo imekuwa design kwa kuchukua mizigo, ipakiwe Binaadam zaidi ya ELFU MOJA ? Hivi viongozi wetu hawakuliona hili tokea awali ? Halafu unaona watu wanajitia huzuni, huzuni gani wakati waliokufa ni wanyonge musiowajali ? Hivi ni nchi gani isiokuwa na sheria ya kudhibiti vyombo vake vya baharini ?
Inakuwaje chombo kizame tokea saa saba usiku mpaka ifike saa moja asubuhi Serikali haina hata boti iliofika pale, zaid ya ngarawa za wavuvi,hii ni aibu na fedheha kwa Serikali. Jee wako wapi KMKM walevi wakubwa wa gongo,ambapo kwa uono wangu hizi ndio kazi zao sio kujifanya wakereketwa wakati wa uchaguzi kuwadhibu raia tu, haya yanatia uchungu sana waungwana na dungu zetu mulio dani ya nchi na nje ya nchi pia.Hivi tatizo la usafiri kati ya Unguja na Pemba limekuja kibati mbaya tuseme kama viongozi wetu hawalijui hili...? Kila mwaka tunafanya sherehe za Mapinduzi ya kipumbavu na yasiyokuwa na maana manake walio uliwa mapinduzi ni dungu zetu lakini sisi tunasherekeya tunaharimu mamilioni ya pesa, hivi hizi pesa zinapatikana vipi hata Serikali ishindwe na fedha ya kununulia meli moja ya uhakika..?
Hii ni kuonesha dhahiri kwamba viongozi wetu hawana imani na wananchi wanawaongoza ila wao umuhimu unakuja wakati wa kura tu.Inatia uchungu kuona Wahusika wanashindwa hata kuizuia meli ambayo hata kipofu anajua kwamba hii haitofika safari yake bila kuzama, matokeo yake inaachiwa kwa sababu ni ya tajiri fulani inauwa abiria wanyonge wasio na hatia. Hivi tutajifunza lini, kila siku ajali kama hizi imekuwa ni common kutokea Zanzibar huku wahusika hawachukui hatua yeyote ile. Leo hii Waziri anasema waliohusika watachukuliwa hatua, wakati yeye ndie miongoni mwa wahusika, hivi anatuletea dharau...?
Iko wapi coast guard, zipo wapi zile helcopta zilizowafyatulia Wapemba risasi au hazina mafuta leo hii..?, mbona magari ya maji ya muasho munayafuata china kuja kuwaadhibu raia wenu lakini boti ya kuokolea walala hoi hili haliwezekani sio nyinyi SIO VIONGOZI NYINYI NI MAJIBWA PORI NA NGURUWE PORI NYINYI NDIO MAANA MUNGELIKUWA VIONGOZI HAYA YASINGELITOKEYA.pia Kutokana na tokeo hili Serikali haina budi kubeba lawama zote na sivyenginevyo na wala musitulete kasumba hizi na zile kila muhusika anze kujiuzulu moja moja na hatuwa zichukuliwe,hapana budi kuwaomba radhi Wazanzibar kwani kilichofanyika ni kitendo cha maksudi na kila mtu anajua sio bahati mbaya hata siku moja.
No comments:
Post a Comment