Nianze kwa kutoa pole zangu za dhati kwa jirani zetu wa Kenya kufuatia Kichapo kilichowakumba kwa muda wa siku nne huku likiacha yatima, wajane, na wafiwa kadhaa, kutokana na kupotea kwa roho za raia wa Kenya na wakigeni, wengi wao wakiwa hawana hatia.
Kenya kuwa jirani zetu haswaa, impekana nasi kwa kila upande, iko mpakani mwa nchi zote mbili Tanganyika na Zanzibar. Kenya wamepakana na Tanganyika kwa upande wa Kaskazini mwa nchi ya Tanganyika (Namanga), na wamepakana na nchi ya Zanziabar kwa upande wa kisiwa cha Pemba (Msuka). Pamoja na ujirani wetu mwema, wakenya ni ndugu zetu, ukirudia historia utang’unduwa kwamba, Mombasa ilikuwa sehemu ya dola ya nchi ya Zanzibar kabla ya kugawanywa na kupelekwa Kenya (mainland). Mbali ya hilo, udugu wa Kenya na Zanzibar au na Tanganyika ni zaidi ya udugu wa kihistoria. Wakenya na Wazanzibar/ na Watanganyika, wanaowana, kuuziana, na kusaidiana wakati wa majanga mbali mbali. Itakumbukwa Wazanzibar mwaka 1964 katika mapinduzi ya kupinduliwa nchi ya Zanzibar na kuingia utawala wa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA Wazanzibari wengi walikimbilia Mombasa na hata hivi karibuni tu siku za uchanguzi kwa mara nyengine tana Wazanzibari wenye asili ya kisiwa cha Pemba walipewa hifadhi ya ukimbizi na ndugu zao wakenya (Shimoni-Mombasa) wakati yalipotokea machafuko na mauwaji kule Pemba, January,2001. Hivyo basi tunakila sababu yakuguswa na msiba huu uliolitokea majirani zetu wa nchi ya Kenya (Westgate), msiba wao ni msiba wetu….!
Nimeisikiliza hotuba ya Rais wa Kenya aloitoa siku ya nne baada ya wanamgambo wa Al-shabab kuvamia Westgate,kuuwa, kujeruhi na kuleta hofu kwa wakazi wa Kenya. Hotuba ilijaa maneno ya faraja, pongezi, ujasiri, kujiamini na ushujaa. Pamoja na ukweli kwamba yeye kama Rais (kiongozi wa nchi) hatakiwi kukiri kushindwa au kugofywa….bado haiondoi ulazima wakukubali kukosea au hata kushindwa kama ni hivyo. Usipokubali kuona ulipokosea au kushindwa kamwe huwezi kurekebisha makosa!!! Unahitaji uone aliposhindwa ndipo Utaweze kuipanga serkali yako kisera na kiulinzi ili kuzuia mauwaji ya watu wa sio na hatia kutokea tena katika ardhi yako msimo wa kiswahili asiyekubali kushindwa sio mshindani.
Kenyatta amehutubia taifa, akielezea kwamba Kenya imeshinda, na imewatia aibu Al-Shabab. Hii ni lugha ya kisiasa, kwangu haina nafasi unapohusisha maisha ya watu wasio na hatia na mali zao. Unasema umeshinda, umeshinda nini wakati kutokana na mfumo wako m’baya wa kisera umesababisha Al-Shabab wawafanye raia wako wasio na hatia na wasiohusika na chochote wala kunufaika na lolote katika sera hiyo wawe waathirika wa Al-Shabab na kuwafanya kuliwa kama kachiri rai wako na Al-Shabab Umeshinda nini, wakati udhaifu wa vyombo vyako vya ulinzi na usalama vimeshindwa kuzuia Al-Shabab hawa kuingia na kufanya uhalifu ndani ya ardhi ya nchi yako..?? Umeshinda nini, wakati serkali yako ilisimama kwa muda wa siku nne mfululizo..?? Umeshinda nini wakati raia wako na wageni wameshindwa kufanya shughuli zao za kujieletea maendeleao kwa muda wa siku nne..?? umeshinda nini wakati rai wako na rai wa kigeni wameuliwa kama kuku..?? Ushindi uko wapi wakati Al- Shabab wamepelekea kuuvuruga uchumi wa Kenya kwa muda wa siku nne tu..?? Ushindi upi wakati tayari Wakenya wenye asili ya somalia wanaishi kwa hofu ya kulipiziwa kisasi, ushindi upo wapi wakati Westgate sio ile tena ya awali, imebaki gofu….sioni ushindi hapo, labda kujifariji tu..!!! Wakenya na wapenda amani duniani hatujashinda..!!
Ni kweli Al-Shabab hawapo tena Westgate, na sasa Westagate ipo chini ya vikosi vya ulinzi vya Kenya, lakini kila mtu anajuwa kwamba halikuwa lengo la Al-Shabab kuhamia Westgate au kuivamia Kenya na kufanya ndio makazi yao..!! Wala haikuwa lengo lao kutoka wakiwa hai, ndo maana kupitia msemaji wao (Abuu Omar), waliweka wazi kwamba hawatafanya makubaliano (negotiation) juu ya mateka, kama wangetaka watoke salama na roho zao, wangewacha njia hii ya makubaliano wazi..!!
Nikikumbuka hesabati nilizojifunza shule ya msingi japo kuwa nilikuwa sio mkali sana katika hisabati (hesabu za milinganyo) nilijiuliza swali hili ; Ikiwa Al-Shabab 10 walovamia Westgate imewachukuwa Jeshi la Kenya na polisi wa Kenya na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama (plus wataalamu kutoka USA/Israel ) siku 4 kupambana nao, jee ingekuwa Al-Shabab 100 ingewachukuwa siku ngapi...??? musitufanye kuchaka wakati sio mahali pa kucheka.
Kwa kutumia kanuni rahisi ya mlinganyo (tulikuwa tunaita kwa kimombo “cross multiplication”), utaona Kenya ingesimama kwa zaidi ya mwezi mmoja (siku 40!) Na ingepoteza watu wasio na hatia wasiopunguwa 700, majeruhi 1700 kama Kenya kungekuwa na ”Shopping malls” mfano wa Westgate 10….kwa wapenda amani ya kweli hakuna tulichoshinda..!!!
Viongozi wa nchi zetu lazima mujuwe kwamba hotuba zenu nzuri, zilizojaa majigambo na ujasiri hazitusaidii sisi raia wakawaida wakati usalama wetu upo mashakani. Hazina maana yoyote kwetu wakati tunaendelea kupoteza maisha, na kuishi kwa hofu ndani ya nchi zetu. Sisi raia tunahitaji suluhisho la kudumu, tunahitaji usalama wetu uwe wa asili sio wakuwekwa na kulindwa na mitutu ya bunduki, maana mwenye bunduki hiyo akisinzia usalama wetu haupo tena…
Al-Shabab ni viumbe kama sisi, ni watu wenye kutumia akili, kupanga,wananda,kukusoma wapi wewe ni mwepesi wa kukuvamia,vipi wakuvamiye.sio kama ni watu wapumbvu kama wengi wa watu wanavyo fikiri.hatufurahi wanacho kifanya hata siku moja sio sawa kabisa lakini Pamoja na ubaya wao huo Al-Shabab ni sawa na kirusi cha maradhi hatari kilichotengenezwa maabara (lethal genetically engineered virus).Al-Shabab,boko haramu na wengineyo tunawatengeneza wenyewe kutokana na sera zetu mbaya na mbovu...!!! Nchi za afrika zimeingia katika mkumbo wakuiga nakumbuka siku za nyuma au miaka ya nyuma watu walivyo anza kurap nchini Tanganyika na nchini Zanzibar moja wa warap alikuja na rap yake akisema musii igee ovyo musii igee ovyo ndio nyinyi viongozi wa afrika na kuja na sera na kuiga ovyo sera za mataifa ya Magharibi (USA na UK). Tumeanza kucheza ngoma za mabwana wakubwa hao, wakati ngoma za asili yetu na midundo na aina ya uchezaji hatujui...!!!!!!!
Binafsi, kama muumini wa amani na utulivu, naamini kwamba hakuna vita yoyote (hasa inayohusisha ndugu) ambayo inamalizwa kwa vita..!!! Hakuna m’badala wa mazungumzo katika kutafuta suluhu. Itakuwa kitendo cha ajabu, jirani yako watoto wake wanagombana na wewe unampeleka mwanao mkubwa akamsaidie jirani yako huyo kumpiga mwanawe moja wapo, kwa jina atiii la kuleta amani..!!! Kama ambayo hakuna sababu yoyote itakayo halalisha Al-Shabab kuuwa raia wasio na hatia, vile vile hakuna sababu yoyote itakayo halalisha Jeshi la nchi moja kuingia nchi nyengine kusaidia upande mmoja unaovutana na mwengine. Usinambie eti unasiaidia serekali halali hakuna serekali halali…my foot! Afrika na serekali halali wapi na wapi....? wacheni kujidanganya nafsi zenu Njia wanazotumia serekali zetu nyingi za Afrika kuingia madarakani tunazijuwa, chaguzi zetu ziitwazo ”free and fair” tunazijuwa, kwa hiyo ikitokea kuna kundi linalalamika au kukataa uongozi uliopo madarakani, huo ni sawa na ugomvi wa ndugu wanaogombania mirathi…si juu yako kupeleka jeshi kupigana dhidi ya kundi moja kwanza nchi yako yenyewe ina walala hoi wangapi..? omba omba wangapi...? watu wasio na kazi wangapi..? watu wasio jeweza wangapi….? leo wewe ndio wakwenda kusaidia nchi nyengine wakati nyumba yako mwenyewe imeja nyufa unamzuga nani...???
Serekali za Afrika badala ya kupeleka majeshi kuendelea kuuwa na kuharibu hicho kidogo kilichobakia nchini somalia, ingekuwa jambo la maana sana kama wangekuwa wanapeleka wana ”diplomasia” na wataalam wa kutatua migogoro, ili kuwaleta wanaogombana kwenye meza ya mazungumzo. Naamini kwenye mazungumzo na utayari wa msuluhishaji kutoegemea upande wowote, lazima kutapatikana suluhisho la kudumu. Nasisitiza, lazima anaesuluhisha awe tayari kuyasikia na kuyakubali mapungufu ya kila upande, lakini pia awe tayari kuyasikia na kuyakubali yenye mantiki kutoka kila upande. Haiwezekani kikundi cha watu katika jamii kipaze sauti zao kulalamika halafu iwe hakuna lamaana wanalodai...!!!! Lazima wasikilizwe na wazingatiwe. Sikubaliani na falsafa ya ”wacha walo wachache wasikike na walo wengi waamuwe” Mimi nasema wacha wote (minority and majority) wasikike na wote wazingatiwe katika maamuzi.
Kupeleka jeshi kwenye nchi ya jirani kwa minajili ya kuisadia serekali au kikundi kinachopigana na serekali ni kujijengea maadui katika nchi yako hivi kweli ingelikuwa Kenya ndio somalia iko katika hali mbaya sana ya kivita yenyewe kwa wenyewe Mkikuyu na Mjaluwo wanapigania kuongoza Kenya kisha somalia wakaleta majeshi wawasaidiye Wajaluwo je nyinyi Wakikuyu,Wakamba n.k. mungelionaje...???,hii ni kuwatengenezea mazingira hatarishi raia wako wasiofaidika kwa lolote na sera hiyo ya kibabe, sera ambayo hata muanzilishi mwenyewe (USA) AMECHEMSHA, ameshaanza kujifunza kwamba haina faida zaidi ya hasara na kuongeza maadui. Upinzani anaoupata rais Obama kutoka kwa raia wake na Maseneta wake dhidi ya nia yake ya kutaka kuivamia nchi ya Syria kijeshi ni ushahidi tosha juu ya kuanza kung’amua ubaya wa sera hii. Lazima tujifunze kwamba mauwaji ya aina yoyote huzaa visasi. Mtu anaeshuhudia mzazi wake au jamaa, iwe mama, baba, dada au mtoto wake au hata rafiki anauliwa kwa bomu, risasi au rocket na majeshi wa nchi ya kigeni, anaharibiwa mfumo wake mzima wa maisha, iwe kwa nia njema au mbaya iliyofanywa na majeshi hao, ni rahisi sana kwa mtu huyo kujenga kisasi dhidi ya jeshi au hata raia wa nchi hiyo. Ni rahisi kushawishika kuungana na vikundi vyenye nia ya kulipiza kisasi ( Al-Shabab)! Lakini lazima pia tukubali kwamba, hakuna amani iletwayo kwa vita....!!! Ashindae kwenye vita hupata utulivu wa muda tu, alieshindwa kwenye vita, akijijenga na kupata nguvu atarudi tena na tena na tena kupambana, maana visasi hurithishwa kizazi mpaka kizazi….!!! Tutatue migogoro yetu kwa mazungumzo yenye nia ya kweli ya kuleta suluhisho au tuwachiye wenyewe wana ndugu msimo wa kiswahili wanadungu wakigombana chukuwa jembe ukalime. Viongozi wetu ubabe wenu unaoishia kwenye majukwaa kwa hotuba za kuandikiwa hautusaidii kitu, mwisho wa siku tunaokufa na kuumia ni sisi raia wakawaida au wachini sio nyinyi muliojificha katika IKULU na MAJUMBA YA KIFAHARI NA ULIZI MKALI..!!!!
Mwisho narudia tena kusema sikufurahishwa na hatua ya kundi Al-Shabab hao kuuwa, kujeruhi na kugofya raia wasio na hatia. Kwa kitendo chao hicho hawastahili kuheshimika hata ikiwa wao ndio wanajita wakombozi wa nchi ya somalia pia sifurahishwi na nchi za Burundi,Uganda,Kenya na wengine kuugana na kuwapiga wasomalia wa upande moja na kusaidia upande mwengine. Naungana na familia zilizopoteza wapendwa wao katika mkasa huu, Allah awajaalie mioyo ya subra, na nawaombea wapowe haraka wale walopata majaraha...!!!!!
Huu ni mtazamo wangu tu….lakini kwa kujihami natembea ”alkali” kujikinga na wanaomwagia wenzao ”asidi” au TINDI KALI hapa nchini Zanzibar natumai nitakuwa sio nazalisha chumvi, na kuepusha masikini za mungu kung’olewa meno bila ganzi nawashauri wajichoma ”lidocaine” kabisaaa!
No comments:
Post a Comment