Bora ni anze kwa kucheka kwanza hahahahahaha mwaka 1964 yalipokuja mapinduzi ya Zanzibar hapa nchini zanzibar sisi watu wausi tulitiwa sumu kweli kweli ya kuwachukia dungu zetu na kufurahia kila walilo fanyiwa na Serekali ya Mapinduzi kama kutolewa ndani ya nyumba zao na kupewa sisi au kunyanganywa mashamba yao na kukatwa heki na kupewa sisi kuvunjiwa nyumba zao na hata kunajisiwa wake zao na watoto wao wakike sisi tukawa tunafurahi sana sana na kuimba mapinduzi daima kumbe tulikuwa ni wajinga wa kufikiri maana sasa wao hawapo tena wamefukuzwa tumebaki sisi kwa sisi mambo hayajatengenea toka nchi hii ilipo pinduliwa na majahili Wakizanzibari wakathani wataka madarakani daima mpaka leo nchi hii inakwenda vile vile kithulma tu basi kisha tunalalamika tusilala mike bali tufurahi tena sana na kuimba pia tuendelea kuimba mapinduzi daima mapinduzi daima kwa nini tulalamike..? au kwa nini leo nyumba zetu zikivunjwa tunalia wakati 1964 Wazanzibari wenzetu walipovunjiwa nyumba zao na kutolewa ndani ya majumba yao sisi tulikuwa tukifurahiya.
MAMLAKA ya Maji Zanzibar imevunja nyumba nyengine 39 za makazi katika maeneo ya Mwanyanya wilaya ya Magharibi Unguja na kufanya idadi ya nyumba zilizovunjwa kufikia 55, baada ya kujengwa katika vianzio vya maji.
Kwa mara nyengine buldoza lilishuhudiwa likivunja nyumba hizo huku baadhi ya wamiliki wake wakiangua vilio.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Zahor Suleiman Khatib, alisema nyumba 100 zitavunjwa katika opresheni hiyo.
Alisema Mamlaka imechukua hatua hiyo baada ya wamiliki kujenga kwenye vianzio vya maji na kukaidi amri ya serikali.
Alisema nyumba zilizovunjwa ni zile ambazo wamiliki wake wamevamia na kwamba hakuna mtu atakaelipwa fidia.
Alisema nyumba hizo zimejengwa ndani ya mipaka iliyowekwa na Mamlaka hiyo, ambamo zimo chemchem za maji zinazosambaza huduma katika mji wa Zanzibar na vitongoji vyake.
Aidha alisema, mbali ya kujenga wananchi hao wamekata miti na kusababisha jua kukausha chemchem hizo, zilizoanza kupata athari kubwa ikiwemo kupunguza uzalishaji wa maji.
Alisema pamoja na juhudi zinazochukuliwa kupitia vyombo vya habari kuihamasiaha jamii kuacha kujenga katika vianzio vya maji, bado jamii inaendelea kushindana na serikali kwa kujenga ndani ya vianzio na kuharibu miundombinu ya maji.
“Tunachukua juhudi kubwa kuwafahamisha wanachi kupitia vyombo vya habari kutojenga katika vianzio vya maji pia kwa kuthibitisha hilo tulijenga nguzo zetu 100 kuwaonesha mipaka lakini baada ya wiki tatu nguzo hizo walizibomoa na kushindana,” alisema.
Nae Mwanasheria wa Mamlaka hiyo Khadija Makame, alisema hakuna fidia itakayolipwa kwa waliobomolewa.
Alisema maeneo hayo yalipigwa marufuku zamani kufanywa shughuli zozote ikiwemo kuchibwa mchanga, kutupa taka na kujenga nyumba za maakazi lakini cha kushangaza wananchi hao walikaidi amri hiyo.
Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Mwanyanya, Pembe Khamis Pembe, alisema alikuwa akichukua juhudi za mara kwa mara kuwaelimisha wananchi wake kuwa sehemu hiyo haitakiwi kujengwa lakini wamekuwa wakiendela kujenga na kumuona hana maana.
Hata hivyo, alikanusha kwamba baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo aliwauzia viwanja akishirikiana na Diwani.
Chemchem ya maji Mwanyanya ni ya muda mrefu ambayo ipo tangu mwaka 1923.
Chemchem ya maji Mwanyanya ni ya muda mrefu ambayo ipo tangu mwaka 1923.
No comments:
Post a Comment