Friday, August 21, 2015

MGOMBEA WA CUF ASEMA ATEKWA NA KUPORWA FOMU ZAKE NCHINI ZANZIBAR


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Mkadam Khamis Mkadam. ((usipate tabu...namba RB/6085/2015 aliyo pewa na polisi hiyo nishakuwekea kama mfuatiliaje kweli fuatili tuone laa kama ni wenzi ndio maana wameficha nyuso zao basi utaufya kimya na sisi tutakuwa tushajuwa kuwa ni wenzio ndio maana umeufyata.
Mgombea ubunge wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema kuwa watu wamejaribu kumteka, kutishwa na kuporwa fomu za kugombea katika jimbo la Shaurimoyo, Unguja nchini Zanzibar. Mgombea huyo, Abdi Seif Hamad alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 17, mwaka huu majira ya asubuhi katika maeneo ya jimbo hilo. Alisema akiwa maeneo hayo wakati akitafuta wadhamini, ghafla kikatokea kikundi cha watu wapatao wanane wakiwa wamejifunika nyuso na kumteka, kumtisha kisha kumnyang’anya fomu ambazo alikuwa ametoka kuzichukua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). “Namshukuru Mungu hawakunijeruhi wala kunipiga, waliniambia wanachokihitaji ni fomu ambazo nilizokuwa nimebeba mfukoni,” alisema Abdi.
Alisema kuwa baada ya kumnyang’anya fomu hizo walimuachia na kwenda kuripoti kituo cha polisi cha Ng’ambu na kupewa namba RB/6085/2015 kisha kuripoti NEC na jana alipewa fomu nyingine. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja nchini Zanzibar, Mkadam Khamis Mkadam alisema hajapata taarifa za kuripotiwa kwa tukio hilo((utalipata vipi na wewe ni mkereketwa wa ccm)). “Watu wangu waliopo katika doria siku ya mkutano wa CHADEMA uliongozwa na mgombea wa urais kupitia chama hicho, Edward Lowassa, ndio walipata taarifa hiyo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alitoa taarifa ya tukio hilo akiwa juu ya jukwaa akiwahutubia wananchi,” alisema Mkadam.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment