Saturday, January 5, 2013

UAMSHO WATIWA JELA HUKU TANGANYIKA IKITULETEA NABII MWANAMKE(MAMA KAHABA LAJA ZENJI NAKUUJITA NABII) ASTAGHAFIRU ALLAH


Kwanza nianze kwa kusema ‘astaghafiru lllah astaghafiru llaah.
Pili niseme kuwa, as I said it again and again, kuwa kila mwenye upuuzi wake anakuja kuufanya hapa Nchini kwetu Zanzibar.
Kuna mama mmoja amejitokeza na kujitangaza au kusema kuwa yeye ni ‘Nabii” llah astaghafiru allah na ameshawahi kufika uwingu wa saba…..na kuona….(almuradi kufru siwezi kusema).
Uzuri wa suala lenyewe limefika ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na baadhi ya ulamaa wamekutana naye mama huyu (Nabii). Ubaya wa suala lenyewe, hawa wooote pamoja na elimu zao, wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya kufru hii. Wamekubali kusalim amri, uislamu wao, imani yao, na kuacha kumuogopa Allah ili wairidhie serikali, na CCM na serikali ya Mkoloni wetu Tanganyika.
Hata hivyo, ofisi ya Mufti imetoa kauli kuwa mama huyu aache kwenda misikitini na kuhubiri kweli hii inatosha kusema kuwa asihubiri misikitini tu...? ikiwa tayari mushajuwa kuwa anakufuru.
Pili wametoa fatwa kuwa ahamishwe na kurejeshwa kwao Nchini Tanganyika. Suala hilo limepingwa na Immigration na wamedai kuwa yeye ni Mtanzania hawezi kuondoshwa kutoka Zanzibar to Tanganyika. Suali linakuja, mbona sheikh Kurwa amehamishwa kutoka Zanzibar na kupelekwa Tabora...?
Sheikh Kurwa ana pacha mwenzake anaitwa Dotto,yupo mpaka leo Chake Chake, zamani akifanya ATC — shirika la Ndege,kisha alikuwa anauza duka la michezo. Ahh…hahaha nicheke kwanza  hawa ni pacha baba mmoja/mama mmoja: chajabu ni mmoja ni Raia na mmoja si Raia na kafukuzwa z,bar na kurudishwa Tabora.
OK, huyu mama anayesema kuwa ni Nabii pia Immigration wanasema hawezi kuhamishwa kutoka sehemu moja ya TZ hadi nyengine. Mapalala aliwahi kufanyiwa deportation hiyo. Abdullah Rashid alipokuwa RC Kaskazini Unguja, alizuia watu wa upande mmoja wa kisiwa cha Unguja kwenda kwengine. Deportation act ya ndani ipo, na ndio moja ya sheria mbaya za serekali hii ya SMZ (draconian law, na hata report ya Nyalali ilipendekeza ifutwe).
Turudi kwa MAMA anae jitaa ‘Nabii”. Huyu Immingration wanasema hawezi kuwa deportated just kwa sababu amekuja kuwadhalilisha na kuwatusi wazanzibari na uislamu na serikali inamtetea kwa hali zote. Hii ndio hali inayotukabil jamani, na kama hatutaki kuamka basi hatuamki tena. Huyu mama ni murtad – lakini kaimu katibu wa Mufti anaitwa Jongo anamtetea just kwa sababu ni mtu wa kwao KIMBIJI (mndengereko mwenzake); ahhhh…. ametoka Soraga amekuja Jongo — hao kwa hao.
Huyu mama amekuja (kahaba mmoja tu) amekuja na kujitagazia kuwa yeye ni “nabii’. na sisi Tumekubali. Tumeambiwa katika quran tukufu kuwa Mtume Muhammad SAW ndiye wa mwisho, tunahoji nini au tunataka nini zaidi ya hilo...? leo aje janajike pumbavu kama hili kahaba la kupepea asema yeye ni ‘nabii’ na sisi tumekaa tunakodoa macho tu.je imani zetu ziko wapi..?au sisi ni waislamu wa  aina gani..?
Jana nimezungumza na sheikh mmoja — yeye anasema ‘aah kijana usiwe na wasi wasi huyu anatafuta mume tu’ daaah nilipingwa na butwaa mimi nazungumza mambo ya mshenzi huyu mama kuithalilisha dini sheikh anakejeli. Huyu ni sheikh kweli au ndio hao masheikh ubwaabwaa mjinga hayuko serious kabisa, yeye analetea mambo ya kipumbavu ooh huyo mama anataka mume mwanamke anaifedhehi dini na kujita mtume wewe unasema anataka mume haya muowe basi wewe...?
Angalia: mama huyu aliwahi kuzungumza na rafiki yangu mmoja,miaka miwili iliyopita;rafiki yangu akamuliza una miaka mingapi..? jibu alisema ana miaka 40; kuna msikiti ameingia jana pia amesema kuwa ana miaka 40. Ina maana ‘nabii’ huyu hakui miaka yake...?
Tuendelee kuwakamata UAMSHO, na tuwaenzi ‘manabii’ kutoka Mkuranga na Kimbiji kwa mkoloni mweusi.

UWANJA WA NDEGE MPYA WA ZANZIBAR WADORORA SMZ KULETA MAENDELEO Z,BAR NAKAMA KUMUAMBIA MZUNGU APANDE MNAZI ANGUSHE NAZI AU APANDE MKARAFU


Ndio tumeuanza mwaka mpya. Kuna mengi tuliyoahidi mwaka uliopita kuwa yatakamilika mwaka huu. Mutakumbuka miongoni mwaa hayo ni pamoja na:
* uwekaji wa waya mpya za umeme kutoka nchi ya Tanganyika hadi Zanzibar hata sijuwi kwa nini na tumezungukwa na bahari na juwa lamungu bure sijuwi kwanini bado tunawatengemeya wakoloni weusi kwa umeme.
* Kukamilika kwa mradi mkubwa wa e-government nao ni BUTU.
* Kukamilika kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa, nk
Leo naomba nigusie hili la ujenzi wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa.
Kama tunavyofahamu ujenzi wa uwanja huu umekuwa kwenye mashaka makubwa tokea kuanzishwa kwake ambapo 70 billion USD zimetumika katika ujenzi wake. Halkadhalika kuna maongezeko mengine ambayo mwanzo hayakuwemo kwenye mkataba wa awali.
Vilevile, kama tunavyoshuhudia kusimama na kuendelea polepole kwa ujenzi wenye fungu kubwa la fedha za walipa kodi ambao ni mkopo nafuu kutoka serikali ya Watu wa China. Hii ni sawa na kusema kila Mzanzibar atakuwa anadaiwa fedha zilizotumika kwenye mradi huu.
Kuna jengine jipya limejitokeza. Nalo ni jengo la abiria wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa limejengwa sehemu siyo HAHAHAHA INABIDI NICHEKE KWANZA. Sehemu liliopo jengo hili kwa mujibu wa ramani na vipimo ni sehemu ya kupaki ndege. Jengo lilitakiwa lirudi nyuma zaidi kwenye eneo la nyumba za raia upande wa magharibi ili kupisha nafasi ujenzi wa park za ndege.
Hili ni pigo kubwa kwa mradi huu uliogharimu zaidi ya 70 milioni USD, huku ukichelewa kukamilika kwa wakati wake. Swali zito ni vipi mafundi wa ujenzi huu wataweza kufanya masahihisho ambapo foundation yake ilikuwa kina kikubwa, structure imefungwa na bolts and nuts, huku baadhi ya vipande vyengine kuunganishwa kwa welding.
Ingawa kutakuwa na maswali mengi kuliko majibu, msomaji na wewe unaweza kujiuliza maswali zaidi ya haya nitakayojiuliza:
i) Mjenzi wa uwanja pamoja na uzowefu wake hivi hakutanabahi kwamba anatumia vipo sivyo?
ii) Consultant wa ujenzi huu muda wote huo alikuwa haoni au kujuwa vipimo vilivyotumika sivyo?
iii) Wataalam wa serikali yetu jee pia hawakutanabah kwamba hili jengo liko nje ya eneo la makubaliano?
iv) nani atalipa gharama za fidia kwa hasara zote zitakazotokea, au kama kawaida yake SMZ itaanza kuwandanganya wananchi kunde mbaazi njugu mawee na kathalika..?
v) Jee Serikali yetu itaendelea kuwa mahusiano mazuri na China, huku tukiendelea kuchukuwa mikopo ya bei nafuu kwa masharti ya kupangiwa wajenzi (contractors) wa Kichina?
Kuna haja ya Wazanzibar kuzinduka kutokana na usingizi wa “mnono wa alfajiri” kuendelea kwetu tutaikuta nchi siyo yetu tena. Haya yote yasingetokezea laiti tungekuwa makini katika utendaji kazi wetu.

MASHEIKH WENGINE MBARONI (DPP) WA ZANZIBAR YUKO KUWANGAMIZA WAZANZIBARI NA KUIMARISHA MFUMO KIRISTO NCHINI Z,BAR


 
Mhe. Yessaya Kayange
MAJAJI PIA SASA Z,BAR NI MACHOGO KWELI TUTAPONA SISI..?
HAKIMU KAYANGE HILI JINA TU UNAJUWA WAZI YUKO HAPO KUWANGAMIZA WAZANZIBARI
 
MASHEIKH wawili ambao ni viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wameongezwa katika kesi ya kuhatarisha usalama wa nchi na sasa kuwafanya washitakiwa wawe 10 katika kesi hiyo. Walioongezwa jana wakati kesi hiyo ilipotajwa Mahakama ya Mkoa Vuga mjini hapa ni Abdallah Said Ali (48) ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Fikirini Majaliwa Fikirini (48) ambaye ni Mhadhiri wa Jumuiya hiyo.
Walisomewa mashitaka ya kufanya hujuma kwa kutoa maneno ya uchochezi katika mihadhara mbalimbali katika maeneo ya miji ya Unguja kuanzia Mei 26 hadi Oktoba 19 mwaka jana na kuwachochea wananchi kuvunja amani na kuharibu mali zilizogharimu sh. 500 milioni.
Akisikiliza kesi hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Mkoa, Yessaya Kayange alikataa kutoa dhamana kwa washitakiwa kwa vile kuna hati ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) inayozuia kupewa dhamana kwa washitakiwa hao.

Hakimu Kayange kuhusu ombi la washitakiwa la kutaka kesi yao isikilizwe Mahakama Kuu alisema ombi hilo tayari limeshapelekwa na yasubiriwe maamuzi. Wakili wa upande wa utetezi, Abdallah Juma alidai washitakiwa hao hawapaswi kushitakiwa kwa sheria ya Usalama wa Taifa na wakaongezewa mashitaka mengine na kuongeza kuwa washitakiwa wote wanaweza kupewa dhamana.
“Wateja wangu wamefungwa midomo katika mahakama hii. Kila siku wanaletwa hapa na hawatakiwi kusema chochote, kwa hiyo naomba wapelekwe Mahakama Kuu mbele ya Jaji ili waweze kupewe haki ya kusema kwani huenda wenyewe wakakiri wote makosa yao,” alidai Wakili Juma.
Wakili Juma alidai kwa vile Mahakama ya Mkoa haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo basi haina haki pia ya kuwapeleka rumande na kuwataka wateja wake waachiwe na kurudi nyumbani. Upande wa mashitaka ukiongozwa na Rashid Abdallah na Raya Mselem walikataa madai ya wakili wa utetezi wa kesi hiyo kusoma upya kwa vile wameongezwa washitakiwa wawili na kwamba hawana pingamizi na suala la dhamana lakini waendelee kushitakiwa kwa sheria hiyo hiyo ya Usalama wa Taifa.
Kesi hiyo inasikilizwa chini ya ulinzi mkali na polisi wamekuwa wakiwanyanyasa waandishi wa habari kwa kuwazuia na mwandishi mmoja jana alipigwa virungu viwili na askari mmoja. Washitakiwa wa zamani katika kesi hiyo ni Sheikh Farid Hadi Ahmed (41), Msellem Ali Msellem (52), Mussa Juma Issa (37), Azzan Khalid Hamdan (48), Suleiman Juma Suleiman (66), Khamis Ali Suleiman (59), Hassan bakar Suleiman (39) na Gharib Ahmad Omar (39). Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Januari 14 mwaka huu



Friday, January 4, 2013

DR KUMBI SHEIN APANGIWA KUFUNGUA MRADI BUTU NCHINI ZANZIBAR

Apangiwa kufungua mradi “butu”                                      Afanya uteuzi wenye utata wa hali ya juu                                  

Wengi tunafahamu dunia inapopitia huku nchi nyingi tukiziona zikijikita na kujiingiza kwenye hicho kinachoitwa “KITEKNOLOJIA. Inafahamika fika kuwa Teknolojia ni uwanja mpana, hapa tutazungumza teknolojia moja ambayo ni E-GOVERNMENT.

Kama ilivyotangazwa kwenye ratiba ya sherehe za mapinduzi, hiyo kesho kutakuwa na ufunguzi wa mradi wa E-GOVERNMENT hapo kwenye ofisi ya mradi huo. Imesemwa kuwa Dr Kumbi Shein atafanya ufunguzi huo wakati wa jioni.
Dr Kumbi Shein kwenye mradi huu kauziwa “paka kwenye gunia”. Mradi umegharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi. Sijuwi ni kitu gani Dr Kumbi Shein anakwenda kufungua hiyo kesho hapo Mazizini. Hivi Dr Kumbi Shein anajuwa maana ya E-Government..?
Dr Kumbi Shein E-Government ni zaidi na hicho unachokwenda kukishuhudia kesho. Unachotakiwa kukifahamu ni kuwa unapofunga E-Government ni kwamba chochote unachotaka kukijuwa kilichoko Wizara Fedha, technolojia ikuruhusu kufanya hivyo.
Dr Kumbi Shein E-Government sio kuunganishwa na kuzungumza kwa video conference kwa yule aliye Pemba na Unguja. Hivyo ni kuijaribu “Fibre Cable”. Wala hatuwezi kuiita E-Government.
Dr Kumbi Shein hiyo failure ya mwanzo unaianza kwa mwaka huu mpya wa 2013. Unapousiwa ni kupanua masikio na kusikiliza wengine wanasema nini sia kujidai ujuwaji na huna unalolijuwa.
Kosa jengine lililofanyika ni kwa ule uteuzi wa Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Uteuzi huu umeleta utata mkubwa kwani sector hii imeundwa ndani ya wizara tatu tofauti. Ndani ya Wizara ya Elimu, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na sasa iko kwenye Wizara ya Utumishi na Utawala Bora hivyo kulenga mgongano mkubwa kwa wakurugenzi hao watatu.
Hivi karibuni Dr Kumbi Shein alifanya uteuzi wa Bw Shaaban Choum kuwa Mkurugenzi wa ICT ndani ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, hivyo kuleta mparaganyo mkubwa kiasi cha hata wakurugenzi wengine kususia uteuzi huo na kuahidi kutotoa ushirikiano na mkurugenzi huyu.
Taarifa zaidi inasema kuwa hata uwezo wake ni mdogo sana huku akihusishwa na “mascandal” ya ubadhirfu na mamilioni ya fedha.
Ningemshauru Dr Kumbi Shein amkatae paka hadi atoke nje. Asifungue mradi huu hadi ifahamike fika kwamba mradi umekamilika. Ukifuatilia muundo wa serikali yake hauna tofauti na Serikali ya Watanganyika, hivi kwanini Dr Kumbi Shein hakuiga kule Bara kwa wakoloni weusi wanaotutawala na waliomfanya kuwa waziri asiyekuwa na wizara jinsi walivyofanya mradi wao wa E-Government. Wao wameita “Agency” kabisa na hawakutaka kuutia kwapani mradi huu. Faida yake mradi umekamilika na unafanya kazi yake kama ilivyotarajiwa.
Dr Kumbi Shein, umeanza mwaka mpya na kufeli kiana hii. Kumbuka unakaribia nusu ya muhula wa uongozi wako. Ipo haja ya wewe kujiuzulu haswa maana unatupeleka kubaya au pokea ushauri stahiki kwa wataalam wanaofahamu kwa kina juu ya mradi huu. 20milion USD ni fedha nyingi sana, hazilingani na matumizi ya gharama na utekelezaji wa mradi huu.

NCHI YA TANGANYIKA HAIKOPESHEKE TENA KIMATAIFA KWA KUTO LIPA MADENI NA KUZIDI KUIANGAMIZA NCHI YA ZANZIBAR


Waziri wa fedha, Dk.William Mgimwa
Mwakagenda alisema deni la taifa limeongezeka kwa dola 456.1 za Marekani, sawa na asilimia 4.5 kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu 2011 na hatari ya kukua kwa deni ni nchi kutoaminika na hivyo kushindwa kukopesheka kimataifa.
Madhara mengine ambayo asasi hiyo inasema yanayotokana na deni kubwa kwa nchi, ni uwezekano wa wawekezaji kupunguza imani na mazingira ya kiuchumi na hivyo kukataa kuja nchini kuwekeza.
Mwakagenda alitaja madhara mengine yanayoweza kutokana na kukua kwa deni la taifa kuwa ni uwezekano wa kuvuruga uimara wa Shilingi ya TANGANYIKA pamoja na baadhi ya maofisa wa serikali na watendaji kutumia mwanya wa kukopa kufanya ufisadi na kujilimbikizia mali.
Alisema takwimu za Benki Kuu ya Tanganyika (Tanzaia ni Koti tu) (BoT) zinaonyesha kuwa deni la taifa lilipanda kutoka dola bilioni 1.83 za Marekani mwaka 2010 hadi kufikia dola bilioni 2.3 mwaka 2011 na uwiano wa pato la taifa (GDP) ulikuwa asilimia 44.4.
Mkurugenzi huyo aliishauri Tanganyika kujifunza kutoka kwa baadhi ya nchi za Ulaya ambazo alisema madeni yao yamekuwa siyo endelevu.
Aliongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania ilisamehewa madeni yake yote, lakini inashangaza kuona imekopa tena kiasi kikubwa kama hicho, hali ambayo kwa sasa kinatishia kuvuruga uchumi.
“Siyo kila serikali inapokuwa na shida, cha kwanza kufikiria ni kwenda kukopa, lazima ibadilike na kuanza kufikiria namna nyingine ya kupata fedha za kufanyia maendeleo na shughuli zake nyingine,” alisema Mwakagenda.
MAJIBU YA MBENE MPAMBE WA SEREKALI YA TNGANYIKA ALISEMA HAYA.
Wakati asasi hiyo ikitoa kauli za kuikosoa serikali kwa matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi, Naibu wa Fedha, Janet Mbene, jana alijibu hoja hizo akisema kuwa bado Tanganyika inakopesheka na taasisi za kimataifa zikiwamo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).akiendelea kujikosha

Akizungumza na FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI BILA YA KUJUWA ALISEMA,Mbene kuwa Tanganyika ina rasilimali nyingi ambazo inaweza kuzitumia kuweka rehani ili ipate mikopo na haijafikia hatua ya serikali ishindwe kukopesheka na kupinga madai yaliyotolewa na Mwakagenda.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa fedha zote zilizokopwa na serikali zilitumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli, kuwekeza katika sekta za elimu, afya na kukuza uchumi.
Alifafanua kuwa Tanganyika ni miongoni mwa nchi 10 za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa haraka na IMF na WB wametoa ripoti inayosifia juhudi za serikali katika kukuza uchumi wake.
Kuhusu serikali kukopa fedha kutoka katika benki za ndani, Mbene alikiri kuwapo utaratibu huo, lakini alisema suala la kukopa siyo kosa kama mkopaji analipa deni analokopa.

“Ni kweli tunachukua fedha, lakini tunafanya hivyo tukiwa tunaendelea kukusanya mapato yetu na tunapopata tunaenda kulipa deni na serikali haiwezi kuwa na fedha muda wote,” alisema Mbene.
Hata hivyo, Mbene alisema serikali ina akiba ya fedha zinazofikia Shilingi trilioni nne na kwamba kiasi hicho kinatosha kuendesha nchi na kutekeleza shughuli mbalimbali.

Wednesday, January 2, 2013

MUUNGANO NI TANGANYIKA NA Z,BAR AU ZANZIBAR NA KANISA...?


Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam,Nchini Tanganyika Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo 
PENGO AENDELEZA UPANDIKIZAJI WA CHUKI  KATI YA DINI NA DINI SOMA UELIMIKE NA KUMJUWA PENGO            
Kwa ufupi,

“Hata hao wanaofikiri kuwa wakibaki pekee yao na dini zao watakuwa salama hawapo sahihi kwani kuna nchi hivi sasa zipo katika vurugu ingawa zina imani moja ya dini,” alisema Pengo.
Alisema, “Angalieni nchi kama Tunisia, Algeria na nchi nyiingine hazipo salama ingawa zina imani moja ya dini.”

ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amelaani kitendo cha kupigwa risasi kwa Padri wa kanisa hilo, Parokia ya Mpendaye mjini Zanzibar, Ambrose Mkenda na kusema kitendo hicho hakileti matumaini mema kwa amani ya nchi katika siku za usoni.Desemba 24 mwaka 2012, Padri Mkenda alipigwa risasi na watu wasiofahamika nje ya nyumba yake na kufikishwa katika Hospitali ya Muhimbili ambako alitolewa risasi mbili.

Jana, Pengo akizungumza katika ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es Salaam, alisema tukio hilo na vurugu za kuchomwa makanisa ni ushahidi wa wazi kuwa watu hawaitaka amani nchini.

“Padri wetu Zanzibar wakati anapigwa risasi hakuwa anatoka kwenye vilabu vya pombe wala hakuwa katika majumba ya watu, alikuwa anatoka kutimiza majukumu yake ya kiuchungaji lakini akapigwa risasi nje ya nyumba yake, tunakwenda wapi?” alihoji Pengo.
Kadinali Pengo alisema vurugu za kidini zinazoendelea kujitokeza nchini hivi sasa hazileti dalili njema kwa amani ya nchi.

“Hata hao wanaofikiri kuwa wakibaki pekee yao na dini zao watakuwa salama hawapo sahihi kwani kuna nchi hivi sasa zipo katika vurugu ingawa zina imani moja ya dini,” alisema Pengo.
Alisema, “Angalieni nchi kama Tunisia, Algeria na nchi nyiingine hazipo salama ingawa zina imani moja ya dini.”

Alisema wanaochochea vurugu za kidini watambue kuwa hata kama dini nyingine itaondoka na wao kubaki pekee yao hawatabaki salama.

Kadinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa macho na tofauti ambazo zinaweza kuleta vifo katika jamii kwani tofauti za kidini zisiwe sababu ya kutukanana, kukashifiana kwani dini zote zinatoka kwa baba mmoja hivyo haoni sababu za kujengeana chuki.

Pengo alisema mamlaka ya Serikali siyo kusimamia msingi wa dini yoyote na inachaguliwa na watu wote hivyo kazi yake ni kuwahakikishia watu wa dini zote usalama wao na mali zao na iwapo itashindwa na kuwabagua watu kulingana na imani zao ni wazi kuwa itakuwa imepoteza mwelekeo.

“Watu wa imani zote za dini wanapaswa kulindwa na Watanzania wametakiwa kuliombea Taifa lao ili liweze kudumu katika imani na mataifa mengine yaweze kuiga kutoka kwetu,” alisema Pengo na kuongeza kuwa Taifa linahitaji maombi zaidi kipindi hiki kuliko wakati mwingine.

Padri huyo alitolewa risasi mbili kinywani na hali yake inaendelea vizuri na hadi juzi kulingana na taarifa za Jeshi la Polisi Zanzibar, watu wawili walikuwa wakishikiliwa na jeshi hilo kuhusiana na shambulizi hilo na katika ghasia zilisababisha kuchomwa kwa makanisa Zanzibar na Dar es Salaam watu kadhaa kesi zao zipo mahakamani
.

Tuesday, January 1, 2013

BALOZI SEIF ALI IDDI AJIUGA NA KANISA


Balozi wa Tanganyika nchini Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Padri Cosmas Shayo wa Kanisa la Roman Katoliki  Nchini Zanzibar wakati alipokwenda kutoa mkono wa pole kwa uongozi kanisa hilo na familia kufuatia tukio la kujeruhiwa na risasi kwa Padiri Ambrose Mkenda.
Ni dhahiri kwamba hali ya amani Nchini Zanzibar ni tete, huku viongozi wakitajwa kuhusisha dini katika harakati za kufikia malengo yanayotajwa kuwa na nia ya ovu.
Viongozi wa dini, wanasiasa na wanazuoni, wanaelezea umuhimu kwa Taifa kudhibiti uhalifu na kuwachukulia hatua kali wahalifu wanaochochea vurugu, ili kulinda na kuendelea amani Nchini  humo.
Nchini Zanzibar inakabiliwa na kukua kwa vurugu, hujuma na njama za kuteketeza mali na maisha ya raia wasiokuwa na hatia, dalili zikionyesha wazi kuwepo ‘mkono wa wanasiasa.’
BALOZI WA NCHI YA TANGANYIKA NCHINI ZANZIBAR ANENA

Balozi  mdogo wa nchi ya Tanganyika aliyekuweko nchini Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema serikali itahakikisha inawasaka na kuwachukulia hatua za kisheria waliompiga risasi Padri Ambrose Mkenda, Desemba 25, mwaka huu.
Balozi Seif alisema kitendo hicho kimetoa sura mbaya kwa Taifa na serikali, hivyo kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani na umoja wa kitaifa.
“Ni jambo baya na la kusikitisha, tena limetoa sura mbaya kwa Taifa. Serikali haitosita kuachukulia hatua dhidi ya watu waliofanya uhalifu huo,”alisema Balozi Iddi na kuwataka wananchi kuheshimu na kulinda misingi ya amani na umoja wa kitaifa Zanzibar.
Balozi Seif alitoa msimamo huo wa serikali alipokwenda kutoa pole kwa uongozi wa kanisa hilo na nyumbani kwa Padri Mkenda mjini hapa jana.
Alisema SMZ imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi katika mazingira ya hofu isiyokuwa ya lazima wakati Tanganyika na Zanzibar ni nchi za amani.
PADRI WA KATOLIKI AWAONYA WANAOWAPOTOSHA WATOTO
Padri Cosmas Shayo wa Kanisa Katoliki, aliiomba serikali kuimarisha ulinzi wa raia wema wa kikiresto wanao tokeya bara nchini Tanganyika wanao ishi hapa Zanzibar ili kupunguza hofu iliyotanda mioyoni mwao, kutokana na matukio ya hujuma yanayojitokeza visiwani humo.
Padri Shayo alitahadharisha kwamba hulka mbaya iliyoanzishwa na baadhi ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima kwa sababu ya utofauti wa kidini, inawajengea msingi wa maisha mabovu watoto hao.
“Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine, tuelewe kwamba Taifa halitakuwa na mwelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye,” alisema.
Padri Shayo alisema serikali inawajibika kufanya uchunguzi wa kina kufuatia kupigwa risasi kwa kiongozi huyo.
Padri Mkenda alipigwa risasi na watu wawili waliokuwa wamepanda pikipiki majira ya saa 1:45 usiku wakati akitoka kumuangalia mgonjwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja akiwa ndani ya gari wakati akisubiri kufunguliwa geti na mlinzi na hakuna kitu kilichoibiwa baada ya kiongozi huyo kupigwa risasi.
Tukio la kupigwa risasi mbili za shingo kiongozi huyo wa kiroho limetanguliwa na mkasa wa kumwagiwa tindikali Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga wakati akifanya mazoezi ya viungo Novemba 6, mwaka huu.
Hata hivyo hakuna watu waliyokamatwa kuhusiana na matukio hayo. Lakini Jeshi la Polisi limeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuwatafuta watu waliyofanya mashambulio hayo tofauti visiwani hapo.pia FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI tumeguduwa kuwa ni uzushi tu maana mara wanasema amepigwa risasa alipokuwa akitoka kanisani kuelekea kwake mara amepigwa risasi nje ya nyumba yake sasa wanasema alipingwa risasi alipokuwa akitokeya kumtizama mgonjwa katika hospitali ya mnazi moja sasa ukweli ni upiiiiiiiii.....?
HAMAD RASHID AINYOOSHEA KIDOLE CUF
Mbunge wa Wawi (CUF) Hamad Rashid Mohammed, alisema Zanzibar itaingia katika machafuko makubwa endapo hakutafanyika jitihada za haraka kukomesha chuki za kidini zinapandikizwa miongoni mwa raia wake.
Alisema hali si shwari visiwani humo, akiifananisha na ‘yai jeteta’ ambalo kupasuka kwake, kunaathiri watu wote.
Hamad alisema kihistoria Zanzibar ni nchi iliyokuwa na watu wenye uvumilivu wa kidini kwa miaka mingi na hakuna aliyetarajia siku moja watu watatengana na kuhujumiana kwa sababu ya tofauti za kiimani.
Alisema matukio ya kumwagiwa tindikali kwa Katibu wa Mufti Fadhili Soraga na tukio la hivi karibuni Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni baadhi ya matokeo ya chuki hizo zilizopandwa na wanasiasa.
“Hali ya Zanzibar inasikitisha sana, matukio yote mawili ya kujeruhiwa viongozi wa kidini ni jambo la kulaaniwa kwa nguvu zote na inathibitisha kuwepo kwa watu wanaochochea hali hiyo kwa manufaa yao,” alisema Hamad.
Alisema kumekuwepo na viongozi wa kisiasa wanashindwa kukemea hadharani jambo hilo kwa sababu wanahusika kuwashawishi na kuwachochea viongozi wa dini kushiriki vurugu hizo.
“Uongozi wa kisiasa umeshindwa kukemea kwa sababu kuna baadhi ya wanasiasa wanahusika, wakati mwingine wanakwenda kwa viongozi wa dini zote kuchochea, lakini ikumbukwe ikitokea vurugu hakuna atakayepona,” alisema.
Mbunge huyo asiyetambuliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) alichokitumia kugombea na kushinda kiti hicho, alisema suluhu ya tatizo hilo ni kuanzishwa mjadala wa kitaifa kujadili kuhusu chanzo halisi na namna ya kufikia suluhu ya kudumu.
Pia Hamad alisema hakuna viongozi wenye maoni na nguvu ya kuzuia jambo hilo, kwa vile viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa wanatofautiana kiitikadi.
Katika suala hilo alionyesha kufadhaishwa na msimamo wa viongozi wa CUF kutokuwa na upande wa kusimamia kuhusu Muungano, moja ya madai yanayotajwa kutumika kama kigezo cha kuchochea vurugu visiwani humo.
“Ndani ya CUF kuna watu wanataka Muungano wa Mkataba na wengine wanataka Muungano wa serikali tatu, tofauti na CCM ambao wana msimamo mmoja wa serikali mbili,” alisema.
“Hili ni jambo baya sana kwa viongozi wa CUF kutokuwa na msimamo wa kimaadili, haiwezekani chama kuwa na makundi mawili yenye tofauti ya msimamo, kutokana na hili huwezi kusimamia serikali hata mara moja,” aliongeza kusema.
Naye Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alielekeza lawama kwa jeshi la polisi na kusema linafanya kazi kisiasa na kushindwa kutekeleza wajibu wake.
Profesa Lipumba alisema kama polisi wangefanya kazi kwa weledi na kuachana na kutumika kisiasa, matukio yanayotokea Zanzibar yasingekuwepo kwa sababu wahusika wote wangekamatwa.
Hata hivyo alipinga hoja ya Hamad kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imeshindwa kutekeleza wajibu wake katika kuidhibiti hali hiyo.
CHUKI ZILIATHIRI UTENDAJI WA TUME YA KATIBA MPYA
Wakati huo huo, imefahamika kuwa kutokana na kuenea kwa chuki za kidini, wajumbe wa Tume ya kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wanafanya katika hali ya tahadhari, baada ya kukabiliana na matukio ya kibaguzi.
Vyanzo vya habari vimeieleza kuwa baadhi ya wajumbe wasiokuwa waumini wa dhehebu moja wanaofanya kazi kwenye tume hiyo visiwani humo, wanachukua tahadhari kubwa huku wakishindwa kwenda kwenye maeneo yanayoonekana kuwa na watu wenye msimamo mkali wa kidini.
“Mimi mwenyewe ni muathirika wa mambo hayo, lakini siwezi kuzungumzia sana jambo hilo, tunachokifanya ni kutokwenda sehemu tunayoona kuna dalili mbaya,” kilieleza chanzo chetu kutoka tume hiyo.