Saturday, January 5, 2013

UWANJA WA NDEGE MPYA WA ZANZIBAR WADORORA SMZ KULETA MAENDELEO Z,BAR NAKAMA KUMUAMBIA MZUNGU APANDE MNAZI ANGUSHE NAZI AU APANDE MKARAFU


Ndio tumeuanza mwaka mpya. Kuna mengi tuliyoahidi mwaka uliopita kuwa yatakamilika mwaka huu. Mutakumbuka miongoni mwaa hayo ni pamoja na:
* uwekaji wa waya mpya za umeme kutoka nchi ya Tanganyika hadi Zanzibar hata sijuwi kwa nini na tumezungukwa na bahari na juwa lamungu bure sijuwi kwanini bado tunawatengemeya wakoloni weusi kwa umeme.
* Kukamilika kwa mradi mkubwa wa e-government nao ni BUTU.
* Kukamilika kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa, nk
Leo naomba nigusie hili la ujenzi wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa.
Kama tunavyofahamu ujenzi wa uwanja huu umekuwa kwenye mashaka makubwa tokea kuanzishwa kwake ambapo 70 billion USD zimetumika katika ujenzi wake. Halkadhalika kuna maongezeko mengine ambayo mwanzo hayakuwemo kwenye mkataba wa awali.
Vilevile, kama tunavyoshuhudia kusimama na kuendelea polepole kwa ujenzi wenye fungu kubwa la fedha za walipa kodi ambao ni mkopo nafuu kutoka serikali ya Watu wa China. Hii ni sawa na kusema kila Mzanzibar atakuwa anadaiwa fedha zilizotumika kwenye mradi huu.
Kuna jengine jipya limejitokeza. Nalo ni jengo la abiria wa uwanja wa ndege mpya na wakisasa limejengwa sehemu siyo HAHAHAHA INABIDI NICHEKE KWANZA. Sehemu liliopo jengo hili kwa mujibu wa ramani na vipimo ni sehemu ya kupaki ndege. Jengo lilitakiwa lirudi nyuma zaidi kwenye eneo la nyumba za raia upande wa magharibi ili kupisha nafasi ujenzi wa park za ndege.
Hili ni pigo kubwa kwa mradi huu uliogharimu zaidi ya 70 milioni USD, huku ukichelewa kukamilika kwa wakati wake. Swali zito ni vipi mafundi wa ujenzi huu wataweza kufanya masahihisho ambapo foundation yake ilikuwa kina kikubwa, structure imefungwa na bolts and nuts, huku baadhi ya vipande vyengine kuunganishwa kwa welding.
Ingawa kutakuwa na maswali mengi kuliko majibu, msomaji na wewe unaweza kujiuliza maswali zaidi ya haya nitakayojiuliza:
i) Mjenzi wa uwanja pamoja na uzowefu wake hivi hakutanabahi kwamba anatumia vipo sivyo?
ii) Consultant wa ujenzi huu muda wote huo alikuwa haoni au kujuwa vipimo vilivyotumika sivyo?
iii) Wataalam wa serikali yetu jee pia hawakutanabah kwamba hili jengo liko nje ya eneo la makubaliano?
iv) nani atalipa gharama za fidia kwa hasara zote zitakazotokea, au kama kawaida yake SMZ itaanza kuwandanganya wananchi kunde mbaazi njugu mawee na kathalika..?
v) Jee Serikali yetu itaendelea kuwa mahusiano mazuri na China, huku tukiendelea kuchukuwa mikopo ya bei nafuu kwa masharti ya kupangiwa wajenzi (contractors) wa Kichina?
Kuna haja ya Wazanzibar kuzinduka kutokana na usingizi wa “mnono wa alfajiri” kuendelea kwetu tutaikuta nchi siyo yetu tena. Haya yote yasingetokezea laiti tungekuwa makini katika utendaji kazi wetu.

No comments:

Post a Comment