Tumesikia maoni ya kutaka kufanya katiba mpya ya Tanganyika. Tumewasikia viongozi wastahiki wa Zanzibar waliotoa maoni yao katika kuifanya hiyo katiba mpya (kama itakua!), tumeona msimamo mzuri wa viongozi wetu: Karume Jr, Maalim Seif, Moyo, Salim Rashid, n.k ni wengi – wote wameitetea haki ya Zanzibar.
Sijui kama wengi mnajua kuwa Tanganyika haikuwa na kiti pale UN, na walipokuwa nacho, kiliwekwa rehani (walafukuzwa na U.N) baada ya Nyerere kuiunga mkono serikali ya Nigeria kuhusu jimbo la Biafra (successionist). Hapa UN iliwapa red card Tanganyika 1967 nakuwatimuwa kabisa na hawajarudishiwa kiti kile mpaka leo nini kilitokea baada ya Tanganyika kufukuzwa katika U.N...?
Walichokifanya Tanganyika wakati ule ni kukikalia kiti cha Zanzibar kilichopo U.N nakuva koti la Utanzania na kukifanya kiti kile kama ndio chao. Yule Rashid Salim Adi, anayeshughulikia sana suala hili analijua vizuri suala hili, na kama anasoma mada naomba pia achangie au asaidie fikra kwa umankini na umahiri zaidi ili umma wa Zanzibar upate kujua zaidi na zaidi. Haya ni mambo yamefichwa sana chini ya carpet. Vijana wengi wa Zanzibar na Tanganyika wamefundishwa sana ohooo ‘amani na utulivu tuuuuuu,huku viongozi yao yakiwaendea na rai mukiendelea kula joto ya jiwe na pia kudanganywa kuwa Tanganyika na Zanzibar ni Tanzania ni nchi mojamawe —vijana wengi hawajui kuwa Zanzibar ilikuwa na hadhi kubwa kuliko Tanganyika (hili mpaka leo).
Naomba hapo mtupie jicho. In short, Kiti kile pale UN cha Zanzibar (au walichokikalia (Tanzania) Tanganyika) na akina Membe wanakwenda kujinasibu — ni kiti chetu, halali yetu, damu yetu na flus za walipa kodi wa Zanzibar.
Ukijumlisha hilo, na utoaji wa maoni ya kuunda katiba mpya: tuseme Warioba na CCM wenzake wakate kuifanya katiba mpya,hii nikuonyesha kuwa wao walikuwa na mpango mwengine ila wameona hautafanikiwa ndio wataivirigiza mpaka isiwe. pia nataka kuwakumbusha kuwa Zanzibar ina KATIBA yake hilo moja na nchi nyengine kabisa sasa vipi sisi tuwasaidie wao kutafuta katiba yao maana wao hawana katiba na hiyo waliokuwa nayo ya viraka ndio ati wamejifanya kuwa ni katiba ya muungano na hayo sio moja katika makubaliano ya muungano kama kweli hawa watwana wana kheri basi walikuwa wasema ok Tanganyika irudi kwanza huko dodoma waliko ifukia wakaifukuwe.
kisha waseme ok Tanganyika iwe na katiba yake mpya na mambo yake kisha sisi na wazanzibari tukae chini meza moja na kutunga katiba ya muungano hapo kweli lakini laaaa lilelile katiba lao lenyeviraka tele ndio hilo hilo wanalolita la muungano na ndio hilohilo wanalotaka sasa kuligeuza geuza kisha watuambiye hakuna haja ya katiba ya zanzibar madamu sasa tunakatiba ya muungano na nakuhakikisheni wakiliambiya lile buju pale ikulu basi litakubali maana ashasema atafanya jambo ambalo wazanzibari hawatamsahau naam asha anza kufanya maana mpaka leo masheikh wamo ndani bila ya hatiya yoyote.ila naona kashachelewa kwa sababu wazanzibari wote hatutaki muungano kwa sababu wazanzibari takriban wote hatutaki Muungano huu uliopo sasa — Je, Zanzibar tufanye nini? Strategy…………..1
Tunaweza kufanya tena na tena petition U.N kwa kutumia maoni hayo hayo ya 66% na ushei plus+plu+ plus, na kusukuma ajenda ya madi yetu U.N na haina shaka kwa mujibu wa taratibu zao, kama wananchi/raia walio wengi kwa kupiga kura au opinions zinakataa jambo fulani — basi wananchi hao watakuwa na mandate ya kudai haki yao kimsingi.
Kwa hivyo kama akina warioba na Salim Ahmeid Salim (watoto wa Nyerere wataikataa maoni ya katiba mpya feki) basi wanashindwa hata kuifanya ‘oral constitution’ — yaani a sort of fatwa.
Mawazo yangu: mimi binafsi nitaona ajabu sana, sana kama mtu kama warioba ataweza kufanya HAKI, wallah laadhimu. Nitaona ajabu sana, na nitaiweka katika world book of record; hana utamaduni huo, wala value system yake haimruhusu kufanya hivyo. Sijui wallah allah yaalam.
Ninasema hivi sio kwa kukata tamaa ila ni historia na mwenendo wa nchi: ni lini (TZ)TANG au Zanzibar ikakubali au kutekeleza maoni ya ya wananchi au kufuata mapendekezo ya report za uchunguzi. LINI, LINI, LINI – kuanzia report za wizi hadi zile za M.V Spice au Skagit — ipi iliyowahi kufuatwa. Hii ni challenge tu ninatoa, haihusiani na mada ya hapo juu.
Tuendelee kudai haki yetu mpaka tuipate Zanzibar. Hata CCM wanataka Zanzibar yetu kama nchi, basi wewe Warioba hujashtuka tu.
No comments:
Post a Comment