Sunday, January 13, 2013

MIAKA 49 YA MAPINDUZI..KILICHO TOKEA SIKU YA MAPINDUZI NA BAADA YA MAPINDUZI YAJUWE MZANZIBARI



Miaka 49 ya Mapinduzi… kilichotokea siku ya mapinduzi na baadaye
Muhariri wetu FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA
Ilipoishia wiki iliyopita: Marehemu mama yake Abdullah Kassim Hanga aliyekuwa anaishi Miembeni, mjini Unguja na mjomba wake Hanga, mzee Ali Ngwengwe, aliyekuwa anaishi Kikwajuni na baadaye kuhamia Dar es Salaam, walijitahidi kujua kilichomsibu mtoto wao, lakini walishindwa kupata maelezo mpaka walipokufa. Sasa Endelea…
WENGINE waliouawa ni pamoja na Othman Sharif, aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar. Alikamatwa akiwa anafanya kazi Bukoba kama daktari wa wanyama na kuletwa Zanzibar, lakini alitoweka na haijulikani kilichomkuta.
Wengine waliokuwa mawaziri ni Abdulaziz Khamis Twala (fedha) na Saleh Saadala Akida (Mawasiliano na Uchukuzi).
Miongoni mwa waasisi wa ASP waliouawa ni Mdungi Ussi (Mkurugenzi wa Sauti ya Unguja), Abdul Nadhif (katibu mkuu), Salim Jinja, Amour Zahor, Jimmy Ringo na Khamis Masoud. Orodha ni ndefu na haijulikani watu hawa walifukiwa wapi baada ya kuuliwa na serekali hihi walioianzisha inayojiita serekali ya mapinduzi mbona ilirudi na kuwauwa wanamapinduzi wake na kuwafukia pahali pasipojulikana mpaka leo...?
Baadhi ya viongozi wa dini, kama Sheikh Suleiman bin Ameir, Sheikh Hashim Haji Abdulla na Maalim Mattar, wote walilazimika kuhamia Dar es Salaam kunusuru maisha yao,abdallah farsi kukimbilia kenya.
Haya yalikuwa madhila ambayo jamii iliyoamua kuwa na utawala wa haki na sheria haifai kuyafumbia macho. Ukweli lazima utafutwe kwa sababu huu sio wakati wa kudanganyana kwa kauli za amani na utulivu!!! Watu hupaswa kusamehe, lakini ni hatari kama wanasahau yaliyopita.
Wapo watu waliotumia muda mrefu wa ujana wao gerezani na wana wa familia zao kutoruhusiwa kuwatembelea. Watu hawa walikabiliwa na kila aina ya mateso.na sasa tunayaona yanajirudia sheikh msellem,sheikh farid,sheikh azzan wako wapi...?
Kwa kweli Zanzibar kumefanyika unyama usioelezeka na ambao lazima uwekwe hadharani kwani ilikuwa tabu kuamini uchafu ule ulifanyika Zanzibar ambapo watu wake walisifika kwa kuheshimu maisha ya binadamu.
Kutokana na upole wao ndiyo maana Wazanzibari wakajigamba kwa kusema: “Zanzibar ni njema atakaye aje”.
Baadhi ya watu wamenieleza kuwa waliwekwa gerezani bila ya nguo kwa siku kadhaa, na kila siku asubuhi na jioni walicharazwa bakora za mpera na kovu za vipigo walivyopata zimebakia kama ushahidi wa maovu waliyofanyiwa na serekali hihi leo inayo jinata kuwa ni serekali iliyoleta haki sawa kwa wazanzibari wote na kuipa jina la mapinduzi matukufu.astahafiru allah hayo mambo mabaya waliofanyiwa wazanzibar ndio matukufa leo..? na watu kusherehekea na kufurahia.
Watu hawa hawakuelezwa makosa yao. Huu ni unyama usioelezeka na unabaki kuwa sehemu ya historia ya siasa chafu za chuki,ubaguzi,choyo na uhasama zilizokuwepo nchini Zanzibar.
Wapo watu waliolala matajiri siku ya Ijumaa na kuamka masikini Jumamosi baada ya mali zao, kama nyumba, mashamba, fedha zilizokuwepo majumbani na benki na magari yao kutaifishwa hivi hivi na wao kuuliwa au kufukuzwa haswa katika nchi huku watoto wao wa kike na wake zao wakinajisiwa na hao wanaoyaita mapinduzi matukufu je huu ni utukufu au unyama..?
Hapakuwepo fidia kwa watu hawa kwani ilikuwa sawa sawa na ule mchezo wa watoto wa Zanzibar wa kutumia chembe za mahindi yaliyochomwa unaojulikana kama kibafte…kibafte…, yaani pata potea.
Baadhi ya watu waliopoteza mali zao waliyaona maisha Visiwani yamewapa mgongo na kuihama nchi waliozaa watoto, waliozaliwa wao na wazazi wao. Kwa watu hawa Zanzibar haikuwa na tofauti na jehanamu.
Wengine walikimbia kwa siri bila ya kuwaaga wake zao wakiwa na nguo za mwilini tu, kwa sababu ingelijulikana wanatoroka ilikuwa sawa na mtu kujikatia leseni ya kuuwawa.
Mengi yameelezwa kwa njia tofauti, lakini zaidi kwa kutegemea misimamo ya kisiasa au chuki kuhusu mauaji yaliyofanyika wakati wa mapinduzi na miaka zaidi ya 10 iliyofuata.wachilia mbali mchezo unaochezwa kila siku za changuzi wazanzibari lazima roho itoke hata ikiwa ni uchanguzi mdogo vipi lazima mzanzibari afee imekuwa kama ni jambo la kawaida sasa.
Wapo watu wanaotajwa kama wahusika wa mauaji na mateso yaliyofanyika, lakini ninaamini kwa jinsi nilivyomjua kwa karibu mzee Karume, watu waliomzunguka huku wakitembea na bastola viunoni na ambao mzee huyu hakuwa na uwezo wa kuwadhibiti ndio waliohusika zaidi sisemi kama yeye hakufanya laa hasha kama kafanya ili kutunza uraisi wake lakini kulikuwa na watu wao ndio wao kazi kuuwa tu na mpaka sasa tunao sina haja yakuwataja majina.
Siku moja, kama miezi minne baada ya mapinduzi, mzee Karume alikuja nyumbani kwa miguu kumtembelea baba yangu na walikumbushana yaliyotokea kabla ya kuwa rais.
Mzee Karume alipopewa kikombe cha kahawa, kijana mmoja aliyekuwa mmoja wa walinzi wake alikirukia na kumkataza asinywe kahawa. Huku akicheka, mzee Karume alikataa na kunywa vikombe viwili na kuwaambia nyie ndio mnaweza kuwa na mawazo ya kuniua, lakini sio rafiki yangu huyu niliyetoka naye mbali.
Nilipojitokeza kumuamkia, mzee Karume alimwambia baba yangu:
“Sheikh, huyu anakaa hapa kufanya nini? Mwache aondoke Zanzibar, hawa watu ni wabaya na hawaaminiki na mimi nipo mbali siku hizi.”
Nilikuja kuelewa baadaye ujumbe mzito wa kauli ya mzee Karume, nilipojikuta kama miaka 10 baadaye nalazimishwa na maofisa wa Usalama wa Taifa wa Zanzibar waliopata mafunzo iliyokuwa inaitwa Ujerumani ya Mashariki iliyoongozwa na dikteta Walter Ulbrich kutaka nitoe ushahidi wa uongo katika kesi ya uhaini baada ya kuuwawa mzee Karume.
Nilichowaambia maofisa hao, mmoja akiwa nimesoma naye shule, lakini alijifanya hanifahamu, kwamba wao ndio waliopaswa kuwa mashahidi kwa kuwa wao ndio waliokuwa wanalipwa na wananchi wa Zanzibar kumlinda mzee Karume.
Kwahivyo, walitakiwa na jamii kueleza walikuwa wapi siku ile ya Ijumaa ya Aprili 7, mwaka 1972 hata mzee Karume akauawa kwa kupigwa risasi. Vile vile walipaswa kueleza kwa nini hawakugundua mapema njama za kumuuwaa mzee karume.
Mpaka leo Zanzibar ukitaja majina ya baadhi ya watu waliopewa majina kama ya Hitler (dikteta wa Ujerumani aliyeanzisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia, 1938-45) na Sancho (mcheza sinema aliyesifika kwa ukatili na mauaji) watu huingiwa hofu na kutetemeka. Hii inatokana na kukumbuka mateso na madhila waliyofanya kwa watu wa kikundi hiki ambao walijiita wanaa wa Mapinduzi.
Watu wengi hutokwa machozi wakielezea mateso na madhara waliyofanyiwa na watu wa kikundi hiki kilichokuwa kikizunguka mitaani kutisha na kupiga watu ovyo na kupora vitu vya thamani, kama hereni, vidani,mbangili na mikufu ya dhahabu. Pia waliua watu misikitini na kunajisi wanawake na wari.
Mara nyingi kati ya miaka ya 1960 na mwanzo wa miaka ya 1970 kulisikika habari za kugunduliwa mipango ya kuipindua serikali na watu wengi, baadhi yao kwa mara ya tatu au nne, kusukumwa gerezani kwa miezi kadha. Karibu wote hao walitoka gerezani wakiwa na hali mbaya kiafya. Wapo waliopoteza nuru ya macho na wapo waliotoka na maradhi ya ngozi na wapo waliofia huko huko jela na mpaka leo hawajulikani walipozikwa.
Ukielezewa kwa urefu mateso waliyopata hasa katika gereza la Kinumoshi, nje ya mji wa Zanzibar, hutapata fikra nyingine yoyote ile isipokuwa kulinganisha na ufashisti uliotokea Ulaya miaka ya nyuma.
Kila lilipotolewa tangazo kupitia Sauti ya Unguja au katika mkutano wa hadhara juu ya kugunduliwa njama za kuipindua serikali, watu walisakwa majumbani kama paka mwizi aliyekula kitoweo cha masikini.
Hofu ilitawala kila pembe ya visiwa na mara nyingi zilisikika habari za watu, wakiwemo wazee, kuteswa na kudhalilishwa na wengine kupigwa risasi na kufukiwa shimo moja.
Miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwepo makaburi ya watu waliouliwa na kuzikwa pamoja ni Chumbuni, nje ya mji wa Zanzibar, ambapo katika miaka ya 1970 kilijengwa kiwanda cha nguo cha Coast Textiles (Cotex) ambacho sasa hakifanyi kazi. Eneo jingine linalosemekana kuwa na kaburi la aina hiyo ni Kama, Kaskazini Unguja.
Uchunguzi huru ndio utaotoa maelezo sahihi ya kilichotokea wakati ule na kusaidia kuiweka sawa historia ya Zanzibar ambayo imepotoshwa kwa sababu ya maslahi ya kisiasa au ya kifedha na kundanganya wananchi ati nchi hii ni ya amani na utulivu nyuma ya pazia wanauwa na kutesa watu kinyama mfano mzuri tunao sasa uamsho wako wapiiiii....?
Simulizi za watu wanaodai kushuhudia ukatili uliodaiwa kufanyika sehemu mbalimbali za Unguja na Pemba zinatisha na sio rahisi kuamini mtu anapohadithiwa. Bila ya shaka wengine huzidisha chumvi utasema lakini sio kweli ni mambo ambayo yametokea hapa hapa zanzibar na nimabaya sana sana.
Ninakumbuka siku moja, mzee mmoja aliyenieleza kushuhudia baadhi ya maovu haya yalipofanyika alibubujikwa na machozi kama mtoto mdogo anayelilia pipi.
Mzee huyu aliniambia hata baada ya miaka mingi kupita kila alipokutana mitaani au sokoni na watu anaodai walihusika na mauaji, mwili wake ulikuwa unatetemeka na kusababisha kukosa usingizi kwa siku mbili hadi tatu.
“Sijui watasema nini kwa Mungu siku ya hesabu,” aliniambia.
Baadhi ya watu waliodaiwa kuhusika na mauaji baadaye walikuja kuugua kila aina ya maradhi. Wengine walikuwa vichaa na kula kinyesi chao huku wakicheka katika siku za mwisho za uhai wao.
Ukisikiliza maelezo ya mateso waliyopata watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji kabla ya kuiaga dunia hii ambayo binadamu hudanganywa na nguvu zake za misuli, fedha alizonazo au madaraka yake, utabaki kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Haya ni mafunzo anayopata binadamu kila siku katika uhai wake, lakini amekuwa hataki kujifunza kwa anayoyaona, kuyasikia au kuhadithiwa. Wakati unapofika na mtu kuona dunia imempa mgongo ndio hujutia maovu aliyowafanyia wenzake.
JE HAYA NDIO YAKUSHEREHEKEA WAZANZIBARI..?
NCHI YA ZANZIBAR IMEPINDULIWA 1964 NA MACHONGO WA KITANGANYIKA NA IMESHIKILIWA KIJESHI MPAKA SASA NA WACHECHE KUPEWA UONGOZI ILI KUZIBA MIDOMO YAO.

No comments:

Post a Comment