Friday, January 4, 2013

DR KUMBI SHEIN APANGIWA KUFUNGUA MRADI BUTU NCHINI ZANZIBAR

Apangiwa kufungua mradi “butu”                                      Afanya uteuzi wenye utata wa hali ya juu                                  

Wengi tunafahamu dunia inapopitia huku nchi nyingi tukiziona zikijikita na kujiingiza kwenye hicho kinachoitwa “KITEKNOLOJIA. Inafahamika fika kuwa Teknolojia ni uwanja mpana, hapa tutazungumza teknolojia moja ambayo ni E-GOVERNMENT.

Kama ilivyotangazwa kwenye ratiba ya sherehe za mapinduzi, hiyo kesho kutakuwa na ufunguzi wa mradi wa E-GOVERNMENT hapo kwenye ofisi ya mradi huo. Imesemwa kuwa Dr Kumbi Shein atafanya ufunguzi huo wakati wa jioni.
Dr Kumbi Shein kwenye mradi huu kauziwa “paka kwenye gunia”. Mradi umegharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi. Sijuwi ni kitu gani Dr Kumbi Shein anakwenda kufungua hiyo kesho hapo Mazizini. Hivi Dr Kumbi Shein anajuwa maana ya E-Government..?
Dr Kumbi Shein E-Government ni zaidi na hicho unachokwenda kukishuhudia kesho. Unachotakiwa kukifahamu ni kuwa unapofunga E-Government ni kwamba chochote unachotaka kukijuwa kilichoko Wizara Fedha, technolojia ikuruhusu kufanya hivyo.
Dr Kumbi Shein E-Government sio kuunganishwa na kuzungumza kwa video conference kwa yule aliye Pemba na Unguja. Hivyo ni kuijaribu “Fibre Cable”. Wala hatuwezi kuiita E-Government.
Dr Kumbi Shein hiyo failure ya mwanzo unaianza kwa mwaka huu mpya wa 2013. Unapousiwa ni kupanua masikio na kusikiliza wengine wanasema nini sia kujidai ujuwaji na huna unalolijuwa.
Kosa jengine lililofanyika ni kwa ule uteuzi wa Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Uteuzi huu umeleta utata mkubwa kwani sector hii imeundwa ndani ya wizara tatu tofauti. Ndani ya Wizara ya Elimu, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na sasa iko kwenye Wizara ya Utumishi na Utawala Bora hivyo kulenga mgongano mkubwa kwa wakurugenzi hao watatu.
Hivi karibuni Dr Kumbi Shein alifanya uteuzi wa Bw Shaaban Choum kuwa Mkurugenzi wa ICT ndani ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, hivyo kuleta mparaganyo mkubwa kiasi cha hata wakurugenzi wengine kususia uteuzi huo na kuahidi kutotoa ushirikiano na mkurugenzi huyu.
Taarifa zaidi inasema kuwa hata uwezo wake ni mdogo sana huku akihusishwa na “mascandal” ya ubadhirfu na mamilioni ya fedha.
Ningemshauru Dr Kumbi Shein amkatae paka hadi atoke nje. Asifungue mradi huu hadi ifahamike fika kwamba mradi umekamilika. Ukifuatilia muundo wa serikali yake hauna tofauti na Serikali ya Watanganyika, hivi kwanini Dr Kumbi Shein hakuiga kule Bara kwa wakoloni weusi wanaotutawala na waliomfanya kuwa waziri asiyekuwa na wizara jinsi walivyofanya mradi wao wa E-Government. Wao wameita “Agency” kabisa na hawakutaka kuutia kwapani mradi huu. Faida yake mradi umekamilika na unafanya kazi yake kama ilivyotarajiwa.
Dr Kumbi Shein, umeanza mwaka mpya na kufeli kiana hii. Kumbuka unakaribia nusu ya muhula wa uongozi wako. Ipo haja ya wewe kujiuzulu haswa maana unatupeleka kubaya au pokea ushauri stahiki kwa wataalam wanaofahamu kwa kina juu ya mradi huu. 20milion USD ni fedha nyingi sana, hazilingani na matumizi ya gharama na utekelezaji wa mradi huu.

No comments:

Post a Comment