Tuesday, January 31, 2012

HICHI NI KIKAO CHA VIONGOZI WALAFI WANAFIKIRIA MATUMBO YAO NA KUTAKA KUIBIYA RASLIMALI ZA WAZANZIBAR

IMG_3725
Kikao cha kamati ya pamoja ya serekali ya TANGANYIKA(( Tanzania)) na Serekali ya Zanzibar kimekutana chinI ya Mwenyekiti wanae muita Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa ((Tanzania))sisi tunajuwa ni makamuwa wa raisi wa TANGANYIKA Dr.Mohd Gharib Bilali.Kikao hicho kilicho husisha Mawaziri,makatibu Wakuu,Watendaji wa Serekali Wakiwemo pia Wataalamu Kilifanyika kwenye ukumbi wa Blue Ubungo Plaza Mjini Dar es Salaam.Wajumbe wa Kikao hicho walikubaliana kuthibitisha kumbu kumbu za kikao cha Kamati ya pamoja ya SMT na SNZ cha Tarehe 2 Juni mwaka 2010 kilichokutana Bwawani Mjini Zanzibar.Halkathalika Wajumbe hao walipitia Taarifa ya utekelezaji wa yatokanayo na Kikao hicho ambayo ni ushiriki Zanzibar katika jumuiya ya Afrika Mashariki((hatutaki muungano na tanganyika vipi sasa wanataka kujadili mambo ya afrika mashariki wazanzibar hapa ndio tuelewe kuwa sisi rai hatuthaminiwi wao wanafanya wayatakayo wavimbe mitumbo yao)), Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia,Uvuvi katika ukanda wa Bahari kuu na Ushirikiano wa Zanzibar katika Tasisi za nje.((mbona hawakutaja gesi yao,almasi zao,thahabu zao,tanzanaiti zao wala maka ya mawe yao hawataji kila ukisikia ni mafuta ya zanzibar ndio muungano huwo....?MIJAMBAZI MIKUBWA NYIE SIO VIONGOZI.
Tarifa nyingine ni ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika tasisi za Muungano, Mgawanyo wa mapato na faida yatokanayo na Bank kuu , Malalamiko ya wafanya biashara kutozwa kodi mara mbili waingizapo Bidhaa zao Tanzania Bara,usajili wa vyombo vya moto, likiwepo pia ongezeka la gharama za Umeme wa Tanesco kwenda ZECO uharamia na utekaji nyara meli.
Katika majadiliano hayo Mwenyekiti wa kikao hicho Dr Mohd Gharib Bilal aliagiza mamlaka zinazo husika kutowa maelezo ndani ya kipindi cha miezi mine utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asilia.((MUNAMSIKIYA ZIMWI HUYU ANAVYOTAKA KUIMALIZA ZANZIBAR..?
Mapema mwana sheria mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Othmani Masoud Othman Taratibu zote na Baraka kuhusu swala hilo zimeshachukuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Baraza la Mapindizi na Baraza la Wawakilishi na kuliwakilisha Serekali ya Muungano kwa hatuwa za kisheria.
Naye makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisisitiza hoja ya kuwa na ratiba malum ya vikao pamoja na kupunguza urasimu wa utekelezaji wa mamuzi yanayofikiwa katika vikao hivyo vya pamoja.
Balozi Seif alisema itapunguza kero zilizopo na hatimae kuamsha ari ya kuimarisha Muungano kwa pande zote mpili.
Nirahisishieni kazi ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa wajumbe wake wako Solidarity na hakuna mjumbe wa CCM wala CUF katika swala lolote linalohusu Muungano,alisisitiza Balozi Seif.
Katika kikao hicho upande wa wajumbe wa Serekali ya Muungano uliongozwa na Waziri mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda wakati ule wa Zanzibar uliongozwa na makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi seif Ali Iddi.

NCHI YA TANGANYIKA INAIZIKA ZANZIBAR HALI YA KUWA ZANZIBAR IHAI HAIJAFA



Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,tuna muita mshirika wetu wa muungano alitukatalia na kutupa munda tutoke haraka na ndio alipotupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salimin Amour wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingilia. Kwani, zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.
MISUMARI YA MWISHO INAPIGWA SASA  NA TANGANYIKA ((TANZANIA)) KATIKA JENEZA LA ZANZIBAR. JE.WAZANZIBAR MPOOOO AU MUMELALA BADOO.. ?

Ombi la Januari 18,2012 la Tanganyika (Tanzania ) huko Umoja wa Mataifa,New York,  kutanuliwa  mipaka yake ya baharini  ni misumari ya mwisho inayopigwa  kufuatia ule wa  kwanza  katika JENEZA la Zanzibar  hapo April 26,1964. Mara tu baada ya  kuapishwa rasmi Mwalimu Nyerere  kuwa rais wa Jamhuri  ya Muungano ya Watu wa Tanganyika na Zanzibar,kanuni yake ya kwanza aliotunga (decree), ilikua kuifuta Tanganyika  kwa njia za  kiinimacho  na kuibua Tanzania ambayo ni ile ile Tanganyika  aliyoifuta lakini imeibuka na mipaka mipya ya aridhini.Ilijumuisha   visiwa vya unguja na Pemba. Sasa inajiandaa kupiga misumari ya mwisho kwa kutanua zaidi mipaka yake ya baharini na kiliomo ndani yake tangu dagaa hadi papa.mashamba mpaka mjini watu mpaka miti hii ni dalili ya azimio la arusha inaletwa tena kwa njia nyengine bila ya wazanzibar kufahamu nini kinaendeleya ila wakipata ruhusa tu tujuwe tumekwisha tutahamishwo zanzibar tukitaka tusitake ili waigeuze watakavyo kufanya ulanisi na kila balaa.
Tangu 1964, misumari mingi imekuwa ikigongomelewa jeneza letu  tena hatua kwa hatua; na sisi wazanzibari  twatazama macho tu.
Kufuatia Muungano uliofanyika bila umma kuulizwa ndewe wala sikio, akiba kubwa ya fedha za Zanzibar katika Bodi ya ile iliokua Jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI  ziliporwa na tunaemwita Mshirika wetu wa Muungano na kuzitia  kibindoni katika Bank yake (BOT) bila ya ridhaa  umma  au ya serikali yatu. Shabaha ilikua  ni kuiua Zanzibar  kiuchumi ili kuidhibiti. Sehemu ya Zanzibar katika  “Currency Board ” ya Jumuiya ile  ilikua 11.2%. Huo ukawa msumari mwengine kati ya mingi katika jeneza letu. Licha ya juhudi nyingi za Viongozi wetu , walishindwa kuzuwia hilo. Kwani wenzetu hizo wanazoziita “KERO” ndio “MISUMARI” wanayoigongomelea JENEZA LETU hadi watapotuzika kabisa.
Msumari mwengine mjarabu kabisa ni kule  kuunganishwa kwa Afro-shirazi party (ASP) na TANU, 1977 kinyume na  Marehemu mzee Karume alivyowausia   wandani wake wasifanye,kwani yeye binafsi hakuridhia hilo katika utawala wake mzima wa miaka 8 .Kwa msumari huo,hatima ya kisiasa ya Zanzibar ilianza kuamuliwa  Dodoma badala ya kisiwandui. Rais wetu Aboud Jumbe alipofanya nyoko huko Dodoma, 1984 , alikiona kilichomtoa kanga manyoya. Kuanzia hapo hata viongozi wetu wa Zanzibar bila ya ridhaa ya Dodoma,ni mwiko  kukalia kiti cha Urais. Wenzetu wanatuchagulia hata   marais wetu-aibu gani hii ?
Msumari mwengine katika jeneza la Zanzibar ni kuondolewa kwa wadhifa wa ” Makamo-rais ” na kumfanya Rais wetu kana kwamba ni   rais wa kilabu cha mpira cha ” MIEMBENI SPORTS CLUB”. Hana nchi hata akiwa na bendera....SASA AMEKUWA BOYAA TU SHEIN SIO RAISI.
Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,ana jiitaa mshirika wetu wa muungano alitutia munda na kuupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salimin Amour wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingia. Kwani,  Zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.
KABLA SHEREHE ZA MIAKA 50 ZA MUUNGANO 2014, MAITI  ya (ZANZIBAR) iwe tayari kuzikwa kupitia KATIBA MPYA YA SEREKALI YA TANGANYIKA. Zanzibar inazikwa kule kule UMOJA WA MATAIFA,NEW YORK, na sio Mwanakwerekwe ambako kaburi lake lilichimbwa  tayari 1964   pale kiti chake kama dola huru huko kilipotoweka kwa  kiini macho. TANGANYIKA((Tanzania)) inajua kucheza turufu  zake huko  ili kuizika Zanzibar katika  kaburi lile lile iliochimba 1964  kufuatia Muungano FEKI.
Baada ya kupora fedha zetu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki iliovunjika ,sasa tunae muita mshirika  wetu wa Muungano amejianda kupora gesi na mafuta yetu kwa  njia ya kuitanua mipaka ya bahari kama alivyotanua mipaka ya aridhi katika ile Tanganyika kubwa  kwa jina la ((Tanzania.)) Wakati maliasili zao kama gesi,Tanzanite, dhahabu, almasi ,makaa ya mawe na nyenginezo, ni  mali zao pekee yao, mafuta na gesi ya Zanzibar na Pemba  eti ni ubia.
VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR NA SISI UMMA WA ZANZIBAR,  TUTATUMBUA MACHO MPAKA LINI ? AU
MPAKA TUZIKWE KABISA HUKU SANDA TUMESHASHONEWA  NA TUNAIONA ?
Kuna usemi “Kila  Umma  hupata viongozi  uliostahiki kuuongoza.Ukiwa  Umma  ni ngangari, utapata viongozi ngngari kama akina  Jussa,Hamza na Mansuri -wenye kupaza sauti kuutetea Umma.La ,ukiwa  Umma ni wazembe, watapata viongozi wazembe.
Wazanzibari mpo ?
Tusigeuke  ile hadithi ya Mnyamwezi ” Ninamtajama tu” kumbe mwenzake anamharibu.Eti anatafuta ushahidi.
USHAHIDI kuwa tuna muita mshirika mwenzetu wa Muungano hakuwa na nia njema tangu awali, ilidhihirika pale alipopiga msumari wa kwanza,April 26,1964 kwa kuifuta Tanganyika .
Ilikua tangu wakati ule Viongozi wetu  wawaambie  ndugu zetu kuwa, BILA YA TANGANYIKA, HAKUNA MUUNGANO.Mumeivunja wenyewe. TUNAWEZA HATA KUWAAMBIA HIVYO LEO LAIT”I TUNA VIONGOZI NGANGARI- KERO ZIMETOKA WAPI IKIWA HAKUNA MUUNGANO.JAMANI “SI ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO ?”
Ningelikua mimi ni  Rais wa Zanzibar,ningekwenda Studio za Raha leo na kulihutubia Taifa nikiwaamrisha wabunge wote wa Zanzibar katika Bunge la Muungano huko Dodoma, warudi Zanzibar mpaka  kwanza waziri-mkuu  Pinda,kwanza  awataka radhi  Wazanzibari na Rais wao pili hao wanao jiitaa washirika wetu katika huo Muungano FEKI,waifufua Tanganyika  walioifuta  kwa kini-macho.
Je, Wazanzibar mpo au tunasubiri kuzikwa kabisa  2014?..lakini UBAYAA HATUNA RAISI HAPA ZANZIBAR TUNA BOYAA TU LAELEYA KATIKA MAJI YA ZIWA TANGANYIKA.
ILI KUZUWIA KUPIGWA MSUMARI WA MWISHO KATIKA JENEZA LETU  ,TUDAI TUJADILI KWANZA UHALALI WA MUUNGANO NA KUIULIZA NCHI TULIYO UNGANA NAYO TANGANYIKA IKO WAPI IRUDI NA KAMA HAWATAKI BASI NDIO TUNAVUNJA KABISA MUUNGANO MAANA KWANZA HAKUNA MUUNGANO KUNA UBABE TU TUSIKUBALI KUJADILI KATIBA MPYA MAANA HAKUNA NCHI TULIYO UNGANA NAYO SASA TUNAJADILIYANA NA MTU ASAYE KUWEPO......? PIA TUKUMBUKENI KUWA. ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO !

Tuesday, January 24, 2012

DAWA YA MOTO NI MOTO GNU WAZANZIBAR TUNATAKA KITI CHETU CHA U.N.


Hakuna asie fahamu kuwa kiti chetu cha umoja wa mataifa ndicho kinachotumiwa na jina la ((tanzania)),watanganyika kwa sababu zanzibar ndio iliyo  jiunga na U.N.hapo awali sio TANGANYIKA na ushahidi upo na kila kitu TANGANYIKA haijawahi kujiunga na U.N. wala U.N.hawaitambuwi nchi inayoitwa TANGANYIKA ndio walipo amuwa kufanya muungano FEKI wa tangnyika na zanzibar wakapata tanzania yao FEKI ndipo walipotambulika kwa hiyo hawa jama  wametutumia muamvuli wa zanzibar kimataifa kujitajirisha wao,kiuchumi ,kijamii,kibinafsi,yote haya ni kutawala zanzibar na kuipoteza katika ramani ya dunia.Kisu cha kutawaliwa ni chetu wenyewe,kisu hichi kitatuuwa wazanzibari wote ni vyema tukakidai kisu hichi kabla hakijatutuoa machango,maana kisu hichi tumempa chizi hasikii haoni,wakati umefika sasa kukichukua wenyewe,ili tuweze kupunguza jeuri hawa watwana watanganyika.
Ndio maana wanafanya vile wanavyotaka wao wenyewe,imefika wakati tudai kiti chetu cha U.N,tufanye siku tukakenshe nje ya baraza la wakilishi kusisitiza azimio hilo katika serekali yetu ya GNU tuone kama itatusikia sisi wananchi wake au itakuwa kama ile ya SMZ inayosubiri amri kutoka kwa mabwana zao DODOMA.
Tunawaomba viongozi wetu,waache kubembejea serikali ya muungano suala la mipaka ya bahari ya zanzibar,wakati hawa watanganyika hawaheshimu maamuzi ya baraza la wakilishi na katiba yetu,mangapi tuliwaeleza watanganyika wayaondoe kama ni kero za muungano kama ushuru mara mbili kwa wazanzibari,suala la mafuta na mipaka ya zanzibar,yote haya hawayataki kuyaheshimu na ndio kwanza yanashika kasi kila kukicha.Tuache kujidanganya kuwa tutawaandikia barua serikali ya muungano maana kwanza hakuna huo muungano kuna ubabe na unywanywasazi wa rai wa kizanzibar katika nchi yao wenyewe na hawa wanyika kuwanyanyasa wazanzbar haikuanza leo na haita ishaa leo wa kesho mpaka muungano huu FEKI ufe tuwe na jeshi letu polisi wetu yani vijana wa zanzibar ndio yatakwish.la sivyo tutakuwa tukidanganyana tu.na wala tusifikiri kuwa watasimamisha zoezi hilo,hata siku moja hawatafanya kosa,wakati huu tufunge firago vyetu tuende huko huko umoja wa mataifa kulimaliza tatizo hili kwa sheria za kimataifa na mkataba wa muungano na katia yetu.Azimio la kuenda umoja wa mataifa.Kuzuiya mipango ya uwombaji eneo la bahari.Kudai kiti chetu cha umoja wa mataifa.Kudai mkataba ambao uliruhusu kuondolewa zanzibar katika U.N,na kama haupo mkataba huo ulio sainiwa na sehemu mbili ya muungano,tanganyika itatulipa fidia zetu.Mkataba wa muungao pia tunauhitaji ulio unda jamuhuri ya muungano FEKI kama hakuna siku hiyo hiyo zanzibar ijitangaze kuwa ni nchi kamili na kuomba hifadhi ya kijeshi U.N mpaka itakapokuwa na jeshi lake la kuliamini yani vijana wa zanzibar sio wakuryaa na watwana na machongo waliojazwa katika makambi hawana wanalofanya zaidi ya kulewa na kula bure nakutia dada zetu mimba kisha siku za changuzi wanatuuwa na kutupinga na kutunyanyasa ndani ya nchi yetu wenyewe.
Mungu ibariki zanzibar na watu,tupe moyo na nguvu amiin

BAADHI YA WAWAKILI WAMTAKA ALI JUMA SHAMUHUNA AJIUZULU KWA KUIUZIYA SEHEMU YA BAHARI NCHI YA TANGANYIKA BILA YA KUIARIFU SERKALI YA GNU


Wajumbe wengi wa baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar wametaka Waziri wa Maji, Makaazi, na Nishari Zanzibar Juma Shamhuna ajiuzulu. kufuatia sakata la kushirikiana kinyemela na serikali ya TANGANYIKA au feki jamhuri ya muungano wa ((Tanzania)) kufanikisha ombi la kutaka nyongeza ya eneo la bahari ikijumuisha mipaka ya visiwa hivyo, pasipo kulishauri baraza hilo.Wito wa kutakiwa kujiuzulu kwa waziri huyo mkongwe visiwani Zanzibar unafuatia hoja binafsi iliyotolewa na mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa. Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamemtaka waziri wa nishati Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna ajiuzulu, pamoja na kupitisha azimio la kuitaka Serikali ya Zanzibar kuwasilisha mara moja barua ya kupinga kitendo cha Serikali  ya TANGANYIKA au feki Jamhuri ya Muungano wa ((Tanzania)) kuwasilisha ombi la huko Umoja wa Mataifa (UN) kuongezewa eneo la kiuchumui katika bahari kuu (EEZ).
Azimio hilo limefuatia hoja binafsi iliyowasilishwa na Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe  (CUF) Ismail Jussa Ladhu kuhoji uhalali wa serikali ya muungano kuwasilisha ombi hilo UN bila kuishirikisha Zanzibar kikamilifu.
Katika kukabiliana na serikali ya muungano, Jussa akitoa mapendekezo manne ambayo wajumbe wote wapiga kura kuridhia pamoja na pendekezo la tano linaloitaka baraza la mapinduzi Zanzibar kusimamia utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa na baraza la wawakilishi mwezi Aprili mwaka 2009.
Mapendekezo ya Jussa ni kama ifuatayo: Kwamba seriklai ya Zanzibar iiandikie serikali ya muungano barua ya kusitisha mara moja mchakato wa maombi ya kutaka kuongezewa eneo la ukanda wa bahari kuu, na kwamba iwapo serikali ya muungano ikipuuza serikali ya Zanzibar ipeleke ujumbe UN kutaka mchakato usimamishe.
Wiki iliyopita Serikali ya TANGANYIKA au feki Jamhuri ya Muungano kupitia Waziri wake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Anna Tibaijuka iliwasilisha maombi katika umoja wa mataifa kuomba eneo la ziada la maili 150 nje ya eneo la sasa la maili 200 za ukanda wa kiuchumi wa eneo huru la bahari.
Katika mchakato huo serikali ya muungano ilimshirikisha waziri wa nishati wa Zanzibar,  Ali Juma Shamuhuna kama alivyokiri mwenyewe kwa wajumbe wenzake ndani ya baraza la wawakilishi wiki iliyopita. “Kama waziri ni serikali, basi Zanzibar ilishirikishwa,  na nilimpeleka msaidizi wangu kuniwakilisha, lakini kama serikali ni baraza la mapinduzi, basi haikushirikishwa katika jambo hili,” Shamuhuna alisema.
Kauli yake ilizuwa maswali mengi kwa wajumbe wenzake miongoni mwa maswali hayo yakiwa ni inakuwaje jambo zito kama hilo Shamuhuna analibeba peke yake wakati baraza lilipitisha azimio linalotaka eneo lote la bahari la EEZ pamoja na maliasili ya mafuta liondolewe katika orodha ya muungano?
Serikali ya TANGANYIKA NA FEKI muungano haijajibu hadi leo kuhusu azimio la baraza, lakini viongozi wa seriklai ya muungano wamekuwa wakitoa kauli kwamza matatizo yote ndani ya muungano yatashughulikiwa.
Katika kuonesha kutoridhika na Shamuhuna, ndipo baadhi ya wajumbe wakamtaka waziri huyo ajiuzulu mwenywe au rais amtimue kazi kutokana na madai ya kuidhalilisha baraza baada ya kushirikiana na Prof Tibaijuka kupeleka ombi UN.
“Inakuwaje waziri anakuja hapa bila ya kuwa na msimamo juu ya maswala nyeti kama haya…waziri Shamuhuna inabidi ajiuzulu au rais amuwajibishe. Kama hatua haitochukuliwa, tunaweza kutumia kifungu cha 41 kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali…,” alisema mwakilishi Hamza Hassan Juma (CCM Kwamtipura).
Wajumbe wengine ambao walitoa kauli za waziwazi dhidi ya Shamuhuna na kumtaka aachiye ngazi ni Hija Hassan Hija (CUF- Kiwani), Mbarouk Wadi Mussa (CCM- Mkwajuni), Asha Bakari Makame (CCM wanawake), Omar Ali Shehe (CUF-Chakechake), na Rashid Seif Suleiman (CUF- Ziwani).
Ali Mzee Ali (CCM kuteuliwa) alitumia lugha ya kiprofesa pia kumlaumu Shamuhuna kwamba alijitia kitanzi mwenyewe katika kuelezea ushiriki wake katika swala ambalo baraza tayari limetolewa msimamo mwaka 2009.
Juhudi la mwanasheria mkuu wa serikali Othman Masoud kujaribu kutaka kumkingia kifua hazikufua dafu, kwani aliposema kwamba ni mapema kumhukumu mtu barazani  alijibiwa kwa wajumbe kuguna, na baadae Jussa kumwambia kuwa wazanzibari ambao wamekuwa wakimheshimu sana wameanza kuvunjika moyo naye tangu alipopata wadhifa wa mwanasheria mkuu.
Hivi sasa kinachosubiriwa kwa hamu kubwa ni jibu la serikali ambalo makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliahidi wiki iliyopita kuwa katika kikao cha baraza la mapinduzi swala hilo litazungumzwa na kujadiliwa ikiwa pamoja na kuangalia athari ya ombi la serikali ya muungano la kutaka nyongeza ya EEZ kwa Zanzibar.

JE SHEIN AU SIJUWI CHENI UTAMTIMUWA AU NDIO FINIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE...?USIPO MTIMUWA MTU KAMA HUYU NDIO KWELI HATUTAKUWA NA IMANI NA SEREKALI HII MOJA PILI NDIO UNAZIDI KUTUJULISHA KUWA WEWE NI BOYAA TU UMEWEKWA HAPO AMRI YOTE INATOKA DODOMA ALA UJUWE WALIKUWEPO KAMA WEWE MABOYAA NA SASA WAPO WAPI HABU JIULIZE CHENI JIULIZE.

VATICAN YAVAMIA NCHI YA ZANZIBAR KWA KISHINDO KIKUBWA KABISA

KAZI kubwa inayofanywa        
na taasisi za Kikristo
kutoka Tanzania Bara na
nje ya nchi, sasa inaanza
kuzaa matunda.
Digital StillCamera
KUMBUKENI ZAMANI ZANZIBAR WATU WAKIJA KUSOMA DINI NA ILIKUWA
IKITWA MAKKA YA EAST AFRICA SASA IMEKUWA VATICAN YA EAST AFRICA
SHEIN NA SEIF MUTAMUELEZA NI M/MUNGU SIKU YA KIYAMAA..?NA VIONGOZI
WOTE WA ZANZIBAR PIA MUTAMUELEZA NINI M/MUNGU SIKU YA KIYAMA....?

M a k a n i s a y a k i z i d i
kuchipua kama uyoga,
nazo skuli za awali, msingi
na sekondari za Kikristo
zinazotoa elimu bora,
zinaibuka kila mwaka na
kuwa kimbilio la wazazi
wengi wa Kizanzibari.
Katika eneo la Tomondo
n a M o m b a s a k u n a
makanisa zaidi ya kumi na
skuli za Kikristo pamoja
na maduka ya dawa, hali
ambayo inafanya mji huo
mdogo kuonekana kama
‘Vatican’ ya Zanzibar.
Hali kama hiyo ya ‘Vatican
Tomondo’, inaenea pia
kuelekea Kiyanga, Bambi
na shamba nyengine.
H a l i y a ‘ V a t i c a n
Tomondo’ inaonekana pia
Machui na Kiboje.
“Machui wamejiimarisha
na wanazidi kila uchao.
Huko Kiboje unaweza
kwenda msituni ghafla
ukatokezea kijiji kikubwa
a m b a c h o h a k i k u e p o
kabisa awali, ukawakuta
(Wakristo) wamejaa.”
Anasema mchangiaji
mmoja akitoa maoni yake
juu ya kasi ya kusambaa
U k r i s t o n a Wa k r i s t o
Zanzibar.
“Huo ni mmoja katika
m i k a k a t i y a o k u w a
waongozeke Zanzibar bila
sisi kushtuka, ili siku moja
ghafla waje watwambie
kuwa “hamuwezi kuweka


sheria za Kiislamu kwa
sababu tupo 50-50 (sawa
kwa sawa).” Anasema
mchangiaji huyo.
Uchunguzi uliofanywa
na mwandishi umebaini
kuwa, wakati taasisi za
Kikristo zikizidi kufanya
j u h u d i k i m ya k i m ya ,
baadhi ya Masheikh na
wanaharakati wa Kiislamu
wamekuwa wakilalamika
na kushutumu taasisi
za Kikristo hasa kutoka
Bara kwamba zimekuwa
zikiwahadaa wananchi wa
Zanzibar na kupora ardhi
zao.
Madai yanayotolewa ni
kuwa ‘Wabara’ hao Wakristo
wanawatumilia baadhi
ya Wazanzibari kupata
viwanja wakidanganya
kama wanataka kufanya
shughuli za kijamii, lakini
baada ya muda mchache tu,
“unashtukizia washajenga
k a n i s a n a wa n a we k a
msalaba na kengele”.
L a w a m a k u b w a
wamekuwa wakitupiwa
w a n a n c h i a m b a o
w a m e k u w a w a k i u z a
maeneo yao, lakini nao
wamekuwa wakijitetea
k u w a n i u m a s i k i n i
unaowasukuma kuuza kile
ambacho ndio wanaona
kitawasaidia.
Wamesema, tatizo hili
hawezi kulaumiwa mtu
binafsi mmoja mmoja,
bali ingetakiwa jamii ya
Waislamu, labda kupitia
taasisi zao kuliangalia kwa
mapana yake.
“ Wa i s l a m u h a t u n a
mfumo wa zaka na sadaka
wa kusaidia masikini

wala mpango mkakati wa
kuangalia mustakbali wa
Uislamu Zanzibar, sasa
utamlaumi vipi mtu binafsi
anayeuza eneo lake ili apate
kujikimu kwa chakula na
ada ya watoto ya shule?”
Alihoji Mzee mmoja
katika moja ya maeneo
ya shamba ambapo taasisi
za Kikristo zimekimbilia
kununua ardhi.
B a a d h i y a w a t u
wamelinganisha suala
hili la ardhi ya wazalendo
kuuzwa kwa wawekezaji
wa nje (Wakristo) na
mashirika ya kidini ya
Kikristo sawa na ile hali
iliyotokea kwa Wapalestina
ambapo ardhi kubwa
iliuzwa kwa Mayahudi.
Wa n a o t o a h o j a h i i
wanasema kuwa hata
ukiangalia suala la ulevi,
zipo sheria lakini hazifuatwi
kinyume chake baa na
vilabu vya ulevi huwekwa
kila mahali kwa leseni za
serikali jambo linalotia
s h a k a k wa m b a l a b d a
huenda kuna mkakati wa
kusambaza ulevi kuharibu
jamii.
Baadhi ya Wazanzibari
waliolijadili suala hili hasa
kupitia katika mtandao
wanasema kuwa itakuwa ni
fikra potofu kudhani kuwa
Zanzibar ni ya Waislamu
na Wakristo hawana haki.
“Naona kama ni kheri
tukaacha kutiana chuki
hususan kupitia dini na
kujaribu kuleta mitafaruku
ya kidini. Nadhani Zanzibar
wapo Wakristo, mabaniani
na wengine wengi. Hawa

ni minorities (wachache),
l a k i n i t u k u b a l i a n e
kama wapo!” Amesema
mchangiaji mmoja.
“ N a d h a n i w e n g i
watakuwa wamesoma
japo na Mkristo mmoja
skuli, binafsi nimesoma
na Mkristo nilipofika
sekondari. Huyu alikuwa
akitokea Mkwajuni, huko
Wakristo wapo na hilo
hatuwezi kuliepuka.”
Aliongeza.
“ S i o To m o n d o t u ,
‘Vatican City’ kubwa
ipo Machui huko hadi
n g u r u w e w a p o n a
daladala za Waislamu
ndio zinasafirisha pombe.”
A n a s e m a m c h a n g i a j i
mwingine.
Hata hivyo, wengine
wanasema kuwa kama
ilivyo Marekani, Italy,
Ufaransa na Uingereza
ambapo Waislamu wapo,
lakini katika hali halisi ni
nchi za Kikristo.
“Ni kweli Wakristo
walikuwepo tokea zamani,
lakini sio kutuharibia
ardhi yetu kwa kuzijengea
makanisa na majumba
ya madanguro.” Alisema
m c h a n g i a j i h u y o n a
kuongeza akisema kuwa:
“Hizi chuki lazima
zitakuja, kwa vile kwa
nini wananchi wazaliwa
hawapati viwanja na
badala yake wapewe
hawa ili wajenge makanisa
ambayo mengi hayana
hata hao wanaokwenda
kufanya hizo wanazoita
ibada zao,
bali hii ni mipango
maalumu iliopangwa
kuja kukichafuwa kisiwa
chetu. Mbona hizo nchi
za nje hawakubali misikiti
ijengwe kiholela tu?,
Tusijitie
h u r u m a k wa n i l e o
hii Muislamu mbali ya
kujenga misikiti,bali kuvaa
hizo hijabu za kichwa tu
basi imekuwa kero, sasa je,
sisi wanaojenga makanisa
k i h o l e l a ? A l i s e m a
mchangiaji huyo katika
mtandao.
“Ni lazima tupinge
haya kwa nguvu zote,
na tunajuwa kwamba
Wakristo kweli tumekaa
nao tokea zamani lakini
sio kutujengea makanisa
kiholela kwani nina imani
Wakristo wote hapo labda
ni asilimia 4, sasa hata
yakijengwa yakiwepo
m a k a n i s a m a t a t u t u
yashawatosha.”
U c h u n g u z i w a
mwandishi umebaini
kuwa suala hili la ujenzi
wa makanisa na shule
z a K i k r i s t o , l i m e z u a
mjadala mkali katika
mitandao ambapo wengi
wamekuwa wakipinga
huku wengine wakisema
kuwa wa kulaumiwa ni
Wazanzibari wenyewe kwa
maana kuwa kama wao
wamelala wasidhani kuwa
na wengine wamelala au
wamekaa tu kupiga porojo,
wanafanya kazi.
W a n a s e m a j a p o
inaweza kudaiwa kuwa
kwamba hii ni njama
ya mfumokristo, lakini
Waislamu Wazanzibari nao
wameweka mikakati gani
na kuitekeleza kukabiliana
na njama (conspircy) hizo?
Wanahoji.
Wanaotoa hoja hiyo
w a n a t a h a d h a r i s h a
wakisema kuwa watoto
wanaosoma katika skuli
za Kikristo hivi leo ambazo
zinatoa elimu bora kuliko
ilivyo Benbela na nyingine
za serikali, baada ya miaka
m i c h a c h e i j a yo n d i o
watakaokuwa watawala
wa Zanzibar.
“Lawama kubwa ni sisi
wenyewe Wazanzibari,
sisi wenyewe wananchi,
wananchi ndio serikali
sasa nani wa kulaumiwa
? Skuli haziboreshwi,
zimekuwa mahala pa
watoto kujifunzia mipasho
na uhuni wa kila sampuli,
taasisi za Kiislamu na
watu binafsi hawajengi
n a k u e n d e s h a s h u l e
bora, wakijenga wengine
tusilalamike.” Imeandikwa
katika maoni ya mchangiaji
mmoja katika mtandao.
“ N i w a j i b u w e t u
kuilinda nchi yetu, dini
yetu na Utamaduni wetu,
hakuna mwengine wa
kuyafanya hayo isipokua
sisi Waislamu Wazanzibari.
Muhimu Wazanzibari
tuelewe kuwa kizazi chetu
kitakuja kutulaumu kwa

kuiachia nchi ikichukuliwa
na kutoihami dini ya
Kiislamu wakati uwezo
wa kufanya hivyo tunao.”
Ameongeza.
W a l i o c h a n g i a
wa k i wa n a m t i z a m o
huu wanasema kuwa
kulalamika haisaidii kitu
na la muhimu kufahamika
ni kuwa kila jamii ina
haki ya kujiimarisha ili
kuhakikisha uwepo wake
kwa vizazi vijavyo.
K w a m b a k a m a
Waislamu wa Zanzibar
hawafanyi harakati za
kuwaendea Wakristo wa
Bara na kuwaita katika
Uislamu, Wakristo wa
Bukoba na Tukuyu wao
wakija Tomondo na Chake,
huwezi kuwalaumu.
Z i p o t a a s i s i k a m a
JUMIKI, JUMAZA na
UAMSHO, je, hizi zina
mpango wa kuwaendea
Wakristo wa Kyela, Kibosho
au Sumbawanga?
S a s a k a m a h a z i n a
m p a n g o h u o , w a
kulaumiwa sio Kadinali
Pengo anayetuma vijana
wake kuweka misingi
ya kuimarisha Ukristo
na kudhoofisha Uislamu
Zanzibar.
Kwa upande mwingine
imeelezwa kuwa nguvu
kazi na rasilimali kubwa
ya Waislamu imekuwa
ikitumika katika siasa
zisizo na munufaa kwa
jamii badala ya kuzielekeza
katika mambo yenye tija.
“ K a m a u l e u m a t i
unaokusanyika katika
mikutano ya CCM na
CUF ungeelekezwa katika
jambo moja tu dogo na
jepesi la usafi wa mji,
leo Zanzibar isingekuwa
chafu kiasi hiki, lakini
tembea mjini uone na
labda ulinganishe na miji
mingine yaTANGANYIKA(( Tanzania)).”
A m e s e m a  S h e i k h
mmoja ambaye hata hivyo
hakutaka kutajwa jina lake
gazetini.
Sheikh huyo ambaye
anawalaumu wanasiasa
kwa kushindwa kutumia
nguvu kazi ya mashabiki
wao kufanya mambo
y e n y e m a n u f a a k wa
nchi, amewalaumu pia
viongozi wa Kiislamu kwa
kushindwa kuwatumia
waumini wao kuendeleza
Uislamu badala yake nao
wamebaki wakilaumu
makanisa.

Saturday, January 21, 2012

NI KWELI WASEMAVYO KUWA ZANZIBAR SIO NCHI SHEIN NI BOYAA KAMA ALIVYOKUWA KARUME KWA NYERERE BOYAA TU


HAPA NDIO TULIPO MALIZWA SASA NI KAMA KUMSUKUMA MLEVI TU










NATUJIULIZE TUNATOKA WAPI TUNAKWENDA WAPI NA VIONGOZI TULIYOKUWA NAO NA AMBAO TUNAO SASA NINI TAFAUTI AU NGOMAA NDIO ILE ILE....?
PALAU,BIRIANI,WALI WA MAJI AU WA NAZI LAKINI WOTE NI NINI
MCHELE BADO TU WAZANZIBAR HATUJA AMKAA

GNU YATAKIWA KUTOWA MAELEZO KUHUSU NYONGEZA YA MASAFA YA BAHARI

RUSHWA MBAYA JAMAA MMAUZAA NCHI NZIMAA SASA MPAKA BAHARI YA MWENYEZI MUNGU PIA MUUNAUZAA....

kificho1
 January 20, 2012
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho akiendesha kikao cha baraza hilo kinachoendelea katika ukumbi wa Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho ameitaka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kutoa taarifa katika baraza la mawaziri suala la TANGANYIKA kuwasilisha ombi la nyongeza masafa ya bahari kuu kwenye Umoja wa Mataifa. Kificho alisema hivyo baada ya Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna kusema kwamba yeye kama wizara taarifa anayo hiyo lakini katika baraza la mawaziri hakuna taarifa ya jambo hilo iliyowasilishwa.
“Nakuomba waziri mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna kuleta taarifa hiyo baraza la mawaziri kwa ajili ya kuifanyia kazi pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi” alisema Spika Kificho.
Kificho, aliwaambiwa wajumbe wa baraza hilo wasubiri na kuiagiza Serikali kulifuatilia suala hilo kikamilifu ili wananchi wa Zanzibar wajue lengo la hatua hiyo kwa serikali ya TANGANYIKA((LENGO TUNALIJUWA NIKUTUMALIZA KABISA MAANA WASHATUMALIZA TOKA FATHER KARUME ALIPOSEMA NDIO TUMEUNGANA ILIKUWA KISHA SASA NI KUJIKOMBOWA TU SIO DOMO DOMO TUPU KAMA DEBE.
Alitoa agizo kwa serikali kutoa maelezo juu ya upande mmoja wa Muungano kupeleka maombi hayo kwa Umoja wa Mataifa bila kuushirikisha upande wa pili.
Aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufuatilia jambo hilo kabla ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayajatolewa kuhusiana na suala hilo kwani suala hilo linahusu pande mbili na wananchi wa Zanzibar wana haki ya kujua mwenendo wa mambo katika nchi yao.
Awali Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alitoa taarifa mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba Jamhuri ya Muungano wa(( Tanzania))YANI TANGANYIKA MKOLONI MWEUSI  imewasilisha ombi katika umoja wa mataifa kuomba kuongezewa masafa zaidi ya maili mia mbili katika bahari kuu.
Jussa alitoa hoja ndani ya baraza la wawakilishi akiwataka wajumbe wa baraza hilo lijadili suala hilo kwa uwazi hasa kwa kuzingatia suala hilo lina athari kubwa kwa wazanzibari iwapo litafanikiwa.
Alisema hatua hiyo ya Serikali ya Muungano ni nzito na inayogusa wananchi kwa hiyo, ilitakiwa kuangaliwa vizuri kwani waathirika wakuu zaidi ni wazanzibari.
Jussa alifahamisha kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotoka ndani ya vyombo vya habari ombi hilo linawasilishwa jana katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.
“Waheshimiwa wawakilishi hoja hiyo imetugusa sana wananchi wanzanzibari tunaomba muichangamkie, hatutaki mambo ya hewala bwana, hoja ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa(( Tanzania)) TANGANYIKA kusema kuwa Zanzibar imeshirikishwa kwa vile mjumbe mmoja kutoka Zanzibar anaonekana katika picha ya pamoja na mama tibaijuka katika kuwasilisha ombi hilo la umoja wa mataifa hatuitaki wala haitoshelezi” alisema Jussa katika kikao hicho cha baraza la wawakilishi kinachoendelea huko Mbweni Zanzibar.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rasi, Ali Mzee Ali, alisema kuwa ingekuwa jambo la maana suala kama hilo likapigiwa kura kutokana na umuhimu wake kitaifa na sio kuamuliwa na upande mmoja.
Suala la masafa ya bahari kuu limekuwa na mgogoro kati ya Zanzibar pamoja na serikali ya jamhuri ya muungano wa ((Tanzania))TANGANYIKA kiasi ya baraza la wawakilishi kupitisha azimio kuhusu jambo hilo, ambalo limeingizwa katika orodha ya kero za muungano.
Akitoa ufafanuzi zaidi, Shamuhuna                                                                                                      alisema kwamba wizara yake inayo taarifa kamili ya suala hilo ambapo alitakiwa yeye kufunga safari kwenda umoja wa mataifa kuwasilisha ombi hilo pamoja na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi wa jamhuri ya muungano Bi Anna Tibaijuka.
Hata hivyo Shamuhuna alisema kwamba kutokana na kutingwa na kazi nyingi alimtuma afisa wake kufuatana na ujumbe huo kwenda katika safari hiyo.“Ujumbe huo kwa sasa upo katika umoja wa mataifa na tayari unatarajiwa kuwasilisha ombi hilo ambapo TANGANYIKA baadaye itapangiwa tarehe kwenda kusikiliza shauri lao”.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar baadhi yao wamehoji hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya ((Tanzania))TANGANYIKA kupeleka maombi Umoja wa Mataifa (UN) kuomba kuongezewa ukubwa wa eneo la bahari na kutaka ufafanuzi wa suala hilo kuwasilishwa ndnai ya kikao hicho, hatua ambayo kimsingi Spika Kificho alikubaliana nao wajumbe hao na kuiagiza serikali kuwaislisha suala hilo barazani hapo.
TANGANYIKA inawasilisha ombi la kuongezwa zaidi masafa ya eneo la bahari kuu kutoka mia mbili na sasa kufikiya mia nne, kama shauri hilo litakubaliwa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, anaelezwa kuwasilisha hoja hiyo na kuiwasilisha Umoja wa Mataifa (UN) huko New York Marekani.

WAZANZIBAR TUNAPIKANA WENYEWE KWA WENYEWE