Tuesday, January 24, 2012

VATICAN YAVAMIA NCHI YA ZANZIBAR KWA KISHINDO KIKUBWA KABISA

KAZI kubwa inayofanywa        
na taasisi za Kikristo
kutoka Tanzania Bara na
nje ya nchi, sasa inaanza
kuzaa matunda.
Digital StillCamera
KUMBUKENI ZAMANI ZANZIBAR WATU WAKIJA KUSOMA DINI NA ILIKUWA
IKITWA MAKKA YA EAST AFRICA SASA IMEKUWA VATICAN YA EAST AFRICA
SHEIN NA SEIF MUTAMUELEZA NI M/MUNGU SIKU YA KIYAMAA..?NA VIONGOZI
WOTE WA ZANZIBAR PIA MUTAMUELEZA NINI M/MUNGU SIKU YA KIYAMA....?

M a k a n i s a y a k i z i d i
kuchipua kama uyoga,
nazo skuli za awali, msingi
na sekondari za Kikristo
zinazotoa elimu bora,
zinaibuka kila mwaka na
kuwa kimbilio la wazazi
wengi wa Kizanzibari.
Katika eneo la Tomondo
n a M o m b a s a k u n a
makanisa zaidi ya kumi na
skuli za Kikristo pamoja
na maduka ya dawa, hali
ambayo inafanya mji huo
mdogo kuonekana kama
‘Vatican’ ya Zanzibar.
Hali kama hiyo ya ‘Vatican
Tomondo’, inaenea pia
kuelekea Kiyanga, Bambi
na shamba nyengine.
H a l i y a ‘ V a t i c a n
Tomondo’ inaonekana pia
Machui na Kiboje.
“Machui wamejiimarisha
na wanazidi kila uchao.
Huko Kiboje unaweza
kwenda msituni ghafla
ukatokezea kijiji kikubwa
a m b a c h o h a k i k u e p o
kabisa awali, ukawakuta
(Wakristo) wamejaa.”
Anasema mchangiaji
mmoja akitoa maoni yake
juu ya kasi ya kusambaa
U k r i s t o n a Wa k r i s t o
Zanzibar.
“Huo ni mmoja katika
m i k a k a t i y a o k u w a
waongozeke Zanzibar bila
sisi kushtuka, ili siku moja
ghafla waje watwambie
kuwa “hamuwezi kuweka


sheria za Kiislamu kwa
sababu tupo 50-50 (sawa
kwa sawa).” Anasema
mchangiaji huyo.
Uchunguzi uliofanywa
na mwandishi umebaini
kuwa, wakati taasisi za
Kikristo zikizidi kufanya
j u h u d i k i m ya k i m ya ,
baadhi ya Masheikh na
wanaharakati wa Kiislamu
wamekuwa wakilalamika
na kushutumu taasisi
za Kikristo hasa kutoka
Bara kwamba zimekuwa
zikiwahadaa wananchi wa
Zanzibar na kupora ardhi
zao.
Madai yanayotolewa ni
kuwa ‘Wabara’ hao Wakristo
wanawatumilia baadhi
ya Wazanzibari kupata
viwanja wakidanganya
kama wanataka kufanya
shughuli za kijamii, lakini
baada ya muda mchache tu,
“unashtukizia washajenga
k a n i s a n a wa n a we k a
msalaba na kengele”.
L a w a m a k u b w a
wamekuwa wakitupiwa
w a n a n c h i a m b a o
w a m e k u w a w a k i u z a
maeneo yao, lakini nao
wamekuwa wakijitetea
k u w a n i u m a s i k i n i
unaowasukuma kuuza kile
ambacho ndio wanaona
kitawasaidia.
Wamesema, tatizo hili
hawezi kulaumiwa mtu
binafsi mmoja mmoja,
bali ingetakiwa jamii ya
Waislamu, labda kupitia
taasisi zao kuliangalia kwa
mapana yake.
“ Wa i s l a m u h a t u n a
mfumo wa zaka na sadaka
wa kusaidia masikini

wala mpango mkakati wa
kuangalia mustakbali wa
Uislamu Zanzibar, sasa
utamlaumi vipi mtu binafsi
anayeuza eneo lake ili apate
kujikimu kwa chakula na
ada ya watoto ya shule?”
Alihoji Mzee mmoja
katika moja ya maeneo
ya shamba ambapo taasisi
za Kikristo zimekimbilia
kununua ardhi.
B a a d h i y a w a t u
wamelinganisha suala
hili la ardhi ya wazalendo
kuuzwa kwa wawekezaji
wa nje (Wakristo) na
mashirika ya kidini ya
Kikristo sawa na ile hali
iliyotokea kwa Wapalestina
ambapo ardhi kubwa
iliuzwa kwa Mayahudi.
Wa n a o t o a h o j a h i i
wanasema kuwa hata
ukiangalia suala la ulevi,
zipo sheria lakini hazifuatwi
kinyume chake baa na
vilabu vya ulevi huwekwa
kila mahali kwa leseni za
serikali jambo linalotia
s h a k a k wa m b a l a b d a
huenda kuna mkakati wa
kusambaza ulevi kuharibu
jamii.
Baadhi ya Wazanzibari
waliolijadili suala hili hasa
kupitia katika mtandao
wanasema kuwa itakuwa ni
fikra potofu kudhani kuwa
Zanzibar ni ya Waislamu
na Wakristo hawana haki.
“Naona kama ni kheri
tukaacha kutiana chuki
hususan kupitia dini na
kujaribu kuleta mitafaruku
ya kidini. Nadhani Zanzibar
wapo Wakristo, mabaniani
na wengine wengi. Hawa

ni minorities (wachache),
l a k i n i t u k u b a l i a n e
kama wapo!” Amesema
mchangiaji mmoja.
“ N a d h a n i w e n g i
watakuwa wamesoma
japo na Mkristo mmoja
skuli, binafsi nimesoma
na Mkristo nilipofika
sekondari. Huyu alikuwa
akitokea Mkwajuni, huko
Wakristo wapo na hilo
hatuwezi kuliepuka.”
Aliongeza.
“ S i o To m o n d o t u ,
‘Vatican City’ kubwa
ipo Machui huko hadi
n g u r u w e w a p o n a
daladala za Waislamu
ndio zinasafirisha pombe.”
A n a s e m a m c h a n g i a j i
mwingine.
Hata hivyo, wengine
wanasema kuwa kama
ilivyo Marekani, Italy,
Ufaransa na Uingereza
ambapo Waislamu wapo,
lakini katika hali halisi ni
nchi za Kikristo.
“Ni kweli Wakristo
walikuwepo tokea zamani,
lakini sio kutuharibia
ardhi yetu kwa kuzijengea
makanisa na majumba
ya madanguro.” Alisema
m c h a n g i a j i h u y o n a
kuongeza akisema kuwa:
“Hizi chuki lazima
zitakuja, kwa vile kwa
nini wananchi wazaliwa
hawapati viwanja na
badala yake wapewe
hawa ili wajenge makanisa
ambayo mengi hayana
hata hao wanaokwenda
kufanya hizo wanazoita
ibada zao,
bali hii ni mipango
maalumu iliopangwa
kuja kukichafuwa kisiwa
chetu. Mbona hizo nchi
za nje hawakubali misikiti
ijengwe kiholela tu?,
Tusijitie
h u r u m a k wa n i l e o
hii Muislamu mbali ya
kujenga misikiti,bali kuvaa
hizo hijabu za kichwa tu
basi imekuwa kero, sasa je,
sisi wanaojenga makanisa
k i h o l e l a ? A l i s e m a
mchangiaji huyo katika
mtandao.
“Ni lazima tupinge
haya kwa nguvu zote,
na tunajuwa kwamba
Wakristo kweli tumekaa
nao tokea zamani lakini
sio kutujengea makanisa
kiholela kwani nina imani
Wakristo wote hapo labda
ni asilimia 4, sasa hata
yakijengwa yakiwepo
m a k a n i s a m a t a t u t u
yashawatosha.”
U c h u n g u z i w a
mwandishi umebaini
kuwa suala hili la ujenzi
wa makanisa na shule
z a K i k r i s t o , l i m e z u a
mjadala mkali katika
mitandao ambapo wengi
wamekuwa wakipinga
huku wengine wakisema
kuwa wa kulaumiwa ni
Wazanzibari wenyewe kwa
maana kuwa kama wao
wamelala wasidhani kuwa
na wengine wamelala au
wamekaa tu kupiga porojo,
wanafanya kazi.
W a n a s e m a j a p o
inaweza kudaiwa kuwa
kwamba hii ni njama
ya mfumokristo, lakini
Waislamu Wazanzibari nao
wameweka mikakati gani
na kuitekeleza kukabiliana
na njama (conspircy) hizo?
Wanahoji.
Wanaotoa hoja hiyo
w a n a t a h a d h a r i s h a
wakisema kuwa watoto
wanaosoma katika skuli
za Kikristo hivi leo ambazo
zinatoa elimu bora kuliko
ilivyo Benbela na nyingine
za serikali, baada ya miaka
m i c h a c h e i j a yo n d i o
watakaokuwa watawala
wa Zanzibar.
“Lawama kubwa ni sisi
wenyewe Wazanzibari,
sisi wenyewe wananchi,
wananchi ndio serikali
sasa nani wa kulaumiwa
? Skuli haziboreshwi,
zimekuwa mahala pa
watoto kujifunzia mipasho
na uhuni wa kila sampuli,
taasisi za Kiislamu na
watu binafsi hawajengi
n a k u e n d e s h a s h u l e
bora, wakijenga wengine
tusilalamike.” Imeandikwa
katika maoni ya mchangiaji
mmoja katika mtandao.
“ N i w a j i b u w e t u
kuilinda nchi yetu, dini
yetu na Utamaduni wetu,
hakuna mwengine wa
kuyafanya hayo isipokua
sisi Waislamu Wazanzibari.
Muhimu Wazanzibari
tuelewe kuwa kizazi chetu
kitakuja kutulaumu kwa

kuiachia nchi ikichukuliwa
na kutoihami dini ya
Kiislamu wakati uwezo
wa kufanya hivyo tunao.”
Ameongeza.
W a l i o c h a n g i a
wa k i wa n a m t i z a m o
huu wanasema kuwa
kulalamika haisaidii kitu
na la muhimu kufahamika
ni kuwa kila jamii ina
haki ya kujiimarisha ili
kuhakikisha uwepo wake
kwa vizazi vijavyo.
K w a m b a k a m a
Waislamu wa Zanzibar
hawafanyi harakati za
kuwaendea Wakristo wa
Bara na kuwaita katika
Uislamu, Wakristo wa
Bukoba na Tukuyu wao
wakija Tomondo na Chake,
huwezi kuwalaumu.
Z i p o t a a s i s i k a m a
JUMIKI, JUMAZA na
UAMSHO, je, hizi zina
mpango wa kuwaendea
Wakristo wa Kyela, Kibosho
au Sumbawanga?
S a s a k a m a h a z i n a
m p a n g o h u o , w a
kulaumiwa sio Kadinali
Pengo anayetuma vijana
wake kuweka misingi
ya kuimarisha Ukristo
na kudhoofisha Uislamu
Zanzibar.
Kwa upande mwingine
imeelezwa kuwa nguvu
kazi na rasilimali kubwa
ya Waislamu imekuwa
ikitumika katika siasa
zisizo na munufaa kwa
jamii badala ya kuzielekeza
katika mambo yenye tija.
“ K a m a u l e u m a t i
unaokusanyika katika
mikutano ya CCM na
CUF ungeelekezwa katika
jambo moja tu dogo na
jepesi la usafi wa mji,
leo Zanzibar isingekuwa
chafu kiasi hiki, lakini
tembea mjini uone na
labda ulinganishe na miji
mingine yaTANGANYIKA(( Tanzania)).”
A m e s e m a  S h e i k h
mmoja ambaye hata hivyo
hakutaka kutajwa jina lake
gazetini.
Sheikh huyo ambaye
anawalaumu wanasiasa
kwa kushindwa kutumia
nguvu kazi ya mashabiki
wao kufanya mambo
y e n y e m a n u f a a k wa
nchi, amewalaumu pia
viongozi wa Kiislamu kwa
kushindwa kuwatumia
waumini wao kuendeleza
Uislamu badala yake nao
wamebaki wakilaumu
makanisa.

No comments:

Post a Comment