MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Wednesday, January 11, 2012
MFAA MAJI HAWACHE KUTAPATAPA NDIO YA HAMAD RASHID SASA
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, ambaye wiki iliyopita alitangazwa kufukuzwa uanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) na wenzake watatu, amesema kufikia jana alikuwa hajapata barua rasmi kutoka CUF ya kumuarifu kuhusu hatua hiyo dhidi yake.
Hamad, ambaye na wenzake hao; Doyo Hassan, Shoka Khamis Juma, Juma Said Saanan, alisema taarifa za kufukuzwa kwao uanachama, wamekuwa wakizisikia tu kwenye vyombo vya habari, kinyume cha kawaida.
Hata hivyo, alisema tayari amekwisha kumwandikia barua Katibu wa Bunge kumjulisha kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salam, uliozuia kufanyika kwa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa, kilichowafukuza uanachama wa chama hicho.
Amri hiyo ya iliyotolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Augustine Shangwa, ilitaka kikao hicho kisifanyike hadi hapo kesi ya msingi namba 1/2012 iliyofunguliwa na Hamad na wenzake 10 itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Hamad alisema katika barua aliyomwandikia Katibu wa Bunge aliambatanisha pia na nakala ya uamuzi huo wa mahakama.
Alisema nakala ya barua hiyo pamoja na ile ya uamuzi wa mahakama, vimepelekwa pia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kuwajulisha kuhusu uamuzi huo wa mahakama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment