Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,tuna muita mshirika wetu wa muungano alitukatalia na kutupa munda tutoke haraka na ndio alipotupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salimin Amour wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingilia. Kwani, zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.
MISUMARI YA MWISHO INAPIGWA SASA NA TANGANYIKA ((TANZANIA)) KATIKA JENEZA LA ZANZIBAR. JE.WAZANZIBAR MPOOOO AU MUMELALA BADOO.. ?
Ombi la Januari 18,2012 la Tanganyika (Tanzania ) huko Umoja wa Mataifa,New York, kutanuliwa mipaka yake ya baharini ni misumari ya mwisho inayopigwa kufuatia ule wa kwanza katika JENEZA la Zanzibar hapo April 26,1964. Mara tu baada ya kuapishwa rasmi Mwalimu Nyerere kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano ya Watu wa Tanganyika na Zanzibar,kanuni yake ya kwanza aliotunga (decree), ilikua kuifuta Tanganyika kwa njia za kiinimacho na kuibua Tanzania ambayo ni ile ile Tanganyika aliyoifuta lakini imeibuka na mipaka mipya ya aridhini.Ilijumuisha visiwa vya unguja na Pemba. Sasa inajiandaa kupiga misumari ya mwisho kwa kutanua zaidi mipaka yake ya baharini na kiliomo ndani yake tangu dagaa hadi papa.mashamba mpaka mjini watu mpaka miti hii ni dalili ya azimio la arusha inaletwa tena kwa njia nyengine bila ya wazanzibar kufahamu nini kinaendeleya ila wakipata ruhusa tu tujuwe tumekwisha tutahamishwo zanzibar tukitaka tusitake ili waigeuze watakavyo kufanya ulanisi na kila balaa.
Tangu 1964, misumari mingi imekuwa ikigongomelewa jeneza letu tena hatua kwa hatua; na sisi wazanzibari twatazama macho tu.
Kufuatia Muungano uliofanyika bila umma kuulizwa ndewe wala sikio, akiba kubwa ya fedha za Zanzibar katika Bodi ya ile iliokua Jumuiya ya AFRIKA MASHARIKI ziliporwa na tunaemwita Mshirika wetu wa Muungano na kuzitia kibindoni katika Bank yake (BOT) bila ya ridhaa umma au ya serikali yatu. Shabaha ilikua ni kuiua Zanzibar kiuchumi ili kuidhibiti. Sehemu ya Zanzibar katika “Currency Board ” ya Jumuiya ile ilikua 11.2%. Huo ukawa msumari mwengine kati ya mingi katika jeneza letu. Licha ya juhudi nyingi za Viongozi wetu , walishindwa kuzuwia hilo. Kwani wenzetu hizo wanazoziita “KERO” ndio “MISUMARI” wanayoigongomelea JENEZA LETU hadi watapotuzika kabisa.
Msumari mwengine mjarabu kabisa ni kule kuunganishwa kwa Afro-shirazi party (ASP) na TANU, 1977 kinyume na Marehemu mzee Karume alivyowausia wandani wake wasifanye,kwani yeye binafsi hakuridhia hilo katika utawala wake mzima wa miaka 8 .Kwa msumari huo,hatima ya kisiasa ya Zanzibar ilianza kuamuliwa Dodoma badala ya kisiwandui. Rais wetu Aboud Jumbe alipofanya nyoko huko Dodoma, 1984 , alikiona kilichomtoa kanga manyoya. Kuanzia hapo hata viongozi wetu wa Zanzibar bila ya ridhaa ya Dodoma,ni mwiko kukalia kiti cha Urais. Wenzetu wanatuchagulia hata marais wetu-aibu gani hii ?
Msumari mwengine katika jeneza la Zanzibar ni kuondolewa kwa wadhifa wa ” Makamo-rais ” na kumfanya Rais wetu kana kwamba ni rais wa kilabu cha mpira cha ” MIEMBENI SPORTS CLUB”. Hana nchi hata akiwa na bendera....SASA AMEKUWA BOYAA TU SHEIN SIO RAISI.
Na pale Zanzibar ilipojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili inufaike kiuchumi,ana jiitaa mshirika wetu wa muungano alitutia munda na kuupiga msumari mwengine katika JENEZA la kuizika Zanzibar katika Jukwaa la Kimataifa. Marais Mwinyi na Salimin Amour wakavuliwa nguo hadharani na wakakemwe na Mwalimu Nyerere watoke kwa mlango wa nyuma kama walivyoingia. Kwani, Zanzibar haitakiwi kuwa na sauti katika jukwaa lolote la kimataifa na hata kucheza dimba katika FIFA-Shiriklisho la kabumbu Ulimwenguni.
KABLA SHEREHE ZA MIAKA 50 ZA MUUNGANO 2014, MAITI ya (ZANZIBAR) iwe tayari kuzikwa kupitia KATIBA MPYA YA SEREKALI YA TANGANYIKA. Zanzibar inazikwa kule kule UMOJA WA MATAIFA,NEW YORK, na sio Mwanakwerekwe ambako kaburi lake lilichimbwa tayari 1964 pale kiti chake kama dola huru huko kilipotoweka kwa kiini macho. TANGANYIKA((Tanzania)) inajua kucheza turufu zake huko ili kuizika Zanzibar katika kaburi lile lile iliochimba 1964 kufuatia Muungano FEKI.
Baada ya kupora fedha zetu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki iliovunjika ,sasa tunae muita mshirika wetu wa Muungano amejianda kupora gesi na mafuta yetu kwa njia ya kuitanua mipaka ya bahari kama alivyotanua mipaka ya aridhi katika ile Tanganyika kubwa kwa jina la ((Tanzania.)) Wakati maliasili zao kama gesi,Tanzanite, dhahabu, almasi ,makaa ya mawe na nyenginezo, ni mali zao pekee yao, mafuta na gesi ya Zanzibar na Pemba eti ni ubia.
VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR NA SISI UMMA WA ZANZIBAR, TUTATUMBUA MACHO MPAKA LINI ? AU
MPAKA TUZIKWE KABISA HUKU SANDA TUMESHASHONEWA NA TUNAIONA ?
Kuna usemi “Kila Umma hupata viongozi uliostahiki kuuongoza.Ukiwa Umma ni ngangari, utapata viongozi ngngari kama akina Jussa,Hamza na Mansuri -wenye kupaza sauti kuutetea Umma.La ,ukiwa Umma ni wazembe, watapata viongozi wazembe.
Wazanzibari mpo ?
Tusigeuke ile hadithi ya Mnyamwezi ” Ninamtajama tu” kumbe mwenzake anamharibu.Eti anatafuta ushahidi.
USHAHIDI kuwa tuna muita mshirika mwenzetu wa Muungano hakuwa na nia njema tangu awali, ilidhihirika pale alipopiga msumari wa kwanza,April 26,1964 kwa kuifuta Tanganyika .
Ilikua tangu wakati ule Viongozi wetu wawaambie ndugu zetu kuwa, BILA YA TANGANYIKA, HAKUNA MUUNGANO.Mumeivunja wenyewe. TUNAWEZA HATA KUWAAMBIA HIVYO LEO LAIT”I TUNA VIONGOZI NGANGARI- KERO ZIMETOKA WAPI IKIWA HAKUNA MUUNGANO.JAMANI “SI ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO ?”
Ningelikua mimi ni Rais wa Zanzibar,ningekwenda Studio za Raha leo na kulihutubia Taifa nikiwaamrisha wabunge wote wa Zanzibar katika Bunge la Muungano huko Dodoma, warudi Zanzibar mpaka kwanza waziri-mkuu Pinda,kwanza awataka radhi Wazanzibari na Rais wao pili hao wanao jiitaa washirika wetu katika huo Muungano FEKI,waifufua Tanganyika walioifuta kwa kini-macho.
Je, Wazanzibar mpo au tunasubiri kuzikwa kabisa 2014?..lakini UBAYAA HATUNA RAISI HAPA ZANZIBAR TUNA BOYAA TU LAELEYA KATIKA MAJI YA ZIWA TANGANYIKA.
ILI KUZUWIA KUPIGWA MSUMARI WA MWISHO KATIKA JENEZA LETU ,TUDAI TUJADILI KWANZA UHALALI WA MUUNGANO NA KUIULIZA NCHI TULIYO UNGANA NAYO TANGANYIKA IKO WAPI IRUDI NA KAMA HAWATAKI BASI NDIO TUNAVUNJA KABISA MUUNGANO MAANA KWANZA HAKUNA MUUNGANO KUNA UBABE TU TUSIKUBALI KUJADILI KATIBA MPYA MAANA HAKUNA NCHI TULIYO UNGANA NAYO SASA TUNAJADILIYANA NA MTU ASAYE KUWEPO......? PIA TUKUMBUKENI KUWA. ULIANZA UFIZI NDIPO YAKAOTA MENO !
No comments:
Post a Comment