Saturday, December 15, 2012

WAZENJI TUNAKULA UROJO SMZ WAMELEWA MADARAKA NCHI YA ZANZIBAR INASEMA BYE BYE



Wanaotaka tuendelee na Muungano huu,wasubiri Kubatizwa na Kusulubiwe na kanisa Katoliki.
Kwa upande wa Tanganyika waislamu hawana nguvu zaidi ya Kanisa na wamefunikwa na kuzibitiwa na kusalitiwa na Baraza la Wanafiki wa Kislamu BAKWATA.
ndio maana ukawaona Wakristo wametowa takumu fake ya kusema wao ndio wengi kwa hio nilazima serekali na sensa ijuwe hivyo ili kupangiwa bajeti maalumu.
Kwa Upande wa Zanzibar tunakwenda huko huko kuzidiwa nguvu na ishara nyingi zipo za viongozi wetu wa smz kupiga magoti kwa kanisa na kuwazibiti waislamu kila ucheo alimuradi yeye ni raisi,makamo wa raisi,mbuge,waziri,amiri jeshi mkuu,kamishna n.k. basi wako tayari hata kuuwa ndugu zao wa zanzibar kwa vyeo tu.
Wasemao kuwa kanisa halina nguvu zanzibar wanajidanganya tena sana, angalia sala za Jumapili watu huanza safari tokea Jumamosi kuja kutia wingi Zanzibar ,Mbaali na mmiminiko uloko zanzibar bila kujulikana ni wangapi.
Hizi zote ni agenda kabambe za zamani kwa mategemeo ya baadae chini ya wanafiki wetu Smz na hivi sasa kuna kampeni za chini kwa chini , kwanza kila katika watoto 30 wazaliwao Zanzibar katika hospitali ya mwembe ladu Basi Wazanzibar ni watoto 6 tu walio baki utajaza wewe.
Jengine ni Kanisa kusaidia miradi midogo midogo kwa watu wenye asili ya Tanganyika hata kama sio Mumini wao kidini, hii ni kuangalia kuwa focus yao ni kuwa Watanganyika wa zanzibar wote chama ni CCM na lengo ni kulinda Muungano na kufanya Shughuli zao bila kero kwa mgongo wa chama kuwalinda.
Hivi sasa wengi wao wameshafanikiwa kuwa na Zanzibar ID na kukabidhiwa haki zote na fursa zote ambazo hata Mzanzibari mwenyewe hana na hata ukiangalia watendaji wakuu wa Serekali ulimwenguni sio Rais na mawaziri , niwakurugenzi na wahasibu.
Sasa angalia wahasibu je ni Wazanzibar...? jibu ni....?Wakurugenzi je ni Wazanzibari jibu ni...? na Majaji je ni Wazanzibari jibu pia tena litakuwa ni....? je bado tu mzanzibari hujaa amka kuwa hatuna tena zanzibar imebaki jina tu. hebu wangaliye wote hao niliyo wataja hapo juu hapa nchini Zanzibar utajuwa ni watu wenye asili gani..?




WAKOMBOZI WETU WANATESWA JELA WAZANZIBARI TUKO KIMYA KWELI TUNAITAKA NCHI YETU....???



Hadi sasa jeshi la polisi LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA na serikali  feki ya Zanzibar zinataka iaminike kwamba viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wanaowashikilia kwa zaidi ya mwezi sasa, ni washukiwa wa uhalifu. Uhalifu upi..? Fujo, vurugu, kuharibu mali na matusi, angalau kwa kutaja machache. Wanataka sana hilo ndilo limezeshwe kwenye akili zetu sisi wazanzibari. Kila mtu aimbe wimbo huo na mwisho wa siku, sote tuingie kwenye kapu moja la uzembe na uvivu wa kufikiri na ujinga usio kuwa na mwisho.
Lakini shukurani kwa mifumo ya sasa ya kimawasiliano, serikali na vyombo vyake wametukuta wengi wetu tukiwa hatudanganyiki tena na ulaghai wake. Hata kama tunaweza tusiwe na nguvu za kimabavu ilizonazo serikali feki ya zanzibar, maana sisi hatuna polisi, jela wala mahakama, lakini tuna nguvu ya dhamira zetu. Nayo ni nguvu kubwa, kwa hakika.
Kwa nguvu hiyo, ya kuwa na akili huru, ndipo tunakataa kuumeza uongo wa serikali feki wa “kuwahalifisha” viongozi wa Uamsho na wafuasi wao ambao sote ni waznzibari tunao taka nchi yetu. Tunajua – kama inavyojua hiyo serikali feki na vyombo vyake – kwamba viongozi wa Uamsho wanaadhibiwa kwa sababu ya msimamo wao wa kisiasa. Msimamo wa kuitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili, nje ya Muungano wakulazimishana na muungano wakuomeza zanzibar na muungano wa WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA.
Ikiwa kuna kosa lolote ambalo leo hii limemfanywa na Sheikh Msellem Ally ajikute akishindwa kumuuguza na hatimaye kumzika mwanawe mzazi, ni hilo la kwamba ni kiongozi aliyewaongoza Wazanzibari kuidai haki yao ya kuwa huru, heshima yao ya kujiamulia na dhamira yao ya kusonga mbele kama taifa HURU LA ZANZIBAR kama yalivyo mataifa mengine ulimwenguni.
Kwa kufanyiwa wanayofanyiwa viongozi wa Uamsho, serikali feki na vyombo vyake wanajidanganya kwamba wanalizima vuguvugu lililokwishapamba moto la Wazanzibari kudai mamlaka kamili ya nchi yao.
Na hili la upande wa serikali feki na mawakala wake linaweza kuelezeka ingawa halikubaliki. Lakini ambalo haliwezi kuelezeka, kukubalika, wala kuvumilika ni hili la kimya chetu sisi wengine, ambao tunaguswa na dhamira wanayoisimamia akina Sheikh Msellem.
Kwa sababu ya kutotaka kuitwa Uamsho, mimi na wenzangu wengi, tumeshindwa hata kuandika mistari miwili mitatu ya kusimama na viongozi hawa. Tunawaachia waadhibiwe, wateswe, wadhalilishwe kimwili na kisaikolojia. Kama nilivyosema hapo kabla, inawezkena hatuna nguvu za kuwanusuru na mkono dhalimu wenye nguvu wa dola, lakini tunao uwezo wa kuwahuisha mbele ya makini za watu: kuwasafishia majina na kuzitukuza thamani zao, kwa kutokubali “kuununua” uzushi dhidi yao.
Hawa si magaidi, si mahaini, si majambazi,kama ilivyo serekali hii toka itokako imeuwa watu tele imefunga watu tele jela imeharibu wanawake na wasichana tele na mpaka sasa inaendelea na mfumo huo huo wa kuwafunga kila anae dai zanzibar na kuwathalilisha watu. na hao wanoitwa uamsho kwa hakika hata si wahalifu. Hawapo walipo sasa kwa sababu wameiba, wameua au wamemdhulumu mtu. Wapo walipo kwa kuwa wanapigania nchi yao – heshima ya taifa lao. Hawa ni wa kutukuzwa si wa kupewa mgongo! Si wa kupigwa pande!

DR KUMBI SHEIN AKIPOKEA NA KUKARIBISHA IBADA YA KUABUDU MOTO BADALA YA KUABUDU M/MUNGU.


DR KUMBI SHEIN NA IBADA YAKE YA KUABUDU MOTO

WAZANZIBARI KAMA HAMUJA ITIMUWA CCM MUTAENDELEA KUWA MASIKINI NA HAWA WANAENDELEA KUTAJIRIKA NA KULALA USINGIZI MNONO MAANA YAO YANAWAENDEA SISI TUNALALA NA NJAA NA HOSPITALI HAKUNA MADAWA NA IBADA ZA MOTO BADO TUNALETEWA BADALA YA KUABUDU M/MUNG TUNABUDU MOTO.

LAZIMA TUINGOWE CCM NDIO TUTAENDELE ZANZIBAR LAA SIVYO TUTAKUFA NA ZANZIBAR NDIO KWANZA INABURUZWA NA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA

Friday, December 14, 2012

DR KUMBE KISHEIN NA SEREKALI FEKI YA SMZ YAMKATALIA SHEIKH MSELLEM KWANDA MAZIKO YA MTOTO WAKE ALIYEFARIKI .


SERIKALI YA SMZ INAYO ENDESHWA NA KANISA..........YAFANYA KITENDO CHA KINYAMA KUMZUIA SH. MSELLEM KWENDA MAZIKO YA MTOTO WAKE.
MAAMIR WAAMUA KUMSALIA HUKO HUKO GEREZANI..

Serikali ya SMZ wakishirikiana na jeshi la polisi la MKOLONI 

MWEUSI TANGANYIKA  hapa nchini Zanzibar 

wamemzuia Amir Sheikh Msellem Ali kuweza kuhudhuria 

katika mazishi ya mwanawe ambae alifariki jana katika 

hospital ya Mnazimoja na kuzikwa leo asubuhi huko Donge.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozip
ata hivi sasa sababu ya 





kumzuia kwenda kwenye mazishi ya mtoto wake hasa 





hawakutaja ila wanaendeleza ule ubabe na kuwadhalilisha 





masheikh na kuwanyima fursa zote wanazo stahiki.


Tunaona tena jinsi serikali inavovunja katiba na kuvunja haki 





za binadamu kwani niwajibu kwa mfungwa yoyote kuhuzuria 





mazishi ya ndugu wa karibu na ukizingatia sheikh msellem 





sio mfungwa NA PIA ALIYE FARIKI NI MWANAWE pia 





ukumbuke kuwa  ni 
mtuhumiwa tu wa kesi ya kupanga ya 




jeshi la polisi na ya mtumwa dr kumbi kisheni ikishirikiana 





serekali ya MAKABURU 
WEUSI TANGANYIKA.



Hii ndio Serikali yetu feki tuliyodanganywa nayo toka 1964 

kuwa ati ni serekali ya wananchi na inayosema inafata 

democracy.




Bado wanawanyima haki zao Maamir wetu.


Inshallah mungu atawapa la kuwapa biidhni llah.

Wednesday, December 12, 2012

WHERE IS U.N.....? WHERE IS HUMAN RIGHT...?





HAKUNA KUKUSANYA MAONI YA KATIBA SASA NI KUCHOMANA VISU TU NCHINI ZANZIBAR


MIKUTANO ya kukusanya maoni ya upatikanaji wa Katiba Mpya ya MKOLONI MWEUSI Tanganyika na babaisha bwege katika Visiwani  vya Zanzibar, imeingia dosari baada kuzuka ghasia na baadhi ya watu kujeruhiwa kwa kuchomwa visu.

Vurugu hizo ambazo chanzo chake ni siasa, zilitokana na wafuasi wa baadhi ya vyama vya siasa, kuvamia mikutano iliyokuwa ikifanyika Unguja na kusababisha hofu za kiusalama.

Baadhi ya maeneo ambayo vikundi vya janjawee,mbwaa mkali na vyenginevyo ambavyo vyote vimesadikiwa kuwa ni vikundi vya CCM walivamia mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusababisha ivunjike ni Shehia za Magomeni na Mpendae Mkoa wa Mjini Magharibi.Hii ni mara ya kwanza ghasia kuzuka katika mikutano ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya YA MKOLONI MWEUSI Tanganyika Nchini Zanzibar

Tukio la kuchomana visu, lilitokea katika Shehia ya Mpendae baada ya vurugu zilizosababishwa na vijana wa Mbwaa Mkali na vijana wa Ubaya Ubaya kuvamia mkutano uliokuwa ufanyike jana mchana.Vijana hao walianzisha ghasia hizo baada ya kutaka kuvunja utaratibu uliokuwa umewekwa. Walitaka wakae mbele ya wengine waliokuwa wametangulia katika mkutano huo wao walikuja na malori manne na wakataka wakae mbele kuliko mtu mwengine yoyote walivyokataliwa ndio visu vikaanza na baadhi ya watu kujeruhiwa.

Hatua hiyo ilipingwa na kuibua ghasia ziliozababisha watu kadhaa kujeruhiwa kwa visu.

Tukio jingine lililovuruga mkutano huo ni lile lililotokea katika Shehia ya Magomeni, Jumatatu wiki hii baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya makundi mawili yenye misimamo tofauti juu ya mfumo wa Muungano; kuna wanaopinga na wanaoukubali.


Misimamo hiyo imeelezwa kujikita katika misingi na sera za vyama vyao vya kisiasa.

Katika misimamo hiyo, CUF kinaamini katika Serikali ya Zanzibar na Tanganyika kila moja kuwa na mamlaka kamili na Muungano uwe wa mkataba wakati, CCM kinasimamia kwenye Serikali mbili kueleke moja; Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Shehia ya Magomeni
Saa mbili kabla mkutano kuanza, watu wengi walifika Uwanja wa Mzalendo ambako mkutano ulitakiwa kufanyika. Walijipanga kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Tume ambao ni aliyewahi kufika ndiye anayetangulia kutoa maoni.

Hali hiyo ilisababisha wakazi wa Shehia hiyo waliokuwa wenyeji wa mkutano, kukosa nafasi ambayo ingewawezesha kutoa maoni kwa mazungumzo ya ana kwa ana kwa sababu wakazi hao walipofika katika kiwanja hicho kulikuwa na vijana tele walioletwa na malori tofauti kuwa tayari washachukuwa nafasi kwa hiyo kuwafanya wakazi hapa magomeni kuto kuwa na nafasi ya kutowa maana maana vijana ndio washafika.

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni, Salmin Awadh Salmin, alisema hawakuwa tayari kuwa wenyeji wa mkutano ambao hawatashiriki akisema waliokuwa wamejipanga wote walifikishwa kituoni hapo kwa magari kwa lengo maalumu la kuwakosesha wenyeji kutoa maoni yao, kwa kuwa inafahamika kuwa wengi wao ni wana CCM.

Hoja hizo alizitoa kwa wajumbe wa Tume ambao pia hawakuridhishwa na hali ya usalama katika eneo hilo kutokana na vurugu zilizokuwa zikifanywa na wafuasi hao wa CCM.

“Kwa hali ilivyo, hatuwezi kupata utulivu utakaowezesha tufanye kazi kwa ufanisi na kumaliza mkutano kwa amani bila fujo. Natangaza rasmi kuwa leo hakuna mkutano,” Mwenyekiti wa Timu ya Tume hiyo inayokusanya maoni visiwani hapa, Profesa Mwesiga Baregu.

Akizungumza baada ya kuvunjika kwa mkutano huo, Salmin alisema waliokuwa wamefika kutoa maoni walikuwa wakitaka kunadi misimamo ya vyama vyao akisema hiyo ni hali ya kihistoria inayowakabili wakazi visiwani humo.

Tuesday, December 11, 2012

ALIYO YASEMA MZEE KARUME 10-DECEMBER-1963 NI HAYA



A A KARUME risala hii ya Uhuru Alisoma kwa niaba ya Afro-Shirazi Party wote. 
Mzee Karume alisema tunachukuwa fursa hii kuwapa mkono wa furaha watu wote wa visiwa hivi kwa jtihada yao na bidii kubwa, pamoja na misaada mikubwa katika juhudi zetu sote za kuupinga ukoloni na utawala wa kibeberu. Jitihada . Leo mwezi 10 Disemba, 1963, ZANZIBAR imekuwa Huru.
Mzee Karume akaendelea kusema Hii leo sisi watu wa visiwa hivi tumepata haki ya kuchukuwa mahala petu kuwa ni Dola sawa na nyengine katika umoja wa Nchi za Dola za Commonwealth.
Kwa uchache, kuwa mwanachama katika umoja huo, kuna maana kwamba nchi hii ni huru chini ya mpango wa serekali ambayo msingi wake umejengwa juu ya kuendelea kwa ridhaa ya wanaotawaliwa. Ili kufikia matarajio yetu hayo tunayo moja katika Katiba zenye msingi madhubuti iliohusika na shuruti za haki za binadamu, haki za mambo ya siasa na uhuru wa dola yoyote nyengine.
Ni wajibu wa watu wote wa dola yetu mpya, kila mmoja katika sisi bila yakujali fikra zetu za siasa au madaraka yetu kusaidia kweli kweli katiba yetu iweze kufanya kazi. Pamoja na manufaa, haki na uhuru ambayo yote hayo yamepatikana baada ya nchi kuwa huru leo hii 10 Disemba 1963.
Vile vile yapo mambo yaliyo wajibu na lazima ambayo imebidi yatimizwe kwa ajili ya dola na kwa ajili yetu wenyewe kila mmoja juu ya mwenziwe. Kwa hakika kwa ajili ya wajibati hizo na mambo yalo lazima, kama ilivyo juu kufurahikia haki za uraia na haki za siasa na uhuru mbali mbali basi vile vile uhuru wetu lazima utimizwe kwa njia hizo.
Tuliyoyapata leo mwezi 10 Disemba ni mipango ya mwanzo tu ya kuweza kufanya juhudi kwa ukamilifu dhidi ya maadui zetu nao ni ujinga, umasikini na maradhi na kuweza kuleta imani penye khofu na shaka na kuleta masikilizano mahala ambapo hata hivi sasa dawa ipo, na kuleta mapenzi mahala ambapo pana chuki, ili dola yetu mpya ichomoze katika neema, umoja na furaha kwa sote wazanzibar.
Kwa hivyo katika hii siku ya leo na tumwombe Mwenye Enzi Mungu, Inshallah atuweke tuifanye na tuitimilize kazi kubwa ya kujenga taifa ili dola yetu mpya ya ZANZIBAR ipate baraka ya matunda mema ya kazi zetu.
Uhuru na Umoja, Uhuru na kazi!”.
Jarida la MAARIFA la Serikali ya Zanzibar. Makala maalumu kwa kufikilia Uhuru. Jumaane, 10 Disemba, 1963.