Hadi sasa jeshi la polisi LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA na serikali feki ya Zanzibar zinataka iaminike kwamba viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wanaowashikilia kwa zaidi ya mwezi sasa, ni washukiwa wa uhalifu. Uhalifu upi..? Fujo, vurugu, kuharibu mali na matusi, angalau kwa kutaja machache. Wanataka sana hilo ndilo limezeshwe kwenye akili zetu sisi wazanzibari. Kila mtu aimbe wimbo huo na mwisho wa siku, sote tuingie kwenye kapu moja la uzembe na uvivu wa kufikiri na ujinga usio kuwa na mwisho.
Lakini shukurani kwa mifumo ya sasa ya kimawasiliano, serikali na vyombo vyake wametukuta wengi wetu tukiwa hatudanganyiki tena na ulaghai wake. Hata kama tunaweza tusiwe na nguvu za kimabavu ilizonazo serikali feki ya zanzibar, maana sisi hatuna polisi, jela wala mahakama, lakini tuna nguvu ya dhamira zetu. Nayo ni nguvu kubwa, kwa hakika.
Kwa nguvu hiyo, ya kuwa na akili huru, ndipo tunakataa kuumeza uongo wa serikali feki wa “kuwahalifisha” viongozi wa Uamsho na wafuasi wao ambao sote ni waznzibari tunao taka nchi yetu. Tunajua – kama inavyojua hiyo serikali feki na vyombo vyake – kwamba viongozi wa Uamsho wanaadhibiwa kwa sababu ya msimamo wao wa kisiasa. Msimamo wa kuitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili, nje ya Muungano wakulazimishana na muungano wakuomeza zanzibar na muungano wa WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA.
Ikiwa kuna kosa lolote ambalo leo hii limemfanywa na Sheikh Msellem Ally ajikute akishindwa kumuuguza na hatimaye kumzika mwanawe mzazi, ni hilo la kwamba ni kiongozi aliyewaongoza Wazanzibari kuidai haki yao ya kuwa huru, heshima yao ya kujiamulia na dhamira yao ya kusonga mbele kama taifa HURU LA ZANZIBAR kama yalivyo mataifa mengine ulimwenguni.
Kwa kufanyiwa wanayofanyiwa viongozi wa Uamsho, serikali feki na vyombo vyake wanajidanganya kwamba wanalizima vuguvugu lililokwishapamba moto la Wazanzibari kudai mamlaka kamili ya nchi yao.
Na hili la upande wa serikali feki na mawakala wake linaweza kuelezeka ingawa halikubaliki. Lakini ambalo haliwezi kuelezeka, kukubalika, wala kuvumilika ni hili la kimya chetu sisi wengine, ambao tunaguswa na dhamira wanayoisimamia akina Sheikh Msellem.
Kwa sababu ya kutotaka kuitwa Uamsho, mimi na wenzangu wengi, tumeshindwa hata kuandika mistari miwili mitatu ya kusimama na viongozi hawa. Tunawaachia waadhibiwe, wateswe, wadhalilishwe kimwili na kisaikolojia. Kama nilivyosema hapo kabla, inawezkena hatuna nguvu za kuwanusuru na mkono dhalimu wenye nguvu wa dola, lakini tunao uwezo wa kuwahuisha mbele ya makini za watu: kuwasafishia majina na kuzitukuza thamani zao, kwa kutokubali “kuununua” uzushi dhidi yao.
Hawa si magaidi, si mahaini, si majambazi,kama ilivyo serekali hii toka itokako imeuwa watu tele imefunga watu tele jela imeharibu wanawake na wasichana tele na mpaka sasa inaendelea na mfumo huo huo wa kuwafunga kila anae dai zanzibar na kuwathalilisha watu. na hao wanoitwa uamsho kwa hakika hata si wahalifu. Hawapo walipo sasa kwa sababu wameiba, wameua au wamemdhulumu mtu. Wapo walipo kwa kuwa wanapigania nchi yao – heshima ya taifa lao. Hawa ni wa kutukuzwa si wa kupewa mgongo! Si wa kupigwa pande!
No comments:
Post a Comment