Tuesday, December 18, 2012

WAHAFIDHINA NCHINI ZANZIBAR HAWANA PAKUKIMBILIA WAMUWA KUBADILIKA.UKUSANYAJI WA MAONI BAADA KUMALIZA ZANZIBAR NZIMA


MAONI KWA ZANZIBAR NZIMA:
Ukichukua mwelekeo wa maoni yote yaliyotolewa hadharani katika mikutano yote iliyofanywa na Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba katika visiwa vya Zanzibar unapata picha ifuatayo:

Waliotaka Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kufuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 14,998 sawa na 65.98%. Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano (Serikali Mbili) uendelee ni 7,034 sawa na asilimia 30.94%. Waliotaka Serikali Tatu ni 105 sawa na 0.46%. Waliotaka Serikali Moja ni 22 sawa na 0.9%. Waliotoa maoni mengine ni 573 sawa na 2.52%.

MTAZAMO BINAFSI: Inafurahisha kuona wapenda mabadiliko (progressives) katika Zanzibar kwa ujumla asilimia yao imebakia takriban ile ile 66% ambayo ndiyo iliunga mkono kuanzishwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010. Kwa upande mwengine,wahafidhina wanaokataa mabadiliko katika jamii ya Zanzibar wanazidi kupungua kutoka asilimia 33% hadi
asilimia 31%.

No comments:

Post a Comment