A A KARUME risala hii ya Uhuru Alisoma kwa niaba ya Afro-Shirazi Party wote.
Mzee Karume alisema tunachukuwa fursa hii kuwapa mkono wa furaha watu wote wa visiwa hivi kwa jtihada yao na bidii kubwa, pamoja na misaada mikubwa katika juhudi zetu sote za kuupinga ukoloni na utawala wa kibeberu. Jitihada . Leo mwezi 10 Disemba, 1963, ZANZIBAR imekuwa Huru.
Mzee Karume akaendelea kusema Hii leo sisi watu wa visiwa hivi tumepata haki ya kuchukuwa mahala petu kuwa ni Dola sawa na nyengine katika umoja wa Nchi za Dola za Commonwealth.
Kwa uchache, kuwa mwanachama katika umoja huo, kuna maana kwamba nchi hii ni huru chini ya mpango wa serekali ambayo msingi wake umejengwa juu ya kuendelea kwa ridhaa ya wanaotawaliwa. Ili kufikia matarajio yetu hayo tunayo moja katika Katiba zenye msingi madhubuti iliohusika na shuruti za haki za binadamu, haki za mambo ya siasa na uhuru wa dola yoyote nyengine.
Ni wajibu wa watu wote wa dola yetu mpya, kila mmoja katika sisi bila yakujali fikra zetu za siasa au madaraka yetu kusaidia kweli kweli katiba yetu iweze kufanya kazi. Pamoja na manufaa, haki na uhuru ambayo yote hayo yamepatikana baada ya nchi kuwa huru leo hii 10 Disemba 1963.
Vile vile yapo mambo yaliyo wajibu na lazima ambayo imebidi yatimizwe kwa ajili ya dola na kwa ajili yetu wenyewe kila mmoja juu ya mwenziwe. Kwa hakika kwa ajili ya wajibati hizo na mambo yalo lazima, kama ilivyo juu kufurahikia haki za uraia na haki za siasa na uhuru mbali mbali basi vile vile uhuru wetu lazima utimizwe kwa njia hizo.
Tuliyoyapata leo mwezi 10 Disemba ni mipango ya mwanzo tu ya kuweza kufanya juhudi kwa ukamilifu dhidi ya maadui zetu nao ni ujinga, umasikini na maradhi na kuweza kuleta imani penye khofu na shaka na kuleta masikilizano mahala ambapo hata hivi sasa dawa ipo, na kuleta mapenzi mahala ambapo pana chuki, ili dola yetu mpya ichomoze katika neema, umoja na furaha kwa sote wazanzibar.
Kwa hivyo katika hii siku ya leo na tumwombe Mwenye Enzi Mungu, Inshallah atuweke tuifanye na tuitimilize kazi kubwa ya kujenga taifa ili dola yetu mpya ya ZANZIBAR ipate baraka ya matunda mema ya kazi zetu.
Uhuru na Umoja, Uhuru na kazi!”.
Jarida la MAARIFA la Serikali ya Zanzibar. Makala maalumu kwa kufikilia Uhuru. Jumaane, 10 Disemba, 1963.
No comments:
Post a Comment