Thursday, January 19, 2012

SEREKALI YA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA IMEAMUWA KWENDA U.N.KUDAI NYONGEZA YA ENEO LA BAHARI BAINA YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

IMG_1616
Thursday, January 19, 2012
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka ( Mb) akimkabidhi kwa niaba ya Serikali ya TANGANYIKA, Mkurugenzi wa Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Bahari na Sheria ya Bahari, Sergei Tarassenko, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Andiko la kudai nyongeza ya maili 61,000 nje ya eneo la maili 200 la Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana jumatano katika ofisi za Idara hiyo zilizopo katika Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani
NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK
SEREKALI HII YA TANGANYIKA, imewasilisha katika Umoja wa Mataifa, Andiko la kudai eneo la nyongeza lenye ukubwa wa maili 16,000 nje ya eneo la sasa la maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari.
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) ndiye aliyewasilisha Andiko hilo, kwa niaba ya serikali, katika hafla fupi na ya kihistoria iliyofanyika siku ya jumatano katika ofisi za Idara ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Bahari na Sheria ya Bahari.
Andiko hilo limepokelewa na Mkurugenzi wa Idara hiyo, Bw. Sergei Tarassenko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. ambaye aliipongeza TANGANYIKA kwa hatua hiyo muhimu na kuahidi kwamba Idara yake kupitia, Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mipaka ya baharí italifanyi kazi Andiko hili.
Aidha Mkurugenzi huyo ameielezea TANGANYIKA, kama moja kati ya nchi inayoheshima sana na yenye historia nzuri katika Umoja wa Mataifa.MAWE
Akizungumza wakati wa kuwasilisha Andiko hilo, Waziri Anna Tibaijuka, amesema kwa kuwasilisha Andiko hilo, TANGANYIKA si tu kwamba imefanya kazi ya uhakika ya maandalizi na hatimaye uwasilishaji lakini ni hatua kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa TANGANYIKA.((MUNAFIKIRI WAZENJI NI WAJINGA SANA BINU YENU HAPA NI KUHAKIKISHA MAFUTA YANAINGIA KATIKA MIPAKA YA TANGANYIKA KISHA NDIO MUVUNJE MUUNGANO NA ASIYEJUWA MBINU HII....?
Akabanisha kwamba mchakato wa maandalizi ya Andiko hilo ambao umechukua miaka mitano, umewashirikisha wataalamu mbalimbali wakiwamo wa ndani na nje , ikiwa ni pamoja na kuzihusisha nchi ambazo zinapakana kibahari na TANGANYIKA.((JE SEREKALI YA ZANZIBAR MUMEIHUSISHA KAMA YES NANI ALIYEKUWA KATIKA KIKAO HICHOO..?
Akizungumza manufaa ya kudai nyongeza ya eneo hilo, Waziri Tibaijuka anasema. “ TANGANYIKA itanufaika kwa kuongeza ukubwa wa eneo la mipaka ya nchi lakini la msingi zaidi ni unufaikaji wa rasilimali zikiwamo za MAFUTAA na GESII na madini ambazo zitakuwamo katika eneo hilo jipya, rasilimali ambazo kwa sasa zinaelekea kutoweka katika eneo la maili 200”.((YANATOWEKA SASA NDIO MUNATAKA NYONGEZA MUZIDI KUVIMBA NA KUSINZIA BUNGENI DODOMA AU SIO..?
Eneo ambalo TANGANYIKA inadai liongezwe la maili 61, 000 ukubwa wake ni sawa na eneo la mikoa mitatu ikiunganishwa kwa pamoja.
Aidha kuongezwa kwa eneo hilo kutaisaidia pia serikali katika masuala ya ulinzi na usalama hasa katika kipindi hiki ambacho vitendo vya uharamia wa baharini vikiwa vimeongeza katika eneo la bahari ya Hindi.
“ Pamoja na kuwasilisha Andiko hilo, lakini nchi yangu inapenda pia kutoa ombi la pekee kwa idara yako, kuangalia uwezekano wa kuharakisha mchakato wa kupitia nyaraka na vielelezo tulivyowasilisha katika Andiko letu, kwani itatusaidia sana katika ulinzi wa eneo la mipaka yetu dhidi ya uharamia” akasisitiza Waziri .
Na kuongeza kwamba TANGANYIKA, kama ilivyo kwa nchi nyingine ambazo zinaendelea zinahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwamo Idara ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya bahari na sheria ya bahari katika kuukabili uharamia.((NYINYI NDIO MAHARAMIA WA KWANZA KABISA.
Faida nyingine ukiacha za kiuchumi ni kwa wataalamu wa fani mbalimbali kuwa na fursa ya kufanya utafiti katika eneo hilo hapo litakapokuwa limeridhiwa rasmi na kuwa sehemu ya TANGANYIKA.
Baada ya kuwasilisha Andiko hilo, hatua inayofuatia ni kwa TANGANYIKA kupitia wataalamu wake, itatakiwa kulitetea Andiko hilo mbele ya Makamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Mipaka ya Bahari utetezi huo utafanyika mwezi Agosti mwaka huu.
TANGANYIKA imewasilisha Andiko hilo kwa kuzingatia Sheria ya kimataifa ya Bahari namba 76 kifungu kidogo cha 4, sheria hiyo inaziruhusu nchi ambazo ziko kando kando ya bahari kudai eneo la nyongeza iwapo zitakidhi vigezo vilivyotolewa na Umoja wa Mataifa.((NYINYI MUMEKIDHI..?HAHAHAHAH
Mchakato wa kuanda Andiko hilo ulianza mwaka 2007 ukiwashirikisha wataalamu wa kada mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Chuo Kikuu cha Ardhi na Mazingira, Wizara ya Sayansi na Teknolojia na Shirika la Maendeleo ya Petroli ( TPDC).
Sehemu kubwa ya Mradi imefadhiliwa na Serikali Kuu na kwa kusaidiwa na Serikali ya Norway.
Hafla ya kuwasilisha Andiko hilo imehudhuriwa na Balozi wa TANGANYIKA katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue, na waheshimiwa wabunge, Zakhia Meghji na Abulrahman Hassan Shah ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
Wengine waliohudhuri hafla hiyo ni baadhi ya wataalamu waliohusika na maandalizi ya Andiko hilo ambao ni Dr. Sellasie Mayunga, Prof. Evelyne Mbende, Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Kelvin Komba na Bi. Verdiana Mashingia.
TANGANYIKA inakuwa nchi ya 59 kuwasilisha Andiko la kudai nyongeza ya eneo la bahari na ikiwa ni nchi 10 kutoka Afrika kufanya hivyo.TAAMAA TU BASI JINCHI KUBWA KITU GANI LAKINI BADO TU MUTAKUFA MUTAYAWACHA HAPA HAPA KAMA BABA YENU NYERERE MBONA HAKWENDA NAYO HUKO KABURINI KWAKE......?

No comments:

Post a Comment