Saturday, September 29, 2012

HILI NI JIBU KWA UAMSHO IKIJIBIWA NA KUEKWA SAWA

salaam,

Huu ni ukumbusho na wasia kwa Mashekhe wetu kama alivyosema Allah (swt) kuwa “kumbusha kwani ukumbusho utamfaa mwenye imani”

Allah (swt) amesema katika Qur’an kuwa “Na wala msiufiche haki (ukweli) kwa upotevu na kubadilisha ukweli na hali yakuwa munajuwa”.,(kwa tafsiri ya karibu).

Kama tunahitaji uhuru kama wanavyodai hawa Mashekhe wetu basi kwanza tudai uhuru kutoka kwa hao viongozi wa visiwani iliwatuache tujitawale kwa mujibu wa sharia za Muunba wetu na si kwa sharia za viumbe hao. Hii ndio HAKI yetu kubwa ya kuidai kutoka kwao na hawa mashekhe wetu ni lazima wawe msitari wa mbele katika kutekeleza hilo. Mtume wetu kiumbe bora kuliko viumbe vyote duniani anadhalilishwa na hatuna nguvu ya kuzuia hilo. Allah (swt) anapuuzwa na wao hao viongozi wanaruhusu kukejiliwa kwa sharia za Allah (swt) nasisi waislamu tumeona la muhimu zaidi ni Utaifa wetu tuliojipachika kwa visiwa tulivyo azimwa na Muumba kwa muda mchahe. Nini tutajibu kwa uzinufu ulioenea hapo visiwani?, nini tutajibu kwa mabaa na ulivi uliojaa?, nini tutajibu kwa ubaradhuli uliozagaa?, nini tutajibu kwa wizi na ujambazi uliofunika?, nini tutajibu kwa utebeaji uchi wa binaadamu uliowazi?, nini tutajibu kwa riba iliyotawala uchumi na riziki zetu?

Hivyo tusimtumie Allah (swt) pale tunapotaka masilahi yetu binafsi na kumsahau au kumpuuza pale sharia inapohitajika kutekelezwa. Visiwa vya Zanzibar na ardhi yote duniani ni yake Allah (swt) na katujaalia sisi wanaadamu hususan waislamu kuwa ni wasimamizi na wachunga wa amana hiyo. Pia akatuteremshia katiba na sharia ya kutuongaza vipi tuenendeshe maisha yetu hapa duniani ili tuokoke na moto na ghadhabu zake kesho Akhera. kama aliposema katika Qur’an kuwa “Hakika hukumu zote ni zake Allah na ameamrisha kuwa asitiiwe yoyote ispokuwa yeye tu.” na aliposema kuwa “Na yeyote atakayepuuza materemsho yangu basi hao watakuwa na maisha ya dhiki duniani na kesho Akhera watakuwa ni weye khasara.”

Leo vipi hukumu zinazotutawala ni kinyume na zinapinga ufalme wake Allah (swt) halifu eti hapo tunamuomba atusaidie kwa kuzidi kumdhulumu haki yake ya kutawalishwa kwa sahria zake. Jee huu si unafiki? kama alivyo sema katika Qur’an kuwa “Na yeyote asiyehukumu (hukumiwa) kwa sharia alizoteremsha Allah basi hao ni madhalimu” na aya inayofuatia amemalizia kwa kusema basi hao ni mafasiki.

Sasa tujiulizeni Je tunamfanyia Mungu kejeli? au Kuwa yeye ni Mungu wa kutekeleza matakwa yetu tu? au yeye ni Mungu wa swala, funga na hajji tu?

Najuwa baadhi watajibu kwa kusema kuwa tuachwe tupumuwe…. basi na pia tufikirie kauli hiyo kwa Allah (swt) itakuwa na maana gani, “kuwa atuache kwanza tupumuwe kisha yake yatafuatia baadaye tukitaka !

Amesema Allah (swt) kuwa “Enyi mlioamini ! muogopeni Allah kadri anavyostahiki kuogopewa na wala msife ila isipokuwa ni waislamu (mumejisilimisha kikamilifu).” Mwenyezi Mungu hapa anatutaka tufe haliyakuwa ni Waislamu. na katika aya zake ametuzungumza kwa neno la Muslimoona, Muuminoona, Mutaqoona. nk. na katu hatuzungumza kama Wazanzibari wala wataifa fulani. Vipi leo tunajivuna kwa majina ambayo Allah (swt) hakutuita?

Waumini hatujuwi mauti yatatukuta wakati gani na katika hali gani na tukiwa tumishikia kauli ipi kati ya hizi mbili “tuachwe tupumuwe” au “Laa ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah” Ni jukumu letu kuvikombowa visiwa hivyo na Afrika Mashariki nzima kutoka katika tawala za kitwaghuti za kisheria za kibanaadamu na kusimamisha sharia zake Allah (swt) kama tunavyojidai kusoma katika sura Al-Fatiha katiak kila sala kuwa “Yeye tu pekee ndiye tunaye muabudu (kwa kumtii sharia zake) na yeye tu ndiye tunayemuomba msaada wake.”

Yaa Allah tusamehe makosa yetu na uturuzuku uongozi wa sharia zako na tujiite Waislamu kama alivyotuiita baba yetu Nabii Ibrahimu (a.s). Amin.

Wabillahi Tawfiq

No comments:

Post a Comment