salaam,
Huu ni ukumbusho na wasia kwa Mashekhe wetu kama alivyosema Allah (swt) kuwa
“kumbusha kwani ukumbusho utamfaa mwenye imani”
Allah (swt) amesema katika Qur’an kuwa “Na wala msiufiche haki (ukweli) kwa
upotevu na kubadilisha ukweli na hali yakuwa munajuwa”.,(kwa tafsiri ya karibu).
Kama tunahitaji uhuru kama wanavyodai hawa Mashekhe wetu basi kwanza tudai
uhuru kutoka kwa hao viongozi wa visiwani iliwatuache tujitawale kwa mujibu wa
sharia za Muunba wetu na si kwa sharia za viumbe hao. Hii ndio HAKI yetu kubwa
ya kuidai kutoka kwao na hawa mashekhe wetu ni lazima wawe msitari wa mbele
katika kutekeleza hilo. Mtume wetu kiumbe bora kuliko viumbe vyote duniani
anadhalilishwa na hatuna nguvu ya kuzuia hilo. Allah (swt) anapuuzwa na wao hao
viongozi wanaruhusu kukejiliwa kwa sharia za Allah (swt) nasisi waislamu tumeona
la muhimu zaidi ni Utaifa wetu tuliojipachika kwa visiwa tulivyo azimwa na
Muumba kwa muda mchahe. Nini tutajibu kwa uzinufu ulioenea hapo visiwani?, nini
tutajibu kwa mabaa na ulivi uliojaa?, nini tutajibu kwa ubaradhuli uliozagaa?,
nini tutajibu kwa wizi na ujambazi uliofunika?, nini tutajibu kwa utebeaji uchi
wa binaadamu uliowazi?, nini tutajibu kwa riba iliyotawala uchumi na riziki
zetu?
Hivyo tusimtumie Allah (swt) pale tunapotaka masilahi yetu binafsi na
kumsahau au kumpuuza pale sharia inapohitajika kutekelezwa. Visiwa vya Zanzibar
na ardhi yote duniani ni yake Allah (swt) na katujaalia sisi wanaadamu hususan
waislamu kuwa ni wasimamizi na wachunga wa amana hiyo. Pia akatuteremshia katiba
na sharia ya kutuongaza vipi tuenendeshe maisha yetu hapa duniani ili tuokoke na
moto na ghadhabu zake kesho Akhera. kama aliposema katika Qur’an kuwa “Hakika
hukumu zote ni zake Allah na ameamrisha kuwa asitiiwe yoyote ispokuwa yeye tu.”
na aliposema kuwa “Na yeyote atakayepuuza materemsho yangu basi hao watakuwa na
maisha ya dhiki duniani na kesho Akhera watakuwa ni weye khasara.”
Leo vipi hukumu zinazotutawala ni kinyume na zinapinga ufalme wake Allah
(swt) halifu eti hapo tunamuomba atusaidie kwa kuzidi kumdhulumu haki yake ya
kutawalishwa kwa sahria zake. Jee huu si unafiki? kama alivyo sema katika Qur’an
kuwa “Na yeyote asiyehukumu (hukumiwa) kwa sharia alizoteremsha Allah basi hao
ni madhalimu” na aya inayofuatia amemalizia kwa kusema basi hao ni mafasiki.
Sasa tujiulizeni Je tunamfanyia Mungu kejeli? au Kuwa yeye ni Mungu wa
kutekeleza matakwa yetu tu? au yeye ni Mungu wa swala, funga na hajji tu?
Najuwa baadhi watajibu kwa kusema kuwa tuachwe tupumuwe…. basi na pia
tufikirie kauli hiyo kwa Allah (swt) itakuwa na maana gani, “kuwa atuache kwanza
tupumuwe kisha yake yatafuatia baadaye tukitaka !
Amesema Allah (swt) kuwa “Enyi mlioamini ! muogopeni Allah kadri
anavyostahiki kuogopewa na wala msife ila isipokuwa ni waislamu (mumejisilimisha
kikamilifu).” Mwenyezi Mungu hapa anatutaka tufe haliyakuwa ni Waislamu. na
katika aya zake ametuzungumza kwa neno la Muslimoona, Muuminoona, Mutaqoona. nk.
na katu hatuzungumza kama Wazanzibari wala wataifa fulani. Vipi leo tunajivuna
kwa majina ambayo Allah (swt) hakutuita?
Waumini hatujuwi mauti yatatukuta wakati gani na katika hali gani na tukiwa
tumishikia kauli ipi kati ya hizi mbili “tuachwe tupumuwe” au “Laa ilaha illa
Allah Muhammad Rasul Allah” Ni jukumu letu kuvikombowa visiwa hivyo na Afrika
Mashariki nzima kutoka katika tawala za kitwaghuti za kisheria za kibanaadamu na
kusimamisha sharia zake Allah (swt) kama tunavyojidai kusoma katika sura
Al-Fatiha katiak kila sala kuwa “Yeye tu pekee ndiye tunaye muabudu (kwa kumtii
sharia zake) na yeye tu ndiye tunayemuomba msaada wake.”
Yaa Allah tusamehe makosa yetu na uturuzuku uongozi wa sharia zako na tujiite
Waislamu kama alivyotuiita baba yetu Nabii Ibrahimu (a.s). Amin.
Wabillahi Tawfiq
MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment