wananchi wa zanzibar wametakiwa kuwa na umoja wenye msimamo madhubuti wa fikra za ukombozi wa nchi yao pamoja na kuepuka madai ya watu wachache yasiyo sahihi yanaoandaliwa ili kuweza kuugawa umoja wao na kuwarudisha kule kule walipotoka.
Hayo yameelezwa na ustadh Sleiman Haji alipokua akiwahutubia waislamu na wapenzi wote wa zanzibar katika mhadhara uliofanyika katika viwanja vya msikiti wa mbuyuni, mhadhara huo uliohudhuriwa na mamia ya wazanzibar ust Sleiman amesema kuna mbinu nyingi zimeandaliwa juu ya jumuiya ya muamsho ili kuweza kuiondoa hivyo amewataka wazanzibar kujipanga upya kuweza kukabiliana na mbinu zinazoandaliwa ili kuweza kuzishinda na wazanzibar kuendelea mbele na harakati zao za ukombozi wa zanzibar ili kuweza kupata mamlaka kamili ya nchi yao.
Nae ust Mussa Ame amewataka waislamu kuonesha hisia zao za kuchukizwa kwa kitendo kilichofanywa na maadui wa uislamu kwa kumdhalilisha Mtume Muhammad S.A.W hivyo ameonesha masikito yake kwa kuona nchi kama ya zanzibar ambayo ina jumla ya waislamu 99% lakini serikali ya mapinduzi ya zanzibar inashindwa kutoa matamko dhidi ya vitendo mbali mbali wanavyofanyiwa waislamu likiwemo suala la kudhalilishwa Mtume s.a.w.
Nae kwa upande wake amiri wa jumuiya ya muamsho amesema vyombo vya ulinzi nchini Tanzania havifanyi kazi ya kuilinda nchi, kuangalia sheria za nchi au maslahi ya raia bali wanalinda vikundi vya watu wasio nahatia ambao wanaitakia mema nchi yao ili kuweza kuikomboa na kuwa na mamlaka yake. hivyo amewataka wazanzibar wasikubali kauburuzwa na kugawnywa katika kudai haki yao.
No comments:
Post a Comment