Sunday, November 18, 2012

HII NDIO CCM NAKILA ANAYE IFUATA AJUWE NDANI YA KICHWA CHAKE HIVI NDIVYO KILIVYO,MKITAKA MSITAKI MABADILIKO YATAKUJA TUUNyerere laana ya m/mungu imfikie huko huko aliko alithubutu kumwita Kolimba na Malecela kama ni wahuni, kwahiyo Uhuni umejaa CCM na kwa kweli kama tutaendelea kuwa ndani ya utawala wao tujuwe nikuzama na wahuni hao wapo tayari kufanya lolote lile almuradi kupata maslahi yao, ikiwa kuuwa, kuiba, kufitini liwe lolote lile baya, muhimu wanaweza kulifikia lengo lao.
Ikiwa wana CCM kama kweli wanamthamini Abied Amani Karume kwa mila na tamaduni zetu za Kizanzibari mtoto wake na familia yake siku zote zitakuwa zinatukuzwa, lakini kinyume chake ndio hiki leo kumtukana Amani ni sawa kumtukana Baba Karume, tabu nikuwa mhuni hajui alifanyalo ndio tabu yake.
Hawa ni watu hatari sana na lazima kutafutwe suluhisho la mara moja la kuwadhibiti. Mwanamume huwa hana matusi ila awe baradhuli, hakika waandishi hawa wa Kisonge wengi wao ni kaumi hiyo wakiongozwa na Borafya, kutokana na malezi mema ya Kiislamu niliyopewa siwezi kutukana kama wao, lakini ni aibu kwa Borafya huko nyuma alivyowahi kuwa na mambo aliyoyafanya na kwa kweli kile ni chombo kilichokuwa kinakwenda mperampera karibu kitagonga mwamba, subra ni muhimu, ingawa mwenye kasema kala nyama ya mbwa dua hazimpati.
CCM Kisonge wajuwe dunia haibaki kama wanvyofikiria mabadiliko hutokea bila ya mtu kuelewa, wapi Iran na Shah, wapi DDR na Honicker, wapi Yugoslavia na Tito, wapi Romania na Sacisko, wapi Somalia na Said Bare wapi zitakuwa ni nyingi na kutoweka kwake hakuna aliofikiria. Karibuni tumeona tawala kuporomoka kama Misri, Tunisia, Libya ambako hakuna mmoja alitarajia ipo siku yatakuwa hayo, tunajuwa waliofungika kiakili wanaamini CCM na Zanzibar ya kisonge kubakia milele, kwasababu hawajasoma na kutegemea fitna na ubaradhuli kuweza kuwafanya maisha yao yaweze kwenda. Wakati utawasuta watu na watake kujinyonga na kuiona dunia sio.
Amani hawezi kushtakiwa na madhalimu, kwani kumshtaki Amani ni kukishtaki chama cha CCM, Zanzibar na Bara. CCM imejaa dhulma, walimdhulumu Bilali wakampa Amani, sasa leo wanasema nini? Frankenstein amemtengeneza kiumbe kaanza kuleta mashaka, sasa huku hawa wapumbavu wameshindwa kuelewa leo wanatukana nini?
Kumtukana Bibi Fatma Karume nikujiuliza ni kweli huyu alikuwa mke wa muasisi wa Mapinduzi? Hapa ndipo ninapofahamu Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru, kuwa waliofanya Mapinduzi sio sisi wenyewe Wazanzibari, matokeo kile kizazi kichafu cha kina Injini na Mfaranyaki ndicho hadi leo kinaisumbua Zanzibar. Hakuna marefu yasio na mapana na hakuna Kiza kisichopambanukiwa. Mapinduzi sio daima lakini haki ndio daima.

No comments:

Post a Comment