Thursday, November 29, 2012

MSAANI MARUFU SHARO-HUSSEIN AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI-WASHENZI WATANGANYIKA WAMUIBIA KILA KITU CHAKE NA KUMUWACHA NUSU UCHI HALI YAKUWA NI MAITI



Binadamu wote duniani wameumbwa na utambulisho Fulani. Ukiachilia mbali rangi, na kabila kuwa vilingo mahususi vya utambulisho wa mtu, Mila na utamaduni ni kipimo chengine kikubwa cha kuupima utu na utambulisho wa mtu au watu wa jamii Fulani. Utamaduni katika fasili yoyote ile utaingiana na mazoea yaliyoselelea kufanywa au kutendwa na watu Fulani katika jamii au jamii kwa ujumla kama sehemu ya utaratibu wao wa maisha ya kijamii. Huu huweza kuitwa utamaduni.
Ikiwa ni siku nne hivi tangu kufariki kwa ajali mbaya ya gari, msanii Chipukizi Hussein Mkeity maarufu kama Sharo Milionea, katika wilaya ya Muheza kule Tanga, matukio yaliyofanyika baada ya kifo hicho yalizidi tukio lenyewe la ajali. Kwa ufupi tu, baada ya gari la msanii huyo kupindukia na kung’oa roho yake, kilichofanyika pale ni kwa wanakijiji wa kata ile ya Muheza waliokuwepo kukimbilia kumpora maiti huyo kila kitu.
 HUSSEIN MARUFU SHARO MILLIONEA BAADA YA KUFAA NA KUPORWA KILA KITU CHAKE ALICHOKUWA NACHO KATIKA GARI  BADALA  YA KUMSAIDIA WAO WANAMPORA VITU VYAKE WASHENZI NI WASHENZI TU WATANGANYIKA NI WASHENZI WAKUBWA.
Washenzi hao walidiriki kumvua nguo maiti na kumuacha akiwa nusu uchi badala ya kumsitiri. Kitendo hichi sitaki nikitolee fatwa kuwa ni kizuri bali ni kitendo cha kinyama nasijali kusema hivyo kwani kila mtu na atakavyokichukulia kwa sasa kwa mujibu wa mila na desturi za mtu huyo. Kilichonishangaza zaidi ni wakati naperuzi kurasa za magazeti ya hapa nyumbani leo asubuhi ambapo niliona tahariri katika gazeti la ‘Nipashe’, iliyoandikwa na mwandishi maalum, yenye kichwa cha habari ‘Kupora maiti ni unyama usiopimika’. Hili lilinishangaza kwa sababu nyingi sana.
Kwanza, kwanini kupora maiti tu iwe ndio unyama usiopimika..? Kwa taswira za kimaana ya kilugha hapa tunaona kwa mbali kuwa kuna taswira kuwa mwandishi anaamini kuwa kupora si kitu cha ajabu sana kwa nchi ya Tanganyika lakini kupora maiti ndio ni unyama mkubwa zaidi. Pia Napata taswira kuwa kuna badhi ya matukio haya ya kupora ambayo mwandishi wa tahariri anayaona yanapimika au kwa kiasi hayashitui sana kwani yanastahiki kutokea hivyo. Si vibaya, ndio nikasema kila mtu na anavyouona ubaya kwa macho yake na akili yake.
Pili, hii si ajali ya kwanza mbaya kutokea maeneo ya nchi hii ya Tanganyika. Kuna ajali mbaya zaidi zilizouwa watu wengi mno na hutokezea kila mwaka si chini ya mara kumi hapa nchini Tanganyika na hasa hasa dar au mikowani. Katika matukio yote haya, jambo la kwanza baada ya ajali kutokea tu wananchi hukimbilia kuiba kilakilichopo, kiwe mwilini au kimezagaa chini, kiwe cha maiti au cha majeruhi. Huu umekuwa ndio utamaduni wa Watanganyika kila panapotokea ajali. Na kama kuna mtu anabisha ajitokeze.
GARI ALILOPINDUKA NALO HUSSEIN SHARO MILLIONEA NA KUIBIWA KILA KITU CHAKE
Kwa bahati Nzuri au mbaya, binadamu hasikii uvundo wake anaounuka mwenyewe mpaka uzidi kipimo na kuudhi mpaka masafa marefu. Hapo kwa mbali ataanza kuhisi kuwa kweli ananuka uvundo na ataanza kufikiria mbinu za kujipapatua na hili. Katika hali kama hii tunasema huwa maji yamezidi Unga. Na hichi ndicho alichokiona muandishi wa tahariri hii katika Gazeti la Nipashe.
Kuna kila sababu ya mwandishi kulaani kitendo kile kwa sasa ijapokuwa ndio mazoea ya Watanganyika katika nchi yao ya Tanganyika huko kufanya hivyo kila siku na kila mara ajali zinapotokea. Nafikiri jambo lililomsukuma mwandishi kulaani kitendo hicho labda ni kuwa aliekufa ni msanii maarufu na kwa hivyo hakustahili kuporwa na sio tu kwa sababu ni maiti. Kuna maiti kadhaa huporwa katika ajali tena huwa wengi kuliko Sharo mmoja aliyekufa akiwa pekee garini. Hatuoni maandiko yoyote ya kulaani kitendo hicho.
Sababu ya pili yawezekana na vile kuwa tukio hili la uporaji limeripotiwa wazi wazi katika vyombo vya habari sambamba na ripoti za kifo cha msanii huyo. Wachilia mbali kitendo cha kupachika picha yenye kutisha katika vyombo vya habari ya maiti ya msanii huyo kuwa ni jambo la aibu na kashfa katika mila na tamuduni za waungwana wa Kitanganyika,je tukio la kumvua maiti nguo na kumuacha hali ya nusu uchi kama ilivyoripitiwa bila kutia chenga je hili..? pia imewatia aibu watu wa Muheza,na nchi ya Tanganyika  kwa ujumla.
Na labda kwa kuchelea hili, mwandishi wa Nipashe akaamuwa kujikosha, bila kujua kuwa kukoga sio kusafika. Na kwa hili bado hatujasafika kwa kulaani kitendo cha kupora maiti, kwani huu ni utamaduni na mazoea Yawatanganyika wakiwa nchini kwao na hata wakiwa nchi za nje wanajulikana kwa umarufu wa kupora watu na kuibiya watu na kusema uwongo huwo ndio utamaduni wa Watanganyika.Ndio kwanza mkoko unaalika mauwa. Utamaduni haubadiliki siku moja, tuendelee kuulani, si kwa sharobaro tu na mabasi ya mikoani pia. Funika kombe mwanaharamu apite.

M/MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI

No comments:

Post a Comment