MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Friday, November 9, 2012
SHEIN ASEMA SHEIKH FARID NA WENZAKE BORA WAFIYE WANTANAMO YANGU KULIKO MIMI KUONDOLEWA MADARAKANI NA MASULTANI WANGU WA TANGANYIKA.
MAAMIRI,WAKOMBOZI,WATETEZI WA HAKI,VIONGOZI WAMINIFU,MASHUJA,WAUNGWANA,WAPENDA HAKI,WAPENDA AMANI,WASIOTAKA THULMAA,BADO WAKANDAMIZWA NA SEREKALI YA THULMA.SMZ WAUWAJI
SHEIKH MUSSA NA SHEIKH AZZAN WAKITOKA NJE YA KUTI YA MAJAHILI
Miongoni mwa SHEIN na Vikundi vyake vya kiharamia cha kuwatesa wakombozi na wazanzibari kwa ujumla.hapa z,bar SHEIN ndio mkiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na serekali yake ya kikafiri imekuwa na ukiukwaji wa haki za wafungwa hao ni pamoja na kuto kuruhusiwa kubadili nguo ambapo tangu walipokamatwa hawajaruhusiwa kubadilisha nguo kazi nzuri ya SHEIN anayowafanyia mamiri hawa, kulazimishwa kunyolewa ndevu, kukatazwa kuonana na jamaa zao, pamoja na kutengwa kila mmoja katika chumba maalumu chini ya ulinzi mkali.
Mambo mengine ambayo yameelezwa mahakamani hapo ni kulazwa chini ya sakafu, kujisaidia ndani ya ndoo (mtondoo), na kunyimwa fursa ya kufanya ibada yani hawaruhusiwi kuswali je huyu SHEIN kwali muislamu huyu maana serekali yake inafanya mambo hata makafiri hawafanyi pia ni mambo ambayo yanakwenda kinyume na KATIBA maana wao wanabudu na kuifuata zaidi KATIBA kuliko QURAAN kuhusu haki ya kuabudu na kufungiwa ndani ya vyumba saa 24 mambo ambayo hayapaswi kufanyiwa kwa sababu bado ni watuhumiwa hawajatiwa hatiani na ni kinyume na haki za binaadamu na kinyume na katiba.
Wakinukuu baadhi ya vifungu vya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1988 inayotoa fursa ya watu wote kuwa sawa mbele ya sheria, haki ya kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria, mawakili hao wamedai kuwa wateja wao wamekuwa wakikosa haki hizo na kutendewa tafauti na watuhumiwa wengine waliopo rumande.
“Haki za washitakiwa hawa zinavunjwa wazi wazi na maofisa wa Vyuo vya Mafunzo na serikali kwa ujumla, hawa raia kama raia wengine wanapaswa kupatiwa haki zao zote za msingi wanazostahiki kwani hapo ni watuhumiwa lakini wanafanywa kama wameshatiwa hatiani Mheshimiwa”, alidai Wakili Salum Taufiq.
Wakili Tawfik aliiomba mahakama pamoja na serikali ya kishenzi kuacha kuvunja sheria na haki za watuhumiwa hao kwa sababu ni miongoni mwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu na mahakama haipaswi kunyamazia ukiukwaji huo unaotendeka dhidi ya watuhumiwa.
“Mheshimiwa wateja wetu hawana fursa ya kusali sala ya Ijumaa SHEIN hata ijumaa basi..? na wenzao, hawana vitabu vya dini wakati tunafahamu hawa ni viongozi wa dini, hata ndevu wamenyolewa ili kuwadhalilisha na wamefanyiwa kwa makusudi ili kuwavunjia heshima zao katika jamii wakati ni kinyume na katiba kwani kama tunavyofahamu kufuga ndevu kwa muislamu ni sunna na ni ibada lakini kumnyoa ndevu muilslamu ni sawa na mkristo kumvua msalaba”, alisema mahakamani hapo Wakili huyo.
mazingira waliyo nayo Sheikh Farid na Wenzake huko Rumande imekuwa mbaya na itazidi kuwa mbaya tuna towa wito wa jamii ya waislamu na Wazanzibari kuchukuwa hatua inayofaa kusaidia hali hiyo kabla haijawa mbaya zaidi. Kwa bahati nzuri au mbaya.watu zanzibar bado wanafikiri mawakili ndio watakao waokowa mamiri wetu tumesahau kuwa hii si serekali yetu mbali ni watumwa wa mtwanamkoloni mweusi. Kwa sisi tulio nje kama raia huru,kila siku tunaona kama siku moja huona zinaenda mbio sana kiasi ambacho masaa 24 huwa tunaomba yaongezwe japo kidogo ili tumalize mahangaiko yetu. Lakini hali haiko hivyo kwa ndugu zetu wote walio vifungoni na vizuizini kama Sheikh Azzan na wenzake. Naamini siku moja wanayoitumia kule katika WANTANAMO YA SHEIN kwenye mateso ni mwaka mzima kwao, sembuse mateso wanayoyapata na fikira na mawazo yawapatayo kwa hayo yanayowafika huko. Hili hatulioni sisi tulio nje.
Kuna watu ambao wanaamini kuwa nusura ya Sheikh Mselem na wenzake ya huko waliko itapatikana kwa kupitia mawakili wao akina Tawfik. Kuna ndugu zangu wanaoamini kuwa nusura au shufaa ya viongozi hao itapatikana kwa kuripoti katika mashirika ya kutetea haki za binaadamu, pia wako wanaotaka tuombe msaada kwa mataifa mengine ili kuwasaidia kutokana na mateso na madhila waliyo nayo huko ndani ya WANTANAMO YA SHEIN.
Kwa maoni yangu wanaoamini dhana hizo hapo juu wote wanatwanga maji. Na ikiwa msamiati huu haufahamiki nasema wanaota wakiwa macho, kwani yote matatu hayo hayatawezekana kimsingi. Kuna watakaosema hakuna lisilowezekana, mie nasema kwa binadamu liko. Ni kwa mungu tu kusikoshindikana kitu na hamujamtaja kama ni sehemu ya nusura ya Masheikh wetu.
Nasema hoja ya wanaotegemea kupata haki kwa kupitia mawakili akina Salim Tawfik, wamekosea sana na wanaoamini vyengine kwani nina sababu za msingi zinazo nifanya niseme hivi kwaza mafanikio ya juhudi zote za kuwaombea msamaha na shufaa ya mateso waliyonayo.
Kwanza tujue kuwa kesi ya Sheikh Farid inahusishwa na mambo mawili magumu. Moja ni gumu kwa duniani sasa, na la pili ni gumu kwa Tanganyika na kanisa pekee.Tuanze na gumu la dunia nzima, ifahamike Ustadh Farid wameripotiwa kuwa ni kikundi cha waislamu wanaochochea Zanzibar, kufanya fujo, kulipua makanisa na wamefikia kufananishwa na Boko Haram, Al shabab na wengineo wanaohusika na ugaidi.
Kwa dunia ya leo ukitajwa kwa tuhuma za jambo hili, sema baaasi! Huna tena Kinga ya ‘Amnesty’, ‘Human Right watch’ wala mataifa ya magharibi ambayo wenzangu waliyategemea yaambiwe. Pia huna wakala wala wakili wa kukusaidia. Na hivi ndivyo kesi ya Ustadh Farid ilivyoripotiwa na kuenezwa huko duniani.
Ubalozi kama wa Uingereza na marekani wangekuwa washalisemea suali hili lakini kwa vile lina mfungamano na uisilamu na kuvunjiwa makanisa yao, hawa hawana msaada tena kwa hapo. Ndio nikasema wanaowasubiri hawa waje wasaidie waamke, wakapige mswaki waje wanywe chai, wakacheze. Sababu ya pili, ambayo ni kwa Tanganyika na Kanisa tu ni ile kuonekana kuwa ni tishio kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao unayumba sana kwa sasa. Hakuna asiejuwa kuwa watu wa Bara wa Muungano wako tayari kumuuwa mzanzibari yoyote anayetishia kuwatilia kitumbua chao mchanga.
Mtu yoyote anayetishia kuuvunja muungano kwa njia yoyote lazima asahaulike na hata akipona basi hataweza kufanya lolote. Na hii iko wazi kwani ieleweke kuwa Muungano kwa Zanzibar ni kama koloni lao ambalo kuliacha ni kuanguka kukubwa kwani Zanzibar ndio mkono unaowalisha wao, vyereje wakubali kuuukata...?
Hawakubali kwa gharama yoyote na anaesema haya ni uongo atupe wake ukweli. Kwa maana hii uwezo wa akina wakili Tawfik ambao wanasimama zaidi kisheria hauwezi kufanikiwa kwa sababu wenzao hawapo Kisheria kina SHEIN wameingizwa madarakani kimabavu na wengi wa viongozi wa serekali hii ya thulma wako madarakani kimabavu na kiuonevu zaidi ndio maana mukaona SHEIN misikiti ilivyo pingwa mabomu na kunajisiwa na wanawake kuthalilishwa kimya anajuwa akisema tu basi madaraka bye bye. Kwa hali hii nafuta kabisa dhana zote tatu zilizotajwa hapo juu kwani hakuna kitakachowapatia shufaa masheikh wetu.
Masheikh ni waislamu, waislamu si watu mbele ya macho ya dunia ya sasa na hata Serikali yetu hii ya KIKAFIRI. Sasa kuna kipi? Nilitaja siku za nyuma kuwa hali waliyonayo Masheikh kule Rumande hatuijui lakini sio ya kuridhisha. Sasa yamefichuka. Fikiria binaadamu anawekwa chumba kidogo peke yake kwa masaa 24 kwa muda wa wiki tatu, anakuwaje? Fikiria binadamu asiebadilisha nguo wala kuoga kwa wiki tatu hunuka harufu gani..? Fikiria binadamu anaelala chini katika nchi ya joto kama hii yetu yenye mbuu na kunguni wengi huwaje..?
Vuta tena fikira ya mtu hamsa sawalawati aliekuwa hajapata kuacha sala, wala kusoma Quran leo SHEIN anasema wasiruhusiwe kuswali wala kusoma QURAAN bado haijatosha hawana hata ruhusa kuto kuonana na familia zao je watakuwaje..? Hii ni Ishara mbaya. Kuna mengi yanakuja hapa. Na labda nirukie kitu chengine. Umeona kuwa fujo za siku aliyokamatwa ustaadh Farid hazikutokana na wafuasi wa uamsho ule ulikuwa ni mpango maalum wa SHEIN na MAKUNDI YAKE YA UHARAMIA tu wa kukamlisha haya wayatakayo.
Nasema hivi kwa sababu mbona Ustadh walipokamatwa na mateso wanayofanyiwa sasa hakuna alieandamana...?Pia baada ya kukamatwa maustadhi hawa mbona uharamia unaendele watu kuingiliwa majumbani wakipingwa na kuibiwa na kuharibiwa watoto wao wa kike na kufedheheshwa mbele za watu au mtu kuulizwa kuchanguwa vespa yake au mke wake na mengine mengi mbona bado yanaendelea kufanywa na uamsho washatiwa ndani ya WANTANAMO na huku nje ndio kwanza na MSHENZI SHEIN KIMYAAAAAA ndio sasa nasema yale yalio fanywa wakati wa sheikh farid kukamatwa yalikuwa ni mauzauza ya kupata uhalali wa kuwatesa hawa watu bure na kuendelea kuwatesa wazanzibari ili wakubali kutawaliwa na mkoloni mweusi Tanganyika na kuikubali katiba ya mkoloni mweusi hapa zanzibar ili zanzibar iwe sio nchi tena kama walivyovileta vitambulisho vya kitanganyika ili kuvizima vitambulisho vya kizanzibari na kwali wameanza kufanikiwa.
Ukweli wa hatma ya watu hawa ni kwamba Ustadh Mussa na Wenzake hawakusudiwi kuachiwa tena. Na watakaa huko miaka iwapo hali ya nchi itakuwa kimya kama ilivyo. Kesi zao zitapigwa tarehe mpaka 2015. Alie na vidonda vya tumbo atakufa. Alie mzima atakuwa mgonjwa bin tabani na kwa maana hio hapana atakaetoka akaweza kufanya tena kitu hasa ukichukulia mateso haya waliyonayo hivi sasa kabla hawajahukumiwa jiulize wewe mzanzibari je wakihukumiwa itakuwaje..?
Na ukimya wetu ndio unawapa nguvu wao hawa vitumwa wa mkoloni mweusi na wakoloni pia wanapata nguvu zaidi yakutumaliza kwani wanajua kuwa tumekwisha na kwa hivyo watajipigia wanavyotaka. Na mwsiho wa siku juhudi zetu zitakuwa zimefikishwa tamati bila mafanikio. Kama tumeridhika na haya, na bado tunamsubiri wakili, ubalozi na mataifa yawaombee Masheikh wetu ,viongozi wetu,wakombozi wetu basi tuendelee kusubiri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment