Wednesday, September 2, 2015

KUNA MKAKATI UNAANDALIWA NA CCM KUWAVALISHA VIJANA WAO NGUO ZA CHADEMA ILI WAANDAMANE.


Mkakati waandaliwa: CCM kuwavalisha vijana wao nguo za CHADEMA ili waandamane
Wakuu,
Taarifa iliyo rasmi kutoka kwenye mkakati wa CCM unaoratibiwa na vigogo kadhaa wa CCM wanaoongozwa na Didas Masaburi, Wilbrod Slaa, Harison Mwakyembe unaandaa maandamano ambayo polisi tayari wameshatoa kibali katika jiji la Dar Es Salaam.

Kikao kilichokaa jana usiku baada ya press ya Slaa na response ya Tanzania kumpinga Lowassa kukwama, kimefikia kuandaa maandamano ili kuwaaminisha wananchi na kujenga imani yao kwa CCM.
Taarifa zinasema vijana wa CCM watavalishwa nguo za CHADEMA, wataandamana wakimwunga mkono Slaa na kumpinga Lowassa, inasemekana maandamano hayo yataishia Ikulu kwa mapokezi ya mkubwa.
Taarifa zinatanabaisha Didas Masaburi amesikika akisema haya ni maagizo ya Ikulu kuhakikisha maandamano hayo yanafanikiwa ili kuweza kuwaaminisha Watanzania kuwa Slaa alikuwa sahihi.
Kikao kilihudhuriwa na
- Wilbrod Slaa
- Harrison Mwakyembe
- Didas Masaburi
- Watumishi wa kitengo cha usalama
Tunaendelea kufuatilia kwa kila hatua hii movie.....

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment