Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambae pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Siku moja baada ya Rais wa nchi ya Tanganyika Jakaya Kikwete kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amtaje mhusika wa sakata la Richmond anayezunguka naye kwenye kampeni, Mbunge huyo wa Singida Mashariki ameibuka na kusema kuwa Rais huyo ndiye mhusika wa sakata la Richmond kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na kuwawajibisha mawaziri. Juzi, akiwa Kigoma, Rais wa nchi ya Tanganyika Kikwete alieleza kumshangaa Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mtu huyo anazunguka naye kwenye mikutano ya kampeni na kumtaka amtaje la sivyo yeye (Rais Kikwete), atamtaja. Akihutubia mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, mwanasheria hiyo alianza kwa kusema: “Sasa ndugu zangu naomba leo nimjibu Kikwete na tumalizane na hii habari ya Richmond. Alisema mkuu huyo wa nchi ndiye mhusika kutokana na mamlaka yake na; “si ya huyu Lowassa anayedai natembea naye kwenye kampeni. Hapa kwenye mkono wangu nina taarifa ya mwaka 2008 ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, sasa ni miaka zaidi ya saba tangu isomwe bungeni.”
Lissu aliyekuwa akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege, alinukuu maelezo ya taarifa ya Mwakyembe kifungu kwa kifungu na kueleza namna ambavyo taarifa hiyo haikuweza kumtia hatiani Lowasa, bali aliwajibika kutokana na makosa ya watendaji wake. Baada ya kueleza kwa kina taarifa hiyo, Mwanasheria huyo alisema Rais Kikwete ndiye pekee mwenye mamlaka ya kuwateua mawaziri, akisema alimteua Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha na ndiye mwenye mamlaka ya kuwawajibisha. Karamagi na Dk Msabaha walikuwa wameshika uwaziri wa Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa sakata la Richmond na walijiuzulu pamoja Lowassa. “Waziri mkuu Lowassa baada ya kutokea kwa sakata hilo alimwendea Rais Kikwete na kumweleza kuwa ‘kimenuka’ tuvunje mkataba baada ya wabunge wa upinzani kuchachamaa kuhusu sakata hilo, lakini alikataa na kumweleza kuwa hizo kelele za wapinzani zitaisha tu,” alisema. Alisema baada ya Lowassa kujiuzulu mwaka 2008, tayari mashine za kutengeneza umeme zilishafika nchini na baada ya kujiuzulu haikufahamika zilikokwenda na kwamba baadaye mkataba wa Richmond ukahamishiwa kwa kampuni ya Dowans ambayo iliendelea kulipwa mabilioni ya shilingi.
Alimtaka Rais Kiwete awaambie Watanganyika ((Watanzania)) Wazanzibari kwa nini Serikali yake iliendelea kuilipa Dowans mabilioni ambayo ilikuwa ya mfukoni na kwamba kama Lowassa alifanya makosa kwa nini hajapelekwa mahakamani kwa miaka minane tangu ajiuzulu. “Rais Kikwete asitake kumaliza hizi siku chache za kampeni zilizobaki kwa shari na mimi na naomba niwaambie, Lowassa amefanya kazi katika umri wake wote wa miaka 62 ndani ya CCM na Serikali yake, lakini ameamua kuhamia huku kwa ajili ya kuleta mabadiliko na kuacha marupurupu yake yote,” alisema Lissu.
Aliposimama kuhutubia mkutano huo, Lowassa hakugusia kabisa suala hilo la Richmond na badala yake akaahidi iwapo atachaguliwa, serikali yake itafanya kila linalowezekana kuanzisha benki maalumu ya maendeleo kwaa ajili ya mama na baba lishe, vijana wa bodaboda na wamachinga ambao alisema watakuwa ni marafiki wakubwa wa serikali yake. Alieleza kufurahishwa na umati huo akisema umemkumbusha siku alipowasili mkoani hapa kutafuta wadhamini, kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM. Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye aliwataka wananchi kutobabaishwa na vitisho vinavyotolewa na viongozi wa CCM kuwa upinzani ukiingia Ikulu kutakuwa na machafuko. Alisema serikali ya Ukawa ikiingia madarakani itahakikisha inasimamia mambo iliyoyaainisha kwenye ilani ya uchaguzi, tofauti na serikali ya CCM ambayo mbali na kuahidi maisha bora na kukusanya kodi za wananchi, bado hali imeendelea kuwa mbaya siku hadi siku. Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Morogoro Mjini, Albanie Marcos aliahidi kusimamia viwanda mjini hapa vikiwamo vilivyobadilishwa matumizi, kurudi kuwa chini ya wananchi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo Bisimba alisema hilo siyo suala la Rais Kikwete kumuagiza Lissu, bali alitakiwa afanye mwenyewe kwa sababu anayo haki ya kufanya hivyo. “Rais kupitia vyombo husika ndiyo anatakiwa atoe amri mhusika achukuliwe hatua kama anamfahamu, ana kila sababu ya kufanya hivyo, kama alikaa kimya wakati huo, wakati huu haitasaidia?” alisema Bisimba. Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi alisema kujadili suala hilo sasa ni kuwanyima wananchi uhuru wa kujadili mambo ya msingi yenye tija kwa Taifa.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.
No comments:
Post a Comment