Wednesday, September 23, 2015

NCHINI ZANZIBAR SHEIN AHIDI KUJENGA KIWANDA CHA KUSINDIKA SAMAKI NA KUWANUNULIA BOTI ZA KSASA WAVUVI AKICHANGULIWA KUWA RAISI.((MIAKA 5 UMEKA MADARAKANI UMEJENGA MNARA KWA NINI HUKUJENGA HICHO KIWANDA...??))Mgombea urais wa nchi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Shein, ameahidi kuwa akichaguliwa kuwa rais wa nchi ya Zanzibar serikali yake itajenga kiwanda cha kisasa cha kusindika samaki kwenye makopo na kuwapatia wavuvi boti za kisasa zitakazowasaidia kuvua samaki wakubwa.((miaka mitano umekuwa rais hilo hukulifikiria akafikiria kujenga mnara.)) Alitoa ahadi hiyo katika viwanja vya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba jana ikiwa ni mwendelezo wa kampeni zake kisiwani humu.
Dk. Shein alisema katika visiwa vya Unguja na Pemba nchini Zanzibar, kuna zaidi ya wavuvi 6,000 pamoja na vikundi vidogo vidogo vya wavuvi 157 wanaovua samaki kwa kutumia mbinu duni. Alisema kuwa ili kuboresha sekta hiyo, ameshaanza kufanya mazungumzo na kampuni mojawapo kutoka nchi ya Sri Lanka itakayokuja Zanzibar kujenga kiwanda cha kusindika samaki kwenye makopo. Alisema mazungumzo baina ya kampuni hiyo yameshakamilika na kilichobaki sasa ni kuanza utekelezaji wa kujenga kiwanda hicho. 
Kadhalika Dk. Shein alisema mbali na kampuni hiyo kuja kuwekeza nchini, pia itaendeleza uvuvi Pemba kwa kutengeneza boti nyingi zaidi za mita tisa ili zisaidie katika shughuli za uvuvi. Dk. Shein alifafanua kuwa lengo la kuingia mkataba na kampuni hiyo ni kuwawezesha wavuvi kuvua kwa kisasa. Aidha Dk. Shein aliwahakikishia wakazi wa Micheweni Pemba kunakuwapo na miundombinu bora ya maji. Pia alisema atahakikisha huduma ya umeme inakuwa ya uhakika kwa wakazi wa Zanzibar kwa kupeleka umeme katika vijiji 129 ambavyo kwa sasa havina umeme.
KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment