Saturday, September 19, 2015

NCHINI ZANZIBAR SHEIN NA CHAMA CHAKE CHA CCM AENDELEA NA KAMPENI KISIWANI PEMBA


Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar Shein, akiwasalimia Wananchi waliofika katika uwanja wa kunde kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Shein.wakati akiwasili katika viwanja hivyo vya mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad akiwahutubia na kutoa Sere za CCM zilivotelekezwa na kuiletea Maendeleo nchi ya Zanzibar katika kipindi chake Shein cha miaka mitano na kuwataka kumpa kura kwa mara ya pili kuendeleza mafanikio ya Maendeleo Zanzibar katika sekta mbalimbali za Jamii 


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Shein akiwana na Viongozi wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba ikiwa ni mkutano wake wa tatu kisiwani Pemba akiwa katika kampeni zake.


Viongozi wa Jukwaa kuu wakimsikiliza Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar Shein, wakati akiwahutubia Wananchi wa Konde Pemba Wilaya ya Micheweni akiwa katika mikutano yake ya kampeni kisiwani Pemba.

Wazee wa CCM Wilaya ya Micheweni wakiwa katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Urais wa nchi ya Zanzibar wakimsikiliza Shein wakati akiwahutubia na kutowa Sera za CCM kwa wananchi wakati wa mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Wananchi wakishangilia wakati wa kuwatambulisha wagombea Ubunge na Uwakilishi na Udiwani wa Wilaya ya Micheweni Pemba.


Mgombea Urais wa nchi ya Zanzibar Shein, akiondoka viwanja vya Konde Pemba baada ya kumaliza mkutano wake wa tatu wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde Pemba, akiongozana na Viongozi wa CCM wenzake. 

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment