Thursday, February 16, 2012

HR,TIBAIJUKA,SHAMHUNA,BILALI,SAMIA NYAMBIZI,KUFUTWA KWA MITIHANI NA SASA LA UZINI HIZI ZOTE NI MBINU ZA MKOLONI MWEUSI ILI WAZENJI WASAHAU KUDAI NCHI YAO NA KUSHUGHULIKIA MAMBO MADOGO MADOGO YA KIPUMBAVU WAZANZIBAR AMKENI AMKENI

MIMI SITAKI KUWA KAMA HUYU KAKA ZETU ZANZIBAR INUKENI MUIHAMI NCHI YETU ILI NIENDELE KUWA KAMA NILIVYO INUKENI KAKA ZETU NA BABA ZETU MUIKOMBOE NCHI YETU YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR
WEZENJI TUNASUBIRI MPAKA DADA ZETU NA WAKE
ZETU WAFANYWE KAMA HIVI NDIO TUPIGANIYE NCHI YETU..?
Imetolewa na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa – Zanzibar
TUMEJIFUNGIA na WAZEE na tumekaa tukanong’ona ! Kwanza Serikali ya Tanganyika walituletea sakata la Hamad Rashid, na watu wakalivamia. Ikawa mwezi na nusu Wazanzibari hatujadili tena kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Baadae likaja suala la kuongezwa kwa mipaka ya bahari kuu la Tibaijuka na Shamhuna. Akina Bilali, Samia Suluhu na wenziwao tutajuwana nao BAADA ya kuiweka mezani JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Pia kwa makusudi, wamelizusha suala la kufutwa kwa mitihani ya kidato cha nne. Tunalopaswa kufanya ni kuhakikisha Waziri wa Elimu wa Zanzibar, anatoa ripoti juu ya kufutwa kwa mitihani ya kidato cha nne, pamoja na kutueleza kwa kina mfumo wa mzima wa elimu duni uliopo Zanzibar.
Hivi sasa limezuka suala la uchaguzi mdogo wa Uzini na Chadema kuchukua nafasi ya pili baada ya kuwanunua wapiga kura mamluki. Tujue kwamba, Tanganyika iliyojificha ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitosita na haitolala mpaka tuifuate MILA yao ya kuijadili Katiba ya Muungano KWANZA bila ya kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Tukiyafuata waliyoyakusudia na wanayoyapanga, tutakuwa tumetoka nje ya kuidai HAKI yetu ya kimsingi ya kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Hamad Rashid, Bilali, kufutwa kwa mitihani na uchaguzi wa Uzini, zote hizi ni mbinu,kama ile ya popo bawa kama munakubuka na huu ni ujanja na fitina za kutuondoa kwenye lengo KUU la kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Kamwe hatutaicheza ngoma yao!
Zamani ilikuwa ni UHAINI kujadili Muungano. Juzi tu, wajanja hawa hawa kwa kutaka kuiendeleza falsafa hiyo yao YAUJINAMIZI NYERERE, wamepitisha sheria Bungeni ya kumchukulia hatua yo yote atakaejadili lo lote ambalo liko nje ya hadudi rejea za rasimu ya Katiba. Kwa mantiki hiyo, yo yote atakaetoa NGUVU ya HOJA ya kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA na/au Muungano wa Mkataba na kuukataa Muungano wa Katiba wakati wa mchakato wa Katiba utakapokuja, atachukuliwa hatua za kisheria kwa kufikishwa Mahakamani, ili wengine waogope kuendelea kuidai JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR, na badala yake iendelezwe HOJA ya NGUVU na ya UDIKTETAA inayotakiwa ya kujadili Katiba iliyosimama juu ya misingi ya KIKOLONI inayopinga uwepo wa JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR ambayo ndio mbia mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hizo zinazodaiwa kuwa ni hati za Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zilijengwa juu ya taswira ya Muungano baina ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini ya wakati ule, pale Ireland ya Kaskazini ilipokuwa ni koloni la Uingereza.
Kudhihirisha njama za wajanja hawa, juzi tarehe 12 Februari 2012, Halmashauri Kuu ya CCM kwa makusudi, imeifanyia marekebisho Katiba ya CCM yenye lengo la kuwaangusha na kuwadhibiti – MASHUJAA wa MARIDHIANO yetu yaliyo HALALI Kikatiba, na badala yake, kuwabeba VIBARAKA ambao wameonesha wako tayari kuiuza Zanzibar na Wazanzibari kwa UTASHI wa UBINAFSI unaoongozwa na uroho na ulafi wa madaraka.
WAZANZIBARI po pote tulipo duniani TUMESHA AMKAA na KUSIMAMA KIDETE kwa kuelewa kuwa, yote haya ni katika mbinu chafu, hadaa, ghilba na fitina za kutuondoa kwenye lengo KUU la kuipigania na kuirudisha JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR. Tusikubali, na kwa hakika HATUTAKUBALI kuondolewa kwenye njia na lengo letu hilo HALALI la kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye hadhi yake kitaifa na kimataifa; maana sisi wananchi wa Zanzibar, tuna mamlaka na haki ya Kikatiba katika kuendesha nchi yetu kama Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inavyoeleza kwenye Sura ya Pili: (a) “Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe”.
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA! SIO KISHEIN,IDDI AMINI DADA WALA MWENGINE YOYOTE YULE ZANZIBAR LAZIMA IWE NCHI HURU KAMA ILIVYOKUWA HAPO AWALI HAKUNA HILI WALA LILE.

No comments:

Post a Comment