HUYU NI IDDI AMIN DADA
NA HUYU NI IDDI AMINI DADA
JE WANANCHI WA ZANZIBAR MUMELEWA....?
“WAWAKILISHI WAKO SOLIDARITY SIO CCM AU CUF, TUWAGAWE TUWATAWALE” THAT IS VP2 SEIF IDDInasikitisha kwa mara nyengine tena kiongozi aliyechaguliwa kuitetea na kuikomboa Zanzibar kutoka kwa huu Muungano FEKI usiokuwa halali, anafika kusema nirahisishieni kazi kwani Wawakilishi hivi sasa wako Solidarity sio CCM au CUF katika masuala ya Muungano.
Hapa kweli tunakiongozi au KABURU ambaye anadhirisha wazi kwamba lengo ni kuona Wawakilishi wa CCM na CUF wanatafautiana katika kuitetea Zanzibar kwenye huu Muungano wa Watanganyika waliojivika koti la ((Tanzania)).
Kiongozi wa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar anasema maneno ambayo msingi wake mkubwa ni kuwagawa Wawakilishi hivi kweli tutafika na mtu tapeli kama huyu JI KABURU KUBWA.
Yeye na wengine malengo ni kuhakikisha Raslimali zote za Zanzibar zinakuwa mikononi mwa Watanganyika na ndio maana anawaogopa Wawakilishi kwa kauli yake hii ya tuwagawe na tuwatawale..
Kwa taarifa yako Mzee umekwenda mrama lengo na dhamira yenu imeshajulikana na Wazanzibar kwa kupitia Wawakilishi wao wako kitu kimoja na moto umeshawaka hakuna wa kuuzima.
Huyu VP2 anatakiwa aitwe kwenye Baraza la Wawakilishi na kijueleza kwanini haheshimu maamuzi ya Bazara la wawakilishi, Mafuta na Gesi tayari yameshaondolewa kwenye mjadala, kitu gani kinachoendelea kuzungumzwa na Serikali ya Mapinduzi kwenye hivi vikao vya Watanganyika.
Hii inadhirisha wazi kwamba huyu Balozi Iddy Amini DADA ni miongoni mwa kundi la Shamuhuna kutokuheshimu maamuzi ya Baraza la Wawakilishi.na kama hawaheshimu basi dawa nikulazimishwa kujiuzulu kama alivyo ambiwa shamhuna ajiuzulu maana wao wanaona vyeo walivyo navyo basi zanzibar imekuwa kama nyumba ya marehe baba zao na wao ni kaka wakubwa watafanya watakalo sio hii ni nchi sio nyumba.
Kimtazamo wangu anatakiwa apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye na kushindwa kusimamia mamuzi ya vikao vya baraza la wawakilishi kwa hiyo ajiuzulu.
Anafanya mambo kwa matakwa ya Watanganyika na pia huyu Makamo wa Rais Gharib Bilali anatakiwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye ndio itakuwa mwisho wake na asiruhusiwe tena kukanyanga zanzibar kama ilivyo katazwa JOHN OKELLO kuto kukanyanga tenza zanzibar na huyu afanyiwe hivyo hivyo.Wakati ndio huu, wajumbe tayarisheni hoja ya dharura kuiwasilisha barazani kuwaondoa hawa jamaa sio wenye kuitetea Zanzibar.
Mungu ibariki Zanzibar na watu wake
No comments:
Post a Comment