Wednesday, February 1, 2012

MKAPA ATAFIKISHWA LINI (( ICC )) THE HAGUE NCHINI UHOLANZI KUELEZEYA NI KWANINI ALIWAULISHA DUNGU ZETU UNGUJA NA PEMBA...?

HUYU NDIYE ALIYE WAULISHA NDUGU ZETU
UNGUJA NA PEMBA JANUARI 27,2001
HIVI karibuni Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) imewatia hatiani watuhumiwa wanne kati ya sita waliofikishwa katika mahakama hiyo, hivyo watakabiliwa na kesi ya mauaji na vurugu za Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwaka 2007.
Watuhumiwa hao wamekutwa na hatia mjini The Hague, Uholanzi baada ya jopo la majaji chini ya uongozi wa Jaji, Ekaterina Trendafilova kuwasilisha uamuzi wao kwa watuhumiwa baada ya maelezo ya awali ya pande zote.
Wakati hayo yakitokea Kenya, hapa Tanzania Chama cha Wananchi CUF kimeadhimisha miaka 11 tangu yatokee mauaji na mateso kwa viongozi na wanachama wake baada ya kufanya maandamano makubwa katika miji ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba ili kupinga matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2000.
Maandamano hayo yaliyofanyika Januari 27, 2001 yalikabiliwa na polisi na kusababisha vifo na majeruhi. Hadi sasa idadi ya vifo inayotajwa na serikali ni watu 34, lakini kuna madai kuwa waliokufa ni wengi zaidi ya hao. Wengine walipoteza mali zao na mbaya zaidi, Tanzania ilizalisha wakimbizi baada ya baadhi ya wananchi kutoka kisiwani Pemba kukimbilia Mombasa.
Kutokana na tukio hilo wapo baadhi ya Watanzania wanafikiria kuishitaki serikali ya Tanzania ICC kama ilivyofanyika kwa Kenya.
Kwa sasa tunakusanya ushahidi ikiwa ni pamoja na kuwahusisha viongozi waliokuwepo kama vile aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Seif Khatib na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Omar Mahita. Vielelezo vitakapo kamilika tutapeleka kesi mahakamani anasema mmoja wa Watanzania ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini ili kulinda ushahidi wake.
Hata hivyo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Haki za binadamu ndani ya CUF Salum Bimani anasema kuwa chama chake kinasubiri maamuzi ya Bunge ili kuhakikisha kuwa madhila yaliyowapata wanachama na viongozi wake yanapatiwa ufumbuzi.
Kwa sasa tunasubiri maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, kwasababu tuliahidiwa kuwa suala hilo litajadiliwa na litapatiwa ufumbuzi anasema Bimani.
Akizungumzia suala la kuishitaki serikali ICC, Bimani anasema kwa sasa chama chake hakina mpango huo, ila kama kuna watu watajitokeza kufanya hivyo chama kitawaunga mkono.
Kwa sasa hatuna mpango huo, lakini kama kuna watu wamejitokeza kushitaki, sisi tutawaunga mkono katika hilo.pia kuna moja wa vijana ambae hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa mdogo wake alipingwa risasi kwenye mlango wao haswa huko pemba.nasama hivi viongozi kama hawa lazima washughulikiwe na kuhukumiwa ndio nchi hii itasonga mbele kimaendeleo la kama hawa wakifanya ni hewala bwana kama fanya na mnyonge akafanya anapandishwa mahakamani basi hatuna nchi sisi hapa.kwa hiyo viongozi wote waliokuwa madarakani wakati ule wajieleze moja baada ya mwengine mpaka tupate joka kubwa tuliuwe ndio tutaendeleya laa sivyo itakuwa kama tunachezo mdako au bao tu asante sana.hapa ndipo alipo malizia kusema na mpaka sasa watu wengi sana wana taka mamba haya yawekwe wazi ili familia na dungu na jamaa walio uliwa dungu zao wao kuwa serekali haichanguwi wala haibaguwi je yatafanywa haya.....? na serekali hii ya viraka....?

No comments:

Post a Comment