Friday, February 3, 2012

UMASIKINI NCHINI ZANZIBAR UNAZIDI KUONGEZEKA NA MAPINDUZI DAIMA YANAZIDI KUTAJIRIKA WAZENJI MPOO AU MUME LALA FOFOFO....?


kuna tafauti gani kati ya zanzibar 1888 na hii zanzibar ya leo ya 2012..?
huyu ni mzizi na ana watoto hao wanne na wote kawapakia ktk baskili anawapeleka skuli na kila siku kwenye vyombo vya habari utasikia oooh mapinduzi daima ni kuja kuondowa umasiki je umasikini huwo munaouzungumza ni umasikini gani haswa...? wawananchi.. au wamatumbo yenu nyinyi viongozi wa zanzibar..? ikiwa ni wawananchi basi toka 1964 mpaka leo 2012 hakuna moja lililofanyika la maana zaidi ya kuwa na viongozi wengi ndani ya baraza la wawakilishi na maraisi watatu na wabunge kibao.lakini mwananchi maisha yake yako pale pale na kila kukicha ndio yanazidi kuporomoka.lakini ikiwa munazungumza kuhusu umaskini wenu nyinyi viongozi basi sawa hamuna tena umasikini maana hakuna hata mtoto wenu moja anapelekwa skuli na basikili kama hivi au yuko....? je mapinduzi ni ya wananchi au ni ya nyinyi viongozi kuwapinduwa wananchi na kuwawacha katika hali ya umasikini..?nitaweka hapa picha za magari yenu ili tuone kama kweli nyinyi munawajali wananchi au ni matumbo yenu na famili zenu tu.
zanzibar nchi masikini ila kila baada ya miaka mitano ukimalizika uchanguzi tu viongozi wanapata magari kama haya au kuliko haya wananchi wanapata nini wakati wa kampeni taraabu na utenzi na ubale wa kanga na panga au shoka je huo umapinduzi wenu wakuja kuwaondoleya watu umasikini ndio huu...?
HIVI NI MILLIONI NGAPI KUCHONGESHA DESK MOJA..?
NA NI ELFU NGAPI KUNUNUWA MAGARI YENU NYINYI VIONGOZI WA ZANZIBAR..?
MAPINDUZI DAIMA....MAPINDUZI DAIMA....MAPINDUZI DAIMA
ILA KWA VIONGIZI TU RAI KULENI MIHOGO MIKAVU NA MASHELISHELI MPAKA MUZIBE CHOO KWA MIHIGO MINGI

No comments:

Post a Comment