Wednesday, November 6, 2013

ATI NCHI YA ZANZIBAR YAONGEZA MISHAHARA KWA WAWAKILISHI RAI TWAENDELEA KUFANYWA MAZOMBI

VIONGOZI WA NCHI YA ZANZIBAR SIO MAZOMBI BALI MAZOMBI NI SISI RAI WA ZANZIBAR TUNAO WACHAGUWA VIONGOZI HAO HAO KILA BAADA YA MIAKA KUMI HATA KAMA NI JIZI, JIUWAJI,LIMETUVUNJIA NYUMBA AU VIBADA VYETU VYA KUTAFUTA RIZIKI, LINATHULUMU MUDA UKIJA TU TUNALITILIA KURA LIBE VIZURI TENA NA TENA SASA UTAMWITA ZOMBI KWELI HATA MAZOMBI NI SISI RAI.
1. Wawakilishi wamepewa nyongeza ya 750,000/= na ushei
2. Walimu 25,000/= minus Ushei
Ukiachilia yote yanayofanywa na serikali yetu — kutimua timua dala dala pale Darajani, kuvunja nyumba za watu Bububu/Mwanyanya n.k — kupandisha bei ya umeme kwa asilimia zaidi ya 80% kuanzia Novemba 1/2013 — sasa SMZ SEREKALI YA MATHALIMU NA MAJIZI YASIOKUWA NA HARUMA NA RAI WAKE  imekuja na MPYA:
1. Imegeza mishahara ya ‘wafanyakazi’ wa SMZ wote. Wajumbe wa Baraza la wawakilishi watalipwa laki saba na nusu.
2. walimu wamepewa nyongeza ya 25,000/= kama una Phd kama huna; kama umesomesha miaka mitatu, kumi, 20, mmoja n.k katika mfumo kama huo. Almuradi serikali yetu imejaa ‘big thinkers’.
Nimekupeni picha halisi, sitaki kwenda sana katika details – mjue tu kuwa hiyo ndio nyongeza au SMZ wanaita ‘marekebeisho ya mishahara’.Marekebisho haya sio kwa wananchi wavuja jesho bali viongozi na wake zao na watoto wao hii nchi ya Zanzibar sio nchi ya wananchi bali ni nchi ya Viongozi na wake zao na watoto wao basi.
Kuna nyongeza ya siri kwa wakurugenzi na makatibu wakuu, sijui ngapi — maana ndio siri tena, almuradi wamevuna chao sihaba.
Wachunguzi wa mambo — hao hao waajiriwa wanasema kuwa kama hesabu ziko sawa, wao wangaliweza kuongezwa kama 100,000/ kutoka ama kiasa ya wajumbe wa BLW au hao wakurugenzi na pesa itabaki nyingi kwao.
Kuna walimu wamesomesha hao viongozi wa leo, na bado mshahara wao ni 100,000/ au laki moja unusu — wengine ni Master Degree, wengine na PHD holder, na wengine ni graduate lakini katika specialization fulani.
priority ni kujenga mnara wa kutimiza miaka 50 ya mapinduzi, upumbavu mtupu mnara wa mapinduzi tunafurahia kuuwa watu,kunajisi wake zawatu na watoto wa kike,kuowa watoto wawatu kwa lazima,kuwanyowa watu ndevu kwa vigae,kupiga watu mikwaju unguja na pemba,kunyanganya watu mashamba yao na kuyakata heka .
Haramu juu ya haramu na sasa kwajengwa mnara wa kukumbuka haramu kisha ijumaa misikitini allah akbari yagujuuuu mnara wa mapinduzi wakati  hatuna dawa, wanafunzi wanakaa chini, na ugawaji wa rasilmali [mishahara ndio huo mnauona]. Vichekesho vitupu.leo mlo moja Zanzibar watu wanaupata kwa mbinde astahafiru allah.
Ndio pale nilisema kuwa Zanzibar hatuna wawakilishi. Leo wao wameongezwa mara 100 ya kiwango cha wafanyakazi wengine,tunategemea kweli watasema nini hawa..? wameshatiwa kufuli mdomoni. Nyie wenzangu wengine mtaendelea kupigwa bao tu na hadithi za katiba mpya, kwenda kibanda maiti kucheza ngoma, na mambo kama hayo ama Kidumu Chama Mapinduzi au Haki Sawa kwa Wote. Hiyo Hakiiiiiiiii…………..na hiyo ndio Kidumuuuuuuuuuu…….!
Mimi sioni ajabu sana kuna haya maana mawaziri wetu ni akina Haruna Ali Suleiman, Haji Omar Kheri, Ramadhan Abdullah Shaban, Mohammed Aboud na kama hao — si wa kujua A wala B, wao ‘ulaji tu’ ndio wanaoujua.
 BEI YA UMEME KUANZIA NOVEMBA 1, 2013 IMEPANDA KWA ASILIMIA 80% NA ZAIDI, LAKINI WALIOIBA NA KUHUJUMU MABILIONI WAPO PALE PALE, SASA TUNALIPA SISI WAVUJA JASHO MPAKA MAVI YATUTOKE.MUZA MISHKAKI,BATATA ZA UROJO,MUZA MAZIWA,MUZA CHIPS,DALADALA,MSUKUMA RIKWAMA,MCHUKUZI,MUZA MATOFALI,MBEBA NA MCHIMBAJI MCHANGA N.K. MTALIPA UMEME MPAKA MAVI YAWATOKA SIMUNATAKA UMEME.

No comments:

Post a Comment