Sunday, November 10, 2013

HUTBA YA RAISI WA NCHI YA TANGANYIKA KUHUSU MATATIZO WALIYO NAYO NA EAC JE IMEWATOWA TAKA ZA MASHIKIO NA TONGO ZA MACHO WAHAFIDHINA NA VIBARAKA WA WATANGANYIKA MULIO ZANZIBAR AU NDIO KWANZA MELALA..??


VIONGOZI HAWA NDIO KIBOKO NA MUARUBAINI WA NCHI YA TANGANYIKA SIO VIONGOZI WA NCHI YETU YA ZANZIBAR KILA ASEMALO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA HEWALA BWANA MTANGANYIKA
Yeyote ambaye ni Mzanzibari na anaipenda nchi yake ya Zanzibar aliyefuatilia kwa umakini hotuba ya Rais Jakaya Kikwete raisi wa nchi ya Tanganyika alipohutubia katika Bunge la nchi yake mjini Dodoma juzi, bila shaka atakuwa siyo tu ameshangazwa bali atakuwa na maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu hotuba hiyo, pia jinsi alivyozungumzia masuala mazito kwa kuipambapamba nchi yake ya Tanganyika kuwa ndio nchi nzuri haina ubaya inapenda mashirikiano bla blablabla.
Rais wa nchi ya Tanganyika alizungumzia masuala mengi yanayohusu mustakabali wa Tanganyika na nchi hizo za jirani, lakini hapa tutajielekeza tu kwa maelezo yake kuhusu nafasi ya nchi ya Tanganyika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), bila kuizunguzia nchi ya Zanzibar na nyenginezo. baada ya nchi ya Kenya, Uganda na Rwanda kuendesha mambo ya jumuiya hiyo bila kuihusisha nchi ya Tanganyika na kuiweka nchi ya Tanganyika ubao.
Pamoja na kwamba hotuba hiyo ilikuja ikiwa imechelewa, kwa maana ya watendaji wa Serikali wanaohusika na masuala ya nchi za nje, ikiwamo EAC kuachwa kwa muda mrefu wakitoa kauli tata na danganyifu kuhusu mustakabali wa nchi ya Tanganyika katika jumuiya hiyo, kujitokeza kwa Rais Kikwete juzi watanganyika wengi wamethani kuwa Raisi wao kaweka rekodi sawa kuhusu hali ya baadaye ya nchi yao ya Tanganyika katika jumuiya hiyo. Dhana ilikuwa imejengwa na watendaji hao kuwa, kutokana na nchi ya Tanganyika kutengwa na nchi hizo za EAC, kujiondoa kwa nchi ya Tanganyika katika jumuiya hiyo sasa lilikuwa jambo lisiloepukika.
Hivyo, kujitokeza kwa Rais Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika juzi kulizungumzia suala hilo na kuliwekea msimamo bado kuwa Watanganyika wengi wanadhani kuliondoa wasiwasi uliokuwa umetanda miongoni mwa wananchi wa nchi ya Tanganyika siyo tu hapa nchini Tanganyika, bali pia Watanganyika wanafikiri katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.Pia kuna Watanganyika wengi wanao jidanganya kuwa hakuna asiyejua kwamba nafasi ya nchi ya Tanganyika katika jumuiya hiyo ni kubwa na kwamba kujitoa kwake kutaiachia jumuiya hiyo ombwe ambalo kamwe haliwezi kuzibika nacheka kwanza hahahahahah maana haya ndio wanayojidanganya Watanganyika kila siku kuwa nyinyi Wazanzibari mukijitenga mutakuwa hamupati batata,vitugu,umeme utafikiri wanatupa bure nchi yenu itatikisika cha jabu tukiwambiya vunjeni basi Muungano Feki ili Wazanzibari tuteseka wanaogeza majeshi katika kambi za jeshi za nchi yetu. Kwa upande mwingine, Watanganyika wanajuwa kuwa lazima waungane na nchi nyengine la sivyo wao ndio watakao teseka ndipo walipokuja na usemi kuwa nchi ya Tanganyika tayari imewekeza sana katika jumuiya hiyo, hivyo kujitoa katika mazingira ya sasa ni sawa na kumsusia nguruwe shamba la mahindi.
Ni jambo la kheri kwamba Rais Kikwete ameweka wazi msimamo kwamba nchi ya Tanganyika imo, itaendelea kuwamo na haina mpango wa kujitoa katika jumuiya hiyo kama anavyosema mwenyewe licha ya vitimbwi vinavyofanywa na viongozi wa nchi hizo tatu. Hii ni ishara tosha kuwa nchi ya Tanganyika ndio muhitaji zaidi katika nchi hizo tatu kuliko hizo nchi nyengine maana kama sio muhitaji basi wangelijitoa tu lakini wanajuwa wazi kuwa wao ndio wahitaji zaidi nchi ya Tanganyika ndio maana wamengangania kubaki.hakuna na tafauti yoyote na ila ya nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar wakitaka wasitake nchi ya Tanganyika inahitaji zaidi nchi ya Zanzibar kuliko nchi ya Zanzibar inavyo ihitaji nchi ya Tanaganyika ila huta sikia hata siku moja Watanganyika wakisema hilo siku zote wao ndio wahitajiwa hahahahahaha bora nicheke hahahahaahahah.
Ni hotuba iliyojaa uwazi na kweli kuwa wao hawataki kuamuliwa mambo yao au ya nchi yao ya Tanganyika mpaka waamuwe wenyewe. Sasa tunajua kwamba sababu kubwa ya viongozi hao kuitenga nchi ya Tanganyika ni kuwa wanabadilika kama kinyonga pia kuhusu Raisi wa nchi ya Tanganyika msimamo wake wa kupinga kuharakisha kuundwa kwa shirikisho la kisiasa, hasa katika maeneo ya umiliki wa ardhi, uhamiaji na ajira. Msimamo huo umechukuliwa na nchi hizo tatu kama kikwazo kinachochelewesha maendeleo ya jumuiya hiyo, ingawa nchi ya Tanganyika imekuwa ikisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuheshimu mkataba ulioanzisha jumuiya hiyo.hapa ndipo tunawauliza Watanganyika mbona mnakereka Wazanzibari wakikata na Mafuta yao na Gas..?? mbona mnakereka Wazanzibari wakitaka kurudisha Paspoti zao...??  mbona mnakeraka Wazanzibari wakitaka kujuwa kila Mtanganyika anaikuja Nchini Zanzibar awe na sababu malum sio kuingia na kutoka kama chooni..?? mbona mnakeraka Wazanzibari wakitaka kuanzisha Pesa zao..??  mbona mnakereka tukiwauliza Hati ya Muungano Feki iko wapi ili tujuwe mkataba na mambo tulio ungana..?? n.k  n.k. bora nisite hapa maana ni mengi,
Nataka na nyinyi viongozi wa nchi ya Zanzibar mipumbavu mutowe takataka za mashikio na tongo za macho musikilize na muone anavyo juwa kujiweka katika miungano ya nchi nyengine huku wakiendelea kutukandamiza Wazanzibari amkeni amkeni walevi nyieee.Namnuku Raisi wa nchi ya Tanganyika  Kwa maana hiyo, sisi hatuoni tatizo kama msimamo wa Tanganyika ni kuona jumuiya hiyo ikijengwa hatua kwa hatua kama ilivyoainishwa katika mkataba, badala ya kuruka baadhi ya hatua. Hatua hizo zilizoainishwa katika mkataba ni; Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja, Sarafu ya Pamoja na hatimaye Shirikisho la Kisiasa litakalopatikana baada ya wananchi katika nchi wanachama kupiga kura ya maoni. Hivyo, tunadhani Serikali ya Tanganyika iko sahihi kutounga mkono kuharakisha kuunda Shirikisho la Kisiasa ambalo linapaswa kujengwa juu ya misingi imara ya kiuchumi.
Hoja hapa ni kwamba tukiharakisha Shirikisho la Kisiasa Jumuiya itavunjika, kwani kama alivyosema Rais Kikwete, mambo yanayozua mitafaruku siku zote ni ya uchumi wala siyo ya kisiasa. Bahati nzuri huo pia ndiyo msimamo wa wananchi wa nchi ya Tanganyika.

No comments:

Post a Comment