Saturday, April 4, 2015

GARI LILILOTUMIKA KUFANYA USHENZI,MAUWAJI NA KUWAJERUHI WAZANZIBARI WASIO NA HATIA YOYOTE NI GARI LA BHAA STYLE,SHEIN,BALOZI MKAZI,POLISI WOTE KIMYA WAMEUFYATAA

image
KUSHAMBULIWA KWA WAFUASI WA CHAMA HALALI HAYAKUANZA LEO YANAENDELE NA YATAZIDI KUENDELEA MAANA HIYO NDIO KAZI YA CCM CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA CCM SIO CHAMA CHA WAZANZIBARI NI CHAMA CHA KUJA KUWAUWA WAZANZIBARI KWA NJIA TAFAUTI.:WAZANZIBARI WASHA SUBIRI SANA ILA MKAE MKIJUWA SUBIRI SUBIRI INA MIPAKA.


Katika hali tunayoweza kuiita ya kutisha au kuendelea kuwatisha na kuwajengea hofu kwa Wazanzibari iliyotokana na Uharamia wa kundi linalosadikiwa kuwa la ‘janjaweed’, wafuasi kadhaa wa Chama Cha CUF wameshambuliwa na kujeruhiwa vibaya wakiwa njiani kutokea katika mkutano wao ambao ni halali kufanya huko Makunduchi.
Pamoja na ubaya wa tukio lenyewe, nasema matukio kama haya kutoka kwa makundi yanayosadikiwa kuwa chini ya Chama tawala Chama Cha CCM Chama Cha Mkoloni Mweusi Tanganyika, yamekuwa ya kawaida sana dhidi ya Chama Cha CUF. Tangu chama cha CUF kusajiliwa rasmi mwaka 1992, watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kubakia na ulemavu na makovu yasio futika ya kudumu kutokana na adhabu ya vyombo vya dola kama Polisi na Majeshi na vikundi vya kiharamia vilivyo chini yake.Cha kushangaza zaidi, yanapotokea matukio kama haya hakuna hatua yoyote inayochukuliwa; si kwa upande wa CUF zaidi ya tuwe na subra na tusichokozeke. Serikali ndio kabisa huwa wana pamba za mashikio na kumwa na macho kwa hiyo macho huwa hayafunguki kwa tongo nyingi. Hii inanipa taswira ya kuanza tena kuihakiki nafasi ya binaadamu kwa watawala wetu na kwa viongozi wetu wa chama cha CUF pia. Laiti siogopi kukumbusha machungu yaliyowahi kutokezea, basi ningetaja mfululizo wa matukio ambayo wana CUF wamekuwa wakifanyiwa hakuna lolote lililofanyika Serekali kimya wakifanyiwa wana CUF ila likichomwa kanisa au bar yakuuza ulevi basi Shein tayari yuko kwenye TV na Balozi mkazi a.k.a Baloteli atafoka mpaka atokwe na majipovu ya midomo inaonyesha kuwa kuuliwa rai wa nchi hii ni halali ila kanisa na bar ni haramu.....??
Tukio la juzi, limeongeza tu idadi ya matukio kadhaa ya kiharamia wanayofanyiwa wananchi wa nchi ya Zanzibar wasio na hatia yoyote na makundi hayo maovu yanayosimama kwenye mwavuli wa dola na Chama Cha CCM. Kwa bahati mbaya, wanaohusika na matukio hayo wanajulikana kwa majina na wanapokaa pia wanajulikana. Kwa mfano, matukio ya juzi yalitekelezwa katika mpango nzima ulioandaliwa na watu wanaojulikana kwa majina haswa. Gari lililotumika ni gari la mtu maarufu ambaye kwa jina anaitwa BHAA STYLE. Ndani ya gari hilo, walikuwemo vijana wengi waliokuwa wamevaa fulana za njano ambao waliwashambulia watu hao wasio na hatia yoyote. Ikiwa gari liliotumika linajulikana, kwa nini mmiliki wa gari hakushikiliwa kwa mahojiano.....?? Jeshi la polisi limechukua hatua gani juu ya tukio hili na miliki wa gari anajulikana....?? Nani katika viongozi wa Serikali ukitoa yule wa CUF, katoa kauli juu ya matukio kama haya......?? Jawabu ni hakuna wote wameufyata. Ukiuliza kwa nini iwe hivi. Majibu yanayotoka ndani ya chama cha CUF yanakuwa ni yale yale tuliyozoea kuyasikia tangu mwaka 1992 – ‘tuwe na subira!’, ‘hatulipizi kisasi’! tusichokozeke;!! kwa upande wa CCM wao huwa ndio furaha yao kuwa yes tunaendelea kuwatia adabu hula sikuku yao na kuendelea kupaga wapi tutawahujumu tena.
Kauli kama hizi sio mbaya kwa kweli kwani hata Bwana Mungu anazifurahia sana lakini… nasema lakini inategemea na hali na mazingira yalivyo. Uzoefu wa miaka 20 ya Chama Cha CUF, unaonyesha kuwa wahujumu na maharamia wanaoendelea kuwadhuru wanachama wa CUF wamekuwa wakiuchukulia udhaifu wa kauli kama hizi za viongozi, ili kupata wepesi wa kufanya Uharamia wao. Na ndivyo hivi kila siku wanazidi kufanya tena na tena na tena!!!! na kuendelea kuuwawa na kuuwawa na kuuwawa!!!
Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amehudhuria mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) aliyefariki katika ajali ya barabaraniKatibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad amehudhuria mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) aliyefariki katika ajali ya barabarani iliyotokea wakati akirudi katika mkutano wa hadhara wa chama CUF uliofanyika Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja baada ya gari lao kushambuliwa na janjaweed.
Mwaka 2005, tulishuhudia janjaweed Unguja nchini Zanzibar ilivyo fanya kazi yake, wakiwabaka wanawake nje chochoroni. Sisi wengi wetu tupatao maelfu, tukitishwa na kupelekwa mbio na kikundi hicho kidogo cha vijana waliokata tamaa na maisha na kuwaacha dada zetu hao wakifanyiwa uharamia huo hadharani. Kuna wanaume kadhaa waliobakwa na kupitiwa kinyume na maumbile. Wachilia mbali waliojeruhiwa vikali na wanamgambo hao. Sisi kama sisi, CUF tulichukua hatua gani baada ya kufanyiwa unyama huwo pamija na dada kufanywa mambo machafu.......??? Kosa lisipotolewa hukumu, ikaadhibiwa hupata uhalali na walio tenda hupata guvu zaidi maana huwona ni sawa walio wafanyia ndio huzidi na kutaka kufanya mabaya zaidi maana washakuwa na uhakika kuwa hakuna litakalo watokea wao kwa kufanya machafu haya ndiohubakia kaselelea, na likawa mazoea. Na ndio kama hivi tunavyoona leo. Kila ukikaribia uchaguzi, vijana hawa huwezeshwa kuja kutia adabu wafuasi wa CUF wakiamini hawatafanywa lolote. Tabia ya kosa, huzaa kosa. Vijana hawa wanapofanikiwa kuwatisha katika hatua ya kampeni, Wazanzibari wakakubali kutishika tusiwachukulie hatua, ndipo hawa hawa wanapojitokeza siku ya uchaguzi, wakapiga kura mara elfu kila mmoja. Kisha wasitosheke, wakarudi tena usiku kuiba kura! CUF tunabakia tukikariri uradi wetu wa ‘tuwe na subira na tusilipize kisasi’tusichokozeke ambao nadiriki kusema kuwa hata mungu kwa hali ilivyo sasa haoneshei kuwa anauridhia.mgonjwaNguvu ya vikundi kama hivi hapa Unguja imetokana sana na woga wa wafuasi wa CUF wenyewe woga ile mbaya na viongozi wao pia ndio majoga makubwa madomo tu juu ya kimembari lakini wakishuka basi wananjamba cheche mpaka afike kwake ajikomele. Kama kuna mtu anayebisha juu ya hili, natoa mfano hai. Mwaka 2005, vijana wa janjaweed, walipelekwa Pemba kufanya uharamia kama waufanyao Unguja. Haukutimia mwezi, walikimbia wote wakaja zao Unguja. Nini kiliwakimbiza Pemba.......??? Nini hasa.........chezea wapemba wapole ila hawataki kuhanithiwa.
Jibu liko wazi. Kwa miaka mingi kule Pemba vikipelekwa vikosi vya kuwahiliki wananchi. Tukianzia na ‘Melody’ wale FFU wa mwaka 1995. Wananchi wa Pemba walipoona wanaonewa kila siku na chama hakitoi kauli yeyote, wala si serikali haijali, wakaamua kujichukulia hatua mikononi mwao. Na hiki ndicho kilichowakimbiza janjaweed Pemba miaka ya 2005. Tangu Pemba waamke na kuanza kujitetea, matukio ya kiharamia kama haya dhidi yao, yamepungua au tuseme hakuna.
Lakini kwa vile Unguja, tumeshikana na neno subira huku tukiumizwa na kudhulumiwa kila siku, basi sidhani kama kuna popote tutakapofika zaidi ya kuzidi kupata maumivu ya majeraha ya mashambulizi ya vikosi kila uchao. Kwa vile wahalifu wa jambo hili wanapewa kichwa na wenye uwezo na kauli, na wale ambao wanafanyia wanaonekana kustahamili kila siku, basi sidhanii kama haya yatakwisha.
Na ikiwa hali kama hii itaendelea, na bila shaka inaendelea, ushauri wangu kwa wana CUF ni kuwa wanapokwenda mikutanoni, ipo haja wavae mahelmet na nguo za chuma.
Kufanya hivi kutawapunguzia majanga yatokanayo na janjaweed. Ama kuhusu vitendo vya kuwabaka wanawake wanatoka mikutanoni, ushauri pia ni mwepesi sana, ni kuvalia chupii ‘kufuli’ za chuma na funguo za kufuli hizo zikaachwa nyumbani mpaka watu watakaporudi mkutanoni kwani bila hivyo, wanachama na wafuasi wa CUF watakuwa wahanga wa janjaweed na bahati mbaya, hakuna hata wa kuwatetea!!! au mjipange muwa na gari ambazo hizo ni zavijana ambao wao wanawalinda hao wafuasi wa CUF ili janjaweed wakijaribu kutaka kufanya hujuma zao hao vijana wanakula nao sahani moja wao ni watu kama sisi wanaumia kama sisi akikatwa akaiyona damu inamtoka ataaza kulia kama hanithi na atasahau kama yeye ni janjaweed lakini ikiwa wao wanafanya na hakuna anae wafanyia wao wakasikia maumivu basi unguja tutachezea mikongotona kubakiwa dada zetu mpaka tukome.
Pamoja na hayo namalizia kwa kutoa ushauri kuwa ingawa subira ni njema, ifike siku iwe na mipaka. Ingawa tumesema hatulipizi kisasi, tuna haki ya kujitetea na kujihami. Sawa tusilipize kisasi, lakini TUJIHAMI au WATATUMALIZA!!!

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment