Monday, April 20, 2015

BREAKING NEWS: MZEE HASSAN NASSOR MOYO AFUKUZWA CCM CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA


Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ya nchini Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo
MWENYEKIT WA Kamati ya Maridhiano nchini Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo amevuliwa uanachama wa CCM, kufuatia taarifa zilizopatikana hivi punde. Kwa mujibu wa habari, Mzee Moyo amefukuzwa kutoka chama hicho cha Mkoloni Mweusi Tanganyika na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Magharibi, Unguja vibaraka,watumwa wa Mkoloni Mweusi Tanganyika kupitia kikao chake kilichomalizika leo alaasiri.Atii anadaiwa kukisaliti chama hicho kwa kukiuka maadili, katiba na miongozo ya CCM ila Wazanzibari washa amka wanajuwa sasa kama hichi sio chama cha nchi yao bali ni chama cha Mkoloni Mweusi Tanganyika na watumwa wake wachache wasaka tonga hapa nchini ndio maana sasa wanawafukuza katika chama chao Wazanzibari wasio tii amri tena ya Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Hata hivyo, habari zinasema kuwa mwenyewe (Mzee Moyo…binafsi), hakushitushwa na uamuzi huo na amesema kamwe hatorudi nyuma katika kupigania maslahi ya nchi ya Zanzibar. Mzee Hassan Nassor Moyo ndiye Mratibu Mkuu wa Maridhiano ya nchi ya Zanzibar ya Novemba 5, 2009 yaliyowakutanisha Rais Mstaafu wa nchi ya Zanzibar (awamu ya sita), Dk Aman Abeid Karume na Maaalim Seif Sharif Hamad, ambaye sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar. Maridhiano hayo yameleta faraja kubwa kwa wananchi wa nchi ya  Zanzibar, hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu uliyopita wa mwaka 2010. Kwa muda mfupi baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 wananchi wa nchi ya Zanzibar, waliweza kuishi katika hali ya amani, utulivu na mshikamano na kusahau tofauti zao. Tangu kuanza kwa Serikali ya Awamu ya Saba inayoongozwa na Shein, hali ya amani na utulivu imekuwa ikitoweka (tete) kadiri siku zinavyokwenda mbele hasa Unguja. Shein, mara kadhaa amekuwa akinukuliwa kwamba hayatambui Maridhiano.
Mzee Moyo ambaye ameamua kwa muda mrefu kuungana na asilimia kubwa ya wananchi wa nchi ya Zanzibar, wanaopenda kuiona nchi yao inaendesha shughuli zake za kiutawala na kiuchumi bila kuingiliwa na nchi yoyote, ikiwemo Mkoloni Mweusi Tanganyika. Mzee moyo, kupitia Vikao na Makongamano ya Kamati ya Maridhiano, amekuwa akieleza waziwazi kuwa yeye hakushiriki katika Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 katika kundi la watu 14. Mzee Moyo, anasema kuwa amekuwa katika Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano tangu mwaka 1964 ni kutokana na utiifu, uwazi na kuwa mkweli katika kutumikia nchi yake. Anasema: “Hatukuungana kwamba mmoja ammeze mwenzake…hiyo hapana.” Mzee Moyo anasema wakati mmoja akiwa masomoni nchini Urusi, alipigiwa simu na Mzee Abeid Aman Karume (marehemu Mzee Karume), akimtaka kwenda kushiriki katika mazungumzo ya uhuru wa nchi ya Zanzibar, yaliyofanyika London, Lancaster House. Mzee Moyo amekuwa mwanachama wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) tangu kilipoasisiwa Februari 5, 1957 baadaye Februari 5, 1977 akawa mwanachama wa CCM akiwa na kadi namba 7.
Mzee Moyo si mtu wa kutetereka katika kusimamia kauli yake na kile anachokiamini kwani amekuwa akieleza kwa uwazi kuwa yeye hakubaliani na mfumo wa sasa wa Muungano wa nchi ya Zanzibar na Mkoloni Mweusi Tanganyika. Anasema: “Ni tofauti wakati wa Mzee Karume…sasa vijana wetu wamesoma wanahitaji kuendesha nchi yao,” Pia, anasema: “Mambo ya Muungano yalikuwa ni 11 tu…na sasa ni zaidi ya mambo 36 na yote yameingizwa humo kinyemela.” CCM nchini Zanzibar, miaka miwili iliyopita ilimfukuza uanachama waziri wa muda mrefu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansour Yussuf Himid baada ya kuwa na hoja na fikra tofauti juu ya muundo wa Muungano, hasa kuhusu maslahi ya nchi ya Zanzibar. Mansour, kufuatia hatua hiyo aliamua kuunga mkono juhudi za Wazanzibari wanaohitaji kuona nchi yao inapata mamlaka kamili baada ya kuendeshwa mchakamchaka na Mkoloni Mweusi Tanganyika. Kwa muda mrefu, kauli za baadhi ya viongozi wa Tanganyika zimekuwa zikiashiria na kuonesha kana kwamba nchi ya Zanzibar ni koloni la Tanganyika.
Kauli za kutisha zinazoashiria kuwa ni kweli Tanganyika ni Mkoloni Mweusi mpya kwa visiwa vya Unguja na Pemba, ni pamoja na kauli ya Mizengo Pinda kuwa Zanzibar si nchi, na kauli za hivi karibuni za Samuel Sitta na William Lukuvi. Kauli zinaonekana kuwa mwiba miongoni mwa Wazanzibari. Wahenga walisema: “Ukidharau Mwiba Utakatwa Mguu” Maana yake ni kwamba iwapo bado kuna Wazanzibari hadi sasa wanazipuuza kauli za viongozi hawa Wakoloni Weusi Tanganyika, wasubiri kukatwa mguu. Mzee Moyo, hayuko tayari kuwa dalali wa nchi yake. Hao wanaosubiri ushahidi kamili wapaswa kutambua kuna siku watakuja kujuta. Mzee Hassan Nassor Moyo, kaona mbali.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment