MWENYEKITI WA NEC JAJI MSTAAFU DAMIAN LIBUVA ALHAMISI, APRIL 2, 2015 (( 6;02))
TUME YA Taifa ya Uchaguzi ya nchi ya Tanganyika (NEC) imekubali kuahirisha upigaji Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa iliyopangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu. Sababu zilizoelezwa za kuahirishwa kwa kura hiyo ni kutokana na kutokamilika kwa uandikishaji wa daftrai la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya ‘Biometric Voters Registration’ (BVR). Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo mfululizo wa matamko na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wa demokrasia kwamba zoezi hilo lisingewezekana kwa sasa hasa kutokana kusuasua kwa mwenendo wa BVR. Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam nchini Tanganyika leo kuwa kazi ya uboreshaji daftari la wapiga kura ni ya msingi kabla ya taratibu zote za upigaji kura.
Jaji Lubuva aliyeonekana kuwa mpole zaidi, alisema kwa uzoefu walioupata Njombe, zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura bado halijakamilika katika mkoa huo na mingine iliyosalia. “Hivyo tume haitaweza kuendelea na zoezi la upigaji kura ya maoni na zoezi hilo lililotangazwa hapo awali kufanyika Aprili 30, 2015 limeahirishwa hadi tarehe itakapotangazwa na NEC, baada ya kushauriana na Tume ya Uchaguzi ya nchi ya Zanzibar,” alisema Jaji Lubuva. Kwa nyakati tofauti, vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wananchi wamekuwa wakiishauri NEC na Serikali ya CCM, kuahirisha Kura ya Maoni. Aidha kwa muda mrefu, vyama vya siasa vimekuwa vikimtaka Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika atii makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana na Kituo cha Demokrasia (TCD) kuahirisha zoezi hilo hadi baada ya Uchaguzi mkuu.
Jaji Lubuva alisema kuwa tume yake inaendelea kuboresha daftari la wapiga kura nchi nzima ambapo wanatarajia kukamilisha kazi hiyo ifikapo Julai mwaka huu. NEC ilieleza kuwa baada ya kumaliza uandikishaji wapiga kura wa mkoa wa Njombe watahamia mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara na Iringa. Jana, Jaji Mstaafu Mark Bomani aliishauri serikali kuahirisha kwa muda kura ya maoni kwa ajili ya Katiba Pendekezwa ili kuipa nafasi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendelea na maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Jaji Bomani, alitoa ushauri huo Dar es Salaam nchini Tanganyika wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), na kusisitiza: “Ikiwezekana tuachane na mfumo wa BVR ambao umewapa shida wenzetu wa Kenya na Nigeria.” Akieleza sababu mbalimbali za kutaka kura ya maoni iahirishwe, Jaji Bomani alisema hali ya sasa haiwezeshi jambo hilo: “Sidhani kama hilo litawezekana kwani zoezi la uandikishaji wapiga kura linasuasua.” Aliongeza: “Naambiwa eti mpaka sasa waliokwisha andikishwa hawazidi watu milioni moja…wapo takriban zaidi ya watu milioni 20 wataweza kuandikishwa katika wiki nne zilizobaki....??,” alihoji Jaji Bomani.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO
No comments:
Post a Comment