Jumapili ya tarehe 12 Aprili 2015, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, ameongoza ujumbe mzito wa viongozi, wanachama na wafuasi wa CUF kwenda kwenye jimbo la Kitope, ambako pamoja na mengine amefunguwa matawi mapya manne na baraza mbili za vijana. Kubwa kuliko yote ni kuwa wanachama wapya 400 wamejiunga na chama chetu hivi leo katika eneo hili ambalo lilikuwa likifahamika kuwa ni ngome ya CCM.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera kuashiria kufunguliwa kwa barza moja ya Hatudanganyiki kijijini Upenja.
Ni kweli kwamba mkutano mkubwa wa hadhara ambao tulikuwa tumeupanga kuufanya huko ulizuiwa na jeshi la polisi ambalo awali lilidai kwamba mtu aliyekuwa amekubali kutupa kiwanja, alighairi baadaye.Lakini wakati jeshi hilo likidai hivyo, mmoja wa wanachama wapya aliamua hapo hapo kutoa kiwanja chake kilichoko Kilombero huko huko Kitope.
Mwanachama mpya wa CUF ametoa nyumba yake hii itumike kama tawi la chama baada ya hamashauri ya wilaya kukataa kutoa kibali cha kujengea tawi hilo kijijini Upenja.
Kwa hivyo, kizuizi hasa hakikuwa ukosefu wa eneo la kufanyia mkutano, bali jeshi la polisi kutumikia amri ya mmoja wa kiongozi mkubwa wa seriikali ambaye alidhani kwamba angeliweza kuisukuma CUF kwenye mtego wake wa kuangukia kwenye vurugu.
Sisi tunathamini sana maisha na usalama wa watu wetu na wa wananchi wote wa nchi ya Zanzibar. Ndio maana tuliwashawishi maelfu ya watu ambao tayari walishafika kwenye viwanja vya mkutano kurejea nyumbani kwa usalama bila kuchukuwa hatua yoyote kuitumia haki yao ya kikatiba ya kukusanyika. Na kwa kuwa tuna uongozi kwa maana halisi ya uongozi, watu wetu walitusikiliza.
Ujumbe mkubwa na wa pekee leo kwa viongozi wa SMZ ambao wanalazimisha kuiingiza nchi kwenye machafuko ni kwamba sisi CUF tumefika Kitope na Kitope imefika kwetu. Mageuzi hayazuiliki tena.
Sehemu ya mamia ya vijibwa vya kijani waliomwagwa leo Kitope kwa azma ya kuzuia kufanyika kwa mkutano wa hadhara wa CUF na Balozi Mdogo wa Nchi ya Tanganyika wamesimama na mitutu yao wakifedheheka wameshindwa donge na makunduchi kulizui wimbi la mabadiliko itakuwa kitope Balozi mdogo wa Tanganyika utaibika hii ni Zenji sio Tanganyika shauri yako.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO
No comments:
Post a Comment