Friday, June 10, 2016

WAZANZIBARI AMKENI DALILI ZA KIAMA HIZI HAPA NA KARIBU ZOTE ZINATOKEA ZANZIBAR AU HATA NCHI NYENGINE

Dalili Za Siku Ya Qiyama.
Abdullah ibn Abbas (r.a.) amesema kuwa baada ya kumaliza Hajj ya mwisho (mwaka wa 10 Hijriyyah), Mtume Mtukufu s.a.w.w. alisimama mbele ya mlango wa Ka'aba Tukufu, akiwa ameshikilia komeo ya mlango, huku akiwauliza ma-Sahaba wake: "Je, nikuambieni dalili za siku ya Qayama?" Salman Farsi (r.a.) ambaye alikuwa karibu naye, alisema: "Ndiyo, Ewe Mtume wa Allah swt."
Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema, "Hakika,miongoni mwa dalili za saa, ni kuwa
(1) watu watapuuza sala,
(2) watafuata matamanio yao wenyewe
(3) wataelekeza kujipendelea wao wenyewe, watawaheshimu matajiri,
(4) na watauza Dini yao kwa manufaa ya kidunia
(5) wakati huo roho na moyo wa Muumin itayayuka (kwa huzuni) kama chumvi inavyoyayuka katika maji, kwa sababu ataona mambo yaliyoharamishwa na hataweza kuyabadili."
Salman akasema: "Haya yatatokea, ewe Mtume wa Allah swt?"
Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo, naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi 
mwake."
"Ewe Salman,

(6) wakati huo watawala watakuwa wadhalimu
(7) Mawaziri watakuwa waasi,
(8) na wadhamini (wale waliopewa amana kwa 

kuaminiwa) watafanya hiana,
(9) hakika wakati huo maovu yatakuwa mema 

na 

mema yatakuwa maovu,
(10) wale wafanyao hiana wataaminiwa na 

waaminifu watafikiriwa kuwa si waaminifu;na 

mwongo atasadikiwa,na msema kweli 

atahesabiwa mwongo.

(11) Wakati huo kutakuwapo na utawala wa 

wanawake,
(12) Masuria watashauriwa,
(13) na watoto watakaa juu ya mimbar,
(14) udanganyifu utahesabiwa kuwa ni uerevu
(15) na Zaka itakuwa ni kama kutozwa faini; na 

mateka ya vita (yaani mali ya ummah) yatakuwa 

kama ni mali ya mtu binafsi; na mtu atakuwa 

mjeuri kwa wazazi wake na atakuwa mwema 

kwa marafiki zake,
(16) na wakati huo kutatokea na nyota zenye 

mikia (comets)."
Salman akasema: "Haya yatatokea, ewe Mtume 

wa Allah swt?"
Mtume Mtukufu s.a.w.w. akasema: "Ndiyo, 

naapa kwa Aliyonayo roho yangu mkononi 

mwake."

"Ewe Salman!
(17) wakati huo mwanamke atakuwa mshiriki wa 

mumewe katika biashara,

(18) na mvua itakuwa moto sana
(19) na watu wema watabaki katika huzuni; na 

masikini hawata heshimiwa; na wakati huo 

masoko yatakaribiana,
(20) Tena huyu atasema, "Mimi sikuuza 

chochote, na yule atasema, "Mimi sikupata faida 

yoyote." Kwa hivyo hutamkuta mtu yeyote 

asiyemlalamikia Allah swt.
"Ewe Salman!
(21) tena itatokea iwapo watu 

watawazungumzia 

watawala wao, watawaua, na ikiwa 

watanyamaza kimya, watanyang'anywa mali 

yao, watanyimwa heshima zao, watamwaga 

damu yao na mioyo ya watu itajaa woga; kisha 

hutamwona mtu yeyote ila atakuwa mwoga, 

mwenye khofu, ametishika na ameshstushwa"
"Ewe Salman!
(22) Bila shaka wakati huo mambo fulani 

yataletwa kutoka Mashariki
(23) na mambo fulani yataletwa kutoka 

Magharibi,
(24) Basi ole kwa watu walio dhaifu (wa imani) 

katika Ummah wangu kutokana na hayo; Ole ya 

Allah swt iwe kwa hayo. Wao hawatakuwa na 

huruma juu ya wadogo wao, wala 

hawatamsamehe yeyote aliyefanya kosa. Miili 

yao itakuwa ya wanadamu, lakini mioyo yao 

itakuwa ya mashetani."

"Ewe Salman!
(25) Wakati huo wanaume watawaashiki 

wanaume,
(26) na wanawake watawaashiki wanawake;
(27) na watoto wa kiume watapambwa kama 

wanawake;
(28) na wanaume watajifanya kama wanawake
(29) na wanawake wataonekana kama 

wanaume;
(30) na wanawake watapanda mipando
(31) Hapo tena patakuwepo laana ya Allah swt 

juu ya wanawake wa Ummah wangu." 

"Ewe Salman!
(32) Bila shaka wakati huo Misikiti itapambwa 

(kwa dhahabu n.k.) kama inavyofanywa katika 

masinagogi na makanissa,
(33) na Quran zitapambwa (kwa nakshi na rangi 

za kupendeza n.k.)
(34) na minara (ya misikiti) itakuwa mirefu; na 

safu za watu wanaosimama katika sala zitazidi, 

lakini nyoyo zao zitachukiana na maneno yao 

yatatofautiana."
"Ewe Salman!
(35) Wakati huo wanaume watatumia mapambo 

ya dhahabu; kisha watavaa hariri, na watatumia 

ngozi za chui."
"Ewe Salman!
(36) Wakati huo riba itakuwako,
(37) na watu wata-fanyia biashara kwa 

kusemana na rushwa
(38) na dini itawekwa chini, na dunia 

itanyanyuliwa

No comments:

Post a Comment