Wanaharakati na wadau wa mitandao ya kijamii nchini wamemkabidhi Sh4.5 milioni aliyekutwa na hatia ya kumtukana Rais John Magufuli ili akalipe faini aliyotakiwa atoe na mahakamani kuepuka kifungo cha miaka mitatu. Mshtakiwa huyo, Isaack Habakuki alikutwa na hatia baada ya kukiri kosa la kumtukana Rais kupitia ukurasa wake wa facebook. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemtaka kutoa Sh 7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Mratibu aliyekuwa anakusanya michango hiyo kwa Kanda ya Kaskazini, Diwani wa Levolosi, Ephata Nanyaro amesema jana kuwa wamefanikiwa kupata michango hiyo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii waliyoyaanzisha. "Lengo ni kumsaidia mwenzetu kwa kuwa kupitia sheria hii ya mitandao tunaamini hakuna aliyesalama na sheria hii itawagusa wote, " amesema Nanyaro. Naye, Habakuki amewashukuru Watanzania waliojitolea kumchangia.
No comments:
Post a Comment