
#UN ALIPO TUPO ALIPO TUPO
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa kwenye alama ya bastola iliyofungwa kwenye mdomo wa kutokea risasi ambayo imewekwa mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York kuashiria kukataa matumizi ya nguvu na umwagaji wa damu katika kukabiliana na migogoro duniani.
Alama hiyo ilitolewa kwa Umoja wa Mataifa na nchi ya Luxembourg mwaka 1988.
Maalim Seif siku zote amesimamia njia ya mazumgumzo na amani katika kutatua migogoro ya kisiasa. Picha hii ni ukumbusho wa jitihada zake na msimamo wake usiyoyumba katika kukataa matumizi ya nguvu au fujo na kusimamia amani na njia ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment