MUFTI HII NI KWA AJILI YAKO IKIWA HUJAWAHI KUISIKIA ISIKILIZE KISHA WEWE UTAJUWA VYA KUFANYA
Masheikh wa Pemba wavunja ukimya nchini Zanzibar.
Ujumbe wa ofisi ya Mufti wa nchi ya Zanzibar umefanya ziara
na kukutana na baadhi ya Masheikh Kisiwani Pemba kwa
lengo la kutaka kuzungumzia ati haki ya sasa inayoendelea
kisiwani humo ambapo baadhi ya wananchi hususiana
kuuziana bidhaa na kukataa kuzikana kufuatia stafahamu
iliyotokana na uchaguzi mkuu wa Octoba 25 ambapo
inasemekana kilichofanyika ni dhulma ya wazi wa kupora
ushindi wa Chama Cha CUF na kuwapa Chama cha CCM.
Ujumbe huo umefika Pemba na kuwataka Masheikh watumie
taaluma yao ya dini kuwataka wananchi waondokane na hali
ya kutengana na kuishi kama zamani. Haya soma kilichojiri
katika kikao hicho ambacho Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh
Omar Kaabi alikuwa miongoni mwao.
Katika maelezo yake Sheikh Saleh Kaabi na ujumbe wake
aliokwenda nao wakiwataka Masheikh hao kuilimisha jamii
kuishi vyema kwa upendo na mashirikiano kwa kutumia
hadithi na aya za Quran Tukufu huku Masheikh wakielezwa
kwamba wana umuhimu katika jamii.
Lakini Masheikh hao wamekuja juu na kusema kwamba
hapawezekani kuwa na amani na upendo pasi na haki na
uadilifu kutendeka. Mmoja wa masheikh ambao walipata
nafasi ya kuchangia alisema na kuhoji kua tunawezaje
kuyafikia mafanikio wakati hatujapita katika njia ya
mafanikio...?? Huku akisistiza kuwa uislam hauangaliwi
vipande vipande bali unapaswa kutizamwa kwa ukamilifu
wake ambapo alisema kuwa hatuwezi kuangalia mwisho wa
tatizo tu bali pia tunatakiwa kuangaia na chanzo cha tatizo.
Sheikh huyo alimkabili Sheikh Kaabi kwa kumpa fumbo la
kiswahiki kwamba asitegemee kukoroga kinyesi halafu
akategemea kusikia harufu mzuri puani mwake.
Sheikh mwengine naye alipata nafasi ya kuongea alisema
kuwa Dk Shein kafanya dhulma kubwa na mikono yake
inanuka damu na yeye mwenyewe anajua na kumtaka Mufti
huyo wa Zanzibar Sheikh Saleh Kaabi amwambie Dk Shein
arejeshe haki ya wananchi aliowadhulum ndipo amani na
upendo utarudi visiwani humo.
Shekh Saleh pia alinasihiwa na kuambiwa kua aya na hadithi
alizowatolea masheikh hao aende akawatolee na viongozi wa
serikali kama vile Dk Shein, Balozi Seif na Maalim Seif Sharif
Hamad huenda labda na wao kama binaadam wakafaham na
wakaamua kutenda haki.
Huku Sheikh mmoja naye alihoji ni kwa nini mambo haya
waambiwe wao wasiende kuambiwa hao waliosababisha
matatizo haya ambao ni wenye mamlaka ya nchi na cyomvo
vyake..? Alisema daima viongozi wa dini umuhimu wao siku
zote hujulikana kipindi cha shida tu na matatizo lakini kukiwa
hakuna vitu hivyo na nchi imetulia hawaitwi hata kupewa
asante ingawa juhudi za kuituliza nchi kwa kiasi kikubwa
hufanya na viongozi wa dini.
Katika suala la Mazombi na kamatakamata na utesaji pia
baadhi ya Masheikh katika kikao hicho wamelizungumzia
ambapo aliulizwa Sheikh Saleh Kaabi jee wananchi
watafanyaje ikiwa mtu ambaye hana bunduki na uwezo
wowote anateswa na kupigwa na kudhalilishwa na Jeshi la
Polisi na Mazombi bila ya kosa..??Je ni haram kwao wao
kuchukia tu wakati hatua za kuyakataa hayo zipo tatu kwa
mujibu ya mafundisho ya Bwana Mtume...??
Pia aliulizwa tunawezaje kuwa na mapenzi ya kushirikiana na
watu ambao waliwaweka mashekhe wetu ndani na kujisifia
katika majukwaa ya kisiasa huku masheikhe hao na familia
zao zikiendelea kupata tabu kwa mwaka wa tatu sasa...??
Hapo hapo mmoja wa Masheikhe hao akamwambia
Sheikh Saleh kuwa kutokana na alivo anaamin kua kama
angeamua kusimama usiku na kuwaombea dua tu
masheikh wale basi Masheikh wale wangepata nusra ya
Mwenyenzi Mungu lakini inaonekana hata hilo
limeonekana limemshinda.
Aliendelea sheikh huyo kwa kusema kua watu waliomba dua
nyingi ili kuinusuru Zanzibar na mambo mbali mbali lakini
kuna viongozi wa kisiasa na serikali wakawa wanapita na
kusema kua vi Alamtara vyenu havitowasaidia chochote
(Astaghafurullah) sasa je mtu kama huyu ambaye anadharau
na kuidhalilisha hadi Quran (maneno ya Allah) nae
tushirikiane nae...??
Hakika Sheikh Saleh ambaye ni Mufti wa Zanzibar juzi
alipata wakati mgumu sana ambapo hali kama hii aliwahi
kukutana nayo wakati ule alipokwenda Pemba na kukutana
na wanafunzi wake na kumueleza jukumu lake alilonalo
serikalini ambapo Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho
wakiteseka Magerezani huku yeye akiwa amesalia
madarakani.Masheikh hao wamesema hakuna nusura wala
dua itakayoombwa ambayo itainusuru Zanzibar zaidi ya
waliotenda dhambi hiyo ya dhulma ni kurejesha amana kwa
waliowadhulumu ambao ni wananchi wa Unguja na Pemba.
Sheikh Saleh Kaabi aliinama chini mbele ya wanafunzi wake
na kulia sana kwa uchungu baada ya kuelezwa atajibu nini
mbele ya Allah hali ya kuwa Masheikh wanadhalilishwa
Magerezani na kuthubutu kusimama mbele ya Mahakama na
kuangusha vilio vya mateso na udhalilishaji wanaofanyiwa
haki ya kuwa yeye bado yupo serikalini, hali hiyo ilimfanya
achukue uamuzi wa kutaka kujiuzulu lakini wenye mamlaka
walikataa uamuzi huo na hivyo bado anaendelea na wadhifa
huo wa kuwa ndio kiongozi mkuu wa kidini serikalini.
Haizidi kwa mwenye kudhulumu ila khasara.
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI
TUNASEMA HIVI:
Mtume wetu alisema “MAN TASHABBAHA BIQAUMIN FAHUWA MINHU”
Mtume wetu alisema “MAN TASHABBAHA BIQAUMIN FAHUWA MINHU”
mulikuwa mumuache tu ajiuzu kisha aende akatubiye huko
maana toka mwaka jana yuko bega kwa bega na shein na
haramu zote zifanywazu Unguja na Pemba na
PoliCCM,MajeCCM,MazombiCCM na kuitishwa kura feki na
uchaguzi feki kisha kujitagaza feki serikali feki yeye yumo na
yuko pamoja nao leo ati anajidai kulia, Masheikh wako jela
mwaka wa Tatu lini alisimama akasema mimi kama Kadhi
Mkuu Nalani Vikali na kama Masheikh hawakupewa haki yao
Najiuzulu lini kasema hivyo Mnafiki Mkubwa leo ajitia kulia
nenda kamlilia Allah utubu na utake msamaha kwa Allah na
ushukuru kakuziduwa kabla hujafa pia mwambie Shein
ajiuzulu na arudishe haki ya watu ili Maalim apishwa kuwa
ndio Rais aliye shinda Wazanzibari wanataka haki yao.
No comments:
Post a Comment